UVCCM Zanzibar wapingana na tamko la CCM Taifa kuomba radhi kuhusu mabango ya ubaguzi

Wachezee tu hii amani, mmoja wapo atakapo andika barua IS kuomba msaada ndio watajua ubaya wa dhambi ya ubaguzi
Mkuu nilishasema hapa kuwa hawa jamaa wa ISIL, ALSHABAB, ALQAIDA na wengine wa aina hiyo wanapenda sana kwenda kuweka makazi penye migogoro kama ya Zanzibar. Jee wakija hapo huku bara tunaposhabikia ubakaji huu wa demokrasia tutapona kweli?
Tunacheza na mwiba mguuni
 
Mkuu nilishasema hapa kuwa hawa jamaa wa ISIL, ALSHABAB, ALQAIDA na wengine wa aina hiyo wanapenda sana kwenda kuweka makazi penye migogoro kama ya Zanzibar. Jee wakija hapo huku bara tunaposhabikia ubakaji huu wa demokrasia tutapona kweli?
Tunacheza na mwiba mguuni
ukweli ni kwamba ccm wanachokifanya kule zanzibar ni cha aibu. hakistahili kuwepo kabisa kwenye dunia hii iliyostaarabika.
 
Nilikuwa sijuwi kuwa BEN NKAPA ndiye mfitini MKUU.. DU?
Kama unakumbuka mauaji ya Januari 26/27 mwaka 2001 yalipata baraka zake yeye na ni yeye ndie ambae anahofia kurudiwa na sheria za jinai iwapo upinzani utaongoza serikali hapa Zanzibar.
 
OMBI
******
RAIS WETU MAGUFURI NYAKATI HIZI NI NYAKATI ZA UTAWALA WAKO KAMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
RAIS WETU MCHA MUNGU NA MKWELI DAIMA,TUNAKUOMBA LIMALIZE HILI KWA BUSARA ZA HALI YA JUU,MAALIM SEIF NI MTANZANIA,ALKADHALKA DK SHEIN VILE VILE!,KWA NINI IWE SHIDA INGALI MAJESHI NI YA MUUNGANO,POLISI NI WA MUUNGANO,KWA NINI IWE SHIDA?
MR MAGUFURI ITS YOUR TIME NOW!
THE WORLD IS WATCHING YOU!!
ARE YOU STABLE AS YOU OR NOT!
GOD BLESS YOU TOO!
====================


Hawezi kwenda kinyume na GENGE lao. Ukitaka kujua angalia Gbagbo wa kwetu hata aibu zimeshamtoka
 
awali ni awali tu na wala hakuna awali mbili , kiukweli msimamo wa ccm na akina seif idd ni ule ulio kwenye lile bango , mimi nalitambua lile bango kama ndio msimamo halali wa ccm .
 
Fikra ya leo kwa kifupi:

Kwanza: Jana kulizagaa taarifa za Maalim kumuandikia barua Pope Francis ili aingilie kati kutafuta suluhisho la uhuni uliofanyika Oktoba 28 na kuitia Zanzibar katika mkwamo wa kisiasa na kiuchumi.

Kinachozungumzwa sana na wasiojielewa ni kunasabisha udini na utamaduni wa Zanzibar ambao umejengeka kwa misingi ya dini ya kiislamu. Walichosahau hapa ni mambo mawili:

1. Ya kuwa Maalim Seif alifanya hivyo kwa sababu mkubwa wa fitna ya mkwamo huu ni mkatoliki, ambae ni Ben Mkapa. Maalim ameliona hili na kaitumia fursa ya imani ya dini ya Ben Mkapa ambayo inangozwa na Pope Francis kama ni njia ya kumnasihi ajivue na dhambi ya kufitini siasa za Zanzibar.

2. Ya kuwa chama cha CUF kama vyama vyote hakina udini. Hivyo suala la Maalim kumuandikia barua Pope Francis ni njia mojawapo ya jitihada za kidiplomasia anazochukua kutafuta suluhu kwa njia ya amani, na pia ni kuonyesha kwamba anaheshimu dini ambazo yeye mwenyewe sio muumini. Kwa hivyo watu wanaopita wakibeza wanaonyesha wazi kwamba akili zao ni finyu sana na hawana upeo wa kuelewa kwa nini Maalim Seif kafanya hivyo.

Pili: Jana kulitokea kituko cha mwaka pale mzee wa IN BIOLOGICAL, Shaka Hamdu shaka alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa taarifa kwamba lile bango (kiukweli halikuwa moja, tuliyaona mawili) eti limetengenezwa na wapinzani kufanya propaganda?!

Hivi ajiulize, imefikiaje tarehe ya juzi 12/01/2016 CCM ngazi ya Taifa kupitia Mkuu wa Mawasiliano ya Umma, Daniel Chongolo, watoe tamko la kuomba radhi kwa picha iliyotengenezwa na wapinzani?! Anataka kutuaminisha kwamba CCM Taifa ni vilaza na hawana wataalam wa ICT ambao wana uwezo wa kupambanua hilo kuliko yeye mtaalam wa IN BIOLOGICAL ?!

Hili la Shaka ni la kichekesho kweli kweli, na inatufanya tuanze kuamini kwamba ule msemo wa “Wamegeuka samaki sasa walana wao kwa wao” tuanze kuulekeza upande wao. Iweje chama kimoja wanakuja na rai mbili tofauti, tena moja kutoka ngazi ya juu kabisa, na nyengine kutoka kwa mtaalam wa ICT kipimo cha IN BIOLOGICAL........

Mwisho, nakutakieni ijumaa njema na mapumziko mema ya mwisho wa wiki.

Ahsanteni.
Mkuu nikusahihishe kidogo,Ben ni mkristo wa dhehebu la anglikan na siyo katoliki
hata hivyo Ben ni wa kutoka bara iweje aheshimiwe na kukubali kuvunja amani yenu huko
kisiwani kwa kisingizio cha Ben?Wanafiki wamejazana hukohuko zanzibar,na wengi ni wa dini ya kiislam
na si wakristo,ila wanajifanya wanapelekeshwa na wabara.Siku nyingi na mimi nilikuwa nikiamini hivyo
lakini toka nilipouona unafiki wa wazanzibar kwenye bunge maalum la katiba
basi ndo nikajua,wavurugaji wa amani zanziba ni wazanzibar wenyewe akina Ben wanatumiwa kama ngazi.
Na take it from me,vurugu zanzibar zikianza watakaoumia ni wakristo maana hili linaanza kuonyesha
wazi mgawanyiko.
Papa hana mamlaka yoyote juu ya zanziba au tanzania japo anaweza kukemea kama marekani na mataifa mengine
yanavyokemea.Anatajwa Ben,sijui kama wazanzibar mkianza kulipuana kuna atakayethubutu kwenda kulipua nyumbani kwa Ben,
huenda ni kweli amechangia tunayoyaona lakini nashauri hekima itumike maana zanziba ni yenu na viongozi wenu
kama ni adhabu wapeni viongozi wenu na siyo kuwalaumu watu wa bara.
 
awali ni awali tu na wala hakuna awali mbili , kiukweli msimamo wa ccm na akina seif idd ni ule ulio kwenye lile bango , mimi nalitambua lile bango kama ndio msimamo halali wa ccm .
HAKIKA NI KWELI TUPU;-
LILE BANGO LIMEONYESHA UHALISIA WA CCM,KIFIKRA NA KIMTAZAMO.
in fact limekivua Nguo chama tawala.
 
Umesema tatizo la amani ya zanzibar ni huyu mkapa .juzi alizungumza na mh.raisi magufuli alitoka ndani na furaha .na alidai kama raisi anataka kumpa kazi yoyote ampe .sasa bora apewe hili la zanzibar ,maana mchawi mpe mtoto alee
 
Mkuu nilishasema hapa kuwa hawa jamaa wa ISIL, ALSHABAB, ALQAIDA na wengine wa aina hiyo wanapenda sana kwenda kuweka makazi penye migogoro kama ya Zanzibar. Jee wakija hapo huku bara tunaposhabikia ubakaji huu wa demokrasia tutapona kweli?
Tunacheza na mwiba mguuni
Mkuu hawa jamaa wanataka sana waitawale East Africa na kwa sasa hawapo Tanzania tu na hawana haja na Rwanda na Burundi kwa vile migogoro ya wao kwa wao Tutsis na Hutus ni matatizo tosha.

Tanzania inawapa tabu kwa vile hawajapata support ya Local Muslims mpaka sasa hivi na nina imani kubwa hawatopata support. Mind you hawa hawawezi kuingia bila ya suport ya locals. Kinachotia wasi wasi ni huu uonevu wa wazi wa waislamu ndani ya nchi hii na uporwaji wa demokrasia ambayo hard core muslims wanaichukulia ni siasa za Kikafiri. Tatizo ni kuwa CCM hiyo demokrasia hawaitaki ukijumlisha na uonevu wa waislamu, hiyo ni lethal combination. God forbids, lakini naona kuna chance ya hawa jamaa kujiingiza hapa.
 
Unajua hawa jamaa naona wanaendelea kutapatapa.. Ilikuwa mwinyi adui yao mkuu mpaka dua amesomewa.. kuna kipindi karume alikuwa ni kafiri mkubwa sana kwani alisababisha mauaji na watu kufa hata Dr salmin hakufanya kitu hico lakini hivi sasa Karume ni kipenzi chao na wanamuona mkombozi.Walikuwa wanalilaani kanisa katoliki kuwa ndiyo sababu ya Zanzibar kuwa vile hivi sasa wameandika barua kanisa katoliki. Hivi karibuni hapa Zanzibar nzima kulikuwa na harufu nzuri ya udi unaochomwa na CUF na dua kila sehemu wanamuomba m/mungu au wanamshtakia m.mungu kwa yaliyotokea Zanzibar na viongozi wa CCM waliombewa dua kali kali.Lakini leo wameandika barua kwa papa kumuomba asaidie mgogoro wa Zanzibar! Je nina wauliza hivi Imani yao kwa mwenyezmungu waliyekuwa wakimuomba wiki chache zilizopita imeondoka?

PS Hili nataka mliweke moyoni Seif Sharif Hamad hatokuwa raisi wa ZANZIBAR milele... kwani hii chuki iliyokuwapo Zanzibar hivi sasa baina ya upemba na uunguja yeye ndiyo chimbuko kunako mwaka 1985 baada ya mwinyi kupewa kugombea uraisi kuliko yeye kwani alifikiria Nyerere atalipa fadhila ya kuvujisha siri. Na matokeo yake ili akaeneza propaganda ya kuwa hakupewa uraisi kwa sababu si mpemba.
 
Back
Top Bottom