Uwezo wa kujenga hoja, kuielewa hoja na kujibu hoja, bado ni tatizo

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Aug 3, 2020
2,035
2,302
Sio humu tu, nenda kwenye mitandao mingi tu. Sikiliza vipindi vya redio, televisheni, maofisini, mashuleni, utajionea ukweli huu,haraka ya kujibu bila kuielewa hoja, kujibu hoja kwa matusi.

Kejeli na upuuzi mwingi. Kujenga hoja bila ushahidi,kutumia lugha chafu au kiswahili kibovu, tabia ya kujifanya kujua kila kitu, hata kwenye ndoa zetu shida ni hii hii. Je tatizo huwa ni nini?

Karibuni kwa michango yenu
 
Sio humu tu,nenda kwenye mitandao mingi tu,sikiliza vipindi vya redio,televisheni,maofisini,mashuleni,utajionea ukweli huu,haraka ya kujibu bila kuielewa hoja,kujibu hoja kwa matusi,kejeli na upuuzi mwingi.Kujenga hoja bila ushahidi,kutumia lugha chafu au kiswahili kibovu,tabia ya kujifanya kujua kila kitu,hata kwenye ndoa zetu shida ni hii hii.Je tatizo huwa ni nini? Karibuni kwa michango yenu
Kazi kweli kweli
 
Tatizo la kitaifa, nadhani imekuja baada ya kudilute elimu kila eneo, huenda ndio sababu, hata wewe hapa kuweka punctuations kwenye paragraph yenye hoja yako umekwama! Inasikitisha sana taifani:(
 
Sababu kuu ni kukosa elimu ya mijadala kuanzia ngazi ya primary hadi chuo.
Watu wameshindwa kabisa kujua namna ya kutoa hoja ,kujenga hoja na kuhimili maoni kinzani.
Shule nyingi primary na sec kwa Sasa hazina mijadala ya wanafunzi

Tumeua debates kila mahali za lugha zote na kuruhusu kudesa vyuo vikuu kabisa, kule chini walimu wameacha bora liende tu so matokeo ndio haya tunayopata. Professionalism ikifa na taifa linakufa kila nyanja.
 
Unategemea na maada husika, mfano mleta maada unaleta uzi wa kushangaa watu zama hizi kusikiliza mpira kwenye redio, ni maada ya kipuuzi kwa kua hukufanya upembuzi kujua vipato vya watu kumudu kununua runinga, upatikanaji wa nishati kwa baadhi ya maeneo, shughuli za watu n.k
Majibu yako yanaonesha au kuthibitisha kilekile nilichokisema,kutoelewa hoja,kuparamia hoja,uwezo mdogo wa kuelewa na kuhimili hoja,na udhaifu mkubwa wa kujifanya kujua kuliko unachojua
 
Tumeua debates kila mahali za lugha zote na kuruhusu kudesa vyuo vikuu kabisa, kule chini walimu wameacha bora liende tu so matokeo ndio haya tunayopata. Professionalism ikifa na taifa linakufa kila nyanja.
Nimesoma chuo mwanzo mwisho sikuwahi kuona debate ya maana zaidi nilikuwa naona ni hotuba za walio meza kuu
Mic
Sec hasa hizi za kata hata zile za vipaji siku za debate ndio siku za mitihani na remedials hapa lazima shida ipatikane
Ukiua elimu umeua Kila kitu
 
Asante kwa maoni yako
 
Majibu yako yanaonesha au kuthibitisha kilekile nilichokisema,kutoelewa hoja,kuparamia hoja,uwezo mdogo wa kuelewa na kuhimili hoja,na udhaifu mkubwa wa kujifanya kujua kuliko unachojua
Wewe ni mpuuzi tu, jambo la kipuuzi usitegemee kapakwa mafuta kisogoni ili kuku pet pet, beside si kila unaloshangaa wewe lazima liwe mshangao kwa wengine. Endelea kukaa tu kwa wazazi ukishangaa wanaosikiliza redio.
 
Sababu kuu ni kukosa elimu ya mijadala kuanzia ngazi ya primary hadi chuo.
Watu wameshindwa kabisa kujua namna ya kutoa hoja ,kujenga hoja na kuhimili maoni kinzani.
Shule nyingi primary na sec kwa Sasa hazina mijadala ya wanafunzi

Hili ni tatizo kubwa sana
Vijana wetu wa sasa hawawezi kujieleza, wakiulizwa jambo wanakuwa na jaziba au kujibu bila kutumia akili & maarifa na hivyo kushindwa kujenga hoja; ukihudhuria Interview utawahurumia na hata kushangaa kuwa wamepitaje hadi kufika hapo. Baadhi ya mada na uchangiaji mwingine wa hovyo kabisa unao uona hapa jukwaani, ujue ni wa vijana tena waliosoma .....
 
Tatizo la kitaifa, nadhani imekuja baada ya kudilute elimu kila eneo, huenda ndio sababu, hata wewe hapa kuweka punctuations kwenye paragraph yenye hoja yako umekwama! Inasikitisha sana taifani:(
Inashangaza sana, huu ni mfano sahihi wa msemo, " nyani haoni kundule " :D
 
Back
Top Bottom