Utumwa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge wake

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,447
Ndugu wa jukwaa,

Ikiwa ni jumatatu ya blue, napenda kuleta bandiko hili linaloeleza udhaifu wa bunge letu kwa mujibu wa katiba yetu. Ikiwa ni kukubaliana na Bw. Paschal mayala kuwa" bunge la letu ni huru kwa mujibu wa katiba"


1. Bunge letu lilianzishwa kwa ibara ya 62(1) na katiba hivyo lina sehemu mbili yaani Rais na Wabunge.( utumwa unaanzia hapo)

2. Bunge linafunguliwa na kuvunjwa na Rais badala ya spika. Ibara ya 91(1)

3. Bunge linaitishwa na Rais badala ya spika ibara ya 92(3)

4. Uhai wa bunge badala ya wabunge ibara ya 65(1&2)

5. Aina ya wabunge ibara 66 pia inaonesha utumwa uliopo; mwanasheria mkuu wa serikali kama mbunge anayetunga sheria pia anatelekeza sheria kama serikali vilevile bado ni sehemu ya muundo wa uteuzi wa majaji halafu anabishana nao mahakamani tena. Anaendelea kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri. Jamani hii si shida hasa kwenye bunge anapotumika kama mshauri wa masuala ya kisheria?

6. Wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais ambao mwaka 2000 wwaliingizwa kwenye bunge kwa hoja ya Rais kupata wataalamu wa kumsaidia pamoja na kusaidia bunge katika masuala ya kitaalamu. Je, si utumwa unaopelekea kupitisha bungeni mambo yanayolenga kuipendelea serikali?

7. Wabunge wa viti maalumu mimi nawatazama kama watumwa wa vyama vyao mfano wakati wa mgogoro wa CUF. Kwani wanatokana na huruma ya chama kama si upendeleo. Nilitazamia kuwaona kama wagombea wenza majimboni.

8. Wabunge pia kuwa sehemu ya mawaziri kwa ibara ya 51 na 54 ya katiba. Hapo hatuwatazami wabunge kama watumwa wa sserikali kwani kazi aliyopewa na wananchi ni kuisimamia, kuikosoa na kuishauri serikali; mbunge anafanya kazi ya kuendesha serikali ili naye akoselewe, ashauriwe na kusimamiwa na wabunge wenzake, je. Haki ya wananchi kuwakilishwa iko wapi?

Isitoshe, mtu ambaye ni waziri na mbunge aanapata mishahara 2, posho ya bunge na serikali, gari ya bunge na serikali, vyeo viwili vya uongozi wa umma ktk mihimili tofauti.
Hatuoni ni mgongano?

9. Utumwa wa wabunge wetu pia unaoneshwa na wao wenyewe wakati wakati wa nia ya kubadili katiba au sheria ambao hutegemea miswada ya serikali. Lkn pia bunge halina kanuni ya kuwalazimisha wabunge kuleta miswada binfsi. UK (house of commons) wanakanuni za kumsaidia mbunge kuleta mswada mfano droo n.k kwa wabunge kuleta mswada, pia imeonekana serikali kuwatumia wabunge kuleta miswada yao.

Hapa kwetu Tanzania mpaka sasa ni mbunge mmoja wa ccm aliyepeleka mswada 1 binafsi ikiwa. hivi karibuni CHADEMA na wabunge wake wameomba mabadiliko madogo ya katiba na sheria Kupitia Rais kama mkuu wa serikali ili apeleke mswada bungeni. Je, CHADEMA wenye wabunge 70 hawawezi kupeleka mswada? hata kama utashindwa lkn ndiyo kazi yao.

10. Utumwa pia upo kwenye utendaji wa bunge letu kwenye ibara ya 62(3), 99(1&2), 97 n.k;- bunge halipitii mikataba yote isipokuwa baadhi, bunge linapotoa azimio la kumuunga mkono Rais, kusaini au kukataa sheria, bunge kutojadili baadhi ya sheria mpaka Rais aagize. Ibara ya 94 inaminya uhuru wa bunge kuamua mambo kama nchi kwa uzito wa kura badala ya wingi kwani inatoa nafasi kwa baadhi ya mambo kuwa 2/3 ya kura badala yote.


11. Idadi ya wabunge kutoka Zanzibar pia inaashiria bunge lisivyo na nafasi shirikishi ya pande mbili za Muungano kwani idadi ya wabunge 5 ni ndogo hivyo kupelekea hata kero za muungano kutokuzungumzwa kwa mapana hatimaye kuisha au kusadia kubadili aina ya muungano kutoka mabunge mawili kwenda moja au nchi moja bunge moja.

12. Watumishi wa bunge wanateuliwa na rais, rejea ibara 87 na 88. Uteuzi wa katibu wa bunge na sekretariat yake vyoemte chanzo ni Rais. Je, uhuru wa bunge kama muhimili uko wapi? Serikali na mahakama zina tume ya utumishi ambazo uratibu ajira, idadi, nidhamu na mishahara yao.

13. Ukaazi wa wabunge, nchi hii inaonesha wabunge wetu si wakaazi wa majimbo yao si sehemu ya wakaazi bali wapiga kura wa eneo hilo lazima tukubaliane kuwa mbunge anapokuwa mkaazi wa eneo lake haimuondolei haki yake ya kikatiba kwenda sehemu yoyote ya jamhuri. Tumeshuhudia wengine wakija wakati wa uchaguzi baada ya muda mrefu wa ukaazi katika eneo hilo pia hata wabunge kuwa walowezi wa majimbo ya wengine na kurudi majimboni mwao kwa ajili ya ziara, nikutano au vikao na matukio makubwa pengine hadi uchaguzi unaofuata. Huu ni utumwa wa makazi kwa wabunge wetu wanaowajibika kwa wananchi wa jimbo lake

14. Utumwa wa bunge letu pia unaonekana pale linaposhindwa kuwaita viongozi wa vyombi vya kitaifa, mashirika au tume za kitaifa kuonekana bungeni kwa ajili kuwasilisha taarifa zao au kufanya mapitio ya utendaji wao katika vikao vya bunge zima ili kuruhusu wananchi kuelezwa kwa undani, kushughulikia kero zao, kushauri na kutoa mapendekezo yao kupitia wabunge( nchi ambayo madaraka ni mali ya wananchi kupitia bunge)

15. Bunge limefungwa na ibara 75 katika mgawanyo wa majimbo kwa kuacha zoezi chini ya NEC na rais badala NEC na wabunge ili kuruhusu wananchi kuhusika katika maamuzi ya mipaka ya uchaguzi kuliko kufanya maamuzi bila kibali cha watu kwa wawakilishi wao.

16. Madaraka ya Spika yamefungwa na uwepo wa Rais kama sehemu ya bunge. Kama uhitishaji wa bunge, kufunga bunge hata uhairishaji wa bunge bado hoja inatoka kwa serikali. Spika hawezi hata kuteua watendaji wa bunge achilia kamati za wabunge. Inaonekana hata Spika hana sehemu ya utendaji kama mhimili pale inapohitajika badala ya kumuona spika kama kibaraka wa Rais.

Ukomo wa spika kiuongozi ni changamoto kwa kuwa bunge halifi. hivyo, watendaji wa bunge wanakuwepo ila spika hayupo; inaonesha kazi ya spika ni kuongoza vikao vya bunge tu. Pia Spika anapokuwa mbunge inamuondolea nafasi ya kutenda haki bungeni.

17. Ibara ya 67 inaeleza sifa za mtu kuwa mbunge. Ibara ndogo ya 1>b inamtaka lazima awe ndani ya chama cha siasa na wakati si lazima nchi hii kuwa mwanachama wa ushirika wowote ile hali haendi kuwa kiongozi wa ushirika ila watu watakaomtuma( wapo wanaodhaminiwa na chama pia wawepo wanaodhaminiwa na wananchi husika) kipengele hiki kinamkosesha mwananchi kugombea ubunge ktk kuwakilisha wakazi wenzake.

Pia ibara ya 67(3) inamnyima mbunge kugombea Urais ikiwa yeye ni mgombea wa ubunge. Inapaswa kutambuliwa kuwa, kugombea si mgongano wa maslahi na si faida kwa umma wala si hasara kwa umma kwani hatumii fedha za umma, isipokuwa, utakuja baada ya kuchaguliwa.

18. Ukomo wa ubunge unaotajwa na ibara ya 71(1} hasa f) inawanyang'anya wananchi waliochagua mbunge na bunge kukosa mjumbe kutokana na mbunge kupoteza haki ya kuchaguliwa ambayo ni mali ya mchaguliwa na wachagua kwa mantiki kuwa, anawakilisha watu wenye itikadi na mashirika tofauti hivyo mwakilishi hawezi kubanwa na itikadi ya ushirika anapowakilisha bungeni kufanya hivyo linafuata maagizo ya chama na wakati si jukumu lake.

Napenda kuwasilisha.
 
Inawezekana tena bunge limelazimishwa kundelea? Tuliambiwa na katiba kuwa akidi ya mkutano wa bunge ni nusu ya wabunge wote, je 150 ni nusu ya wabunge ambao ni zaid 300?

Tusaidiane kueleweshana pliz
 
Kwanza ni muhimu ufahamu hoja unayotaka kujadili kuliko kurukaruka kama kunguru? Ukitaka kufaidi raha ya uchambuzi lazima ufahamu kile unachotaka kukichambua, vinginevyo kaa kimya kama wengine. Fisi alipoona mkono wa binadamu anayumba kwenda mbele na nyuma alitegemea ungedondoka muda si mrefu, lakini mwisho wa siku alikufa na njaa.
 
Kwanza ni muhimu ufahamu hoja unayotaka kujadili kuliko kurukaruka kama kunguru? Ukitaka kufaidi raha ya uchambuzi lazima ufahamu kile unachotaka kukichambua, vinginevyo kaa kimya kama wengine. Fisi alipoona mkono wa binadamu anayumba kwenda mbele na nyuma alitegemea ungedondoka muda si mrefu, lakini mwisho wa siku alikufa na njaa.
Ndugu, naamini sijui kuchambua ninachokifahamu ila naweza kuandika nisichokijua I'll nifundishwe na kuelewa.
Mimi ni fisi ninayetamani hiyo nyama idondoke na ninamini itadondoka nile.
Prove me wrong.
Angalau tutaelewa hivyo ndivyo tunapaswa kuishi.
Karibu mkuu
 
Kwanza ni muhimu ufahamu hoja unayotaka kujadili kuliko kurukaruka kama kunguru? Ukitaka kufaidi raha ya uchambuzi lazima ufahamu kile unachotaka kukichambua, vinginevyo kaa kimya kama wengine. Fisi alipoona mkono wa binadamu anayumba kwenda mbele na nyuma alitegemea ungedondoka muda si mrefu, lakini mwisho wa siku alikufa na njaa.

Hoja yako ni nini hapa?
 
Hoja yako ni nini hapa?
Ana mengi
Kwanza wengi inaonekana ama wanaogopa kuchangia hoja hii au wanataka kujifunza zaid.

Ukisoma maelezo yake na majibu yangu yanarandana.

Inawezekana anajua nini nimemaanisha katika hoja hii hivyo ananikatisha tamaa.

Hoja inayohusu bunge wengi wanaogopa lkn pia hii hoja haiko kishabiki ila kitaaluma.
Tunahitaji taaluma na uzoefu WA masuala ya kiungozi ndani na nje ya nchi.

Tukiondoa huo utumwa WA bunge utaakisi matokeo makubwa ya nchi yetu na kila MTU mwenye madaraka ataumia.

Tuendelee kueleweshana
 
Hata minofu unahitaji kutafuniwa?
Wow nilijua wewe ni extraordinary people and hard to deal with

Kumbe kuna minofu halafu unasema hoja haieleweki!


parables
 
Kama bunge ni mtumwa basi watanzania wote ni watumwa
Katiba imetafsiri vizur haki zetu lkn ikaweka mipaka ambayo haiathiri haki ya mwingine.

Tunaposema bunge letu lina utumwa tunapata maswali
Je,nani anatumikiwa ?
Kivipi linatumika kwa kuelekezwa na mtawala au vinginevyo?
Kama bunge ni Mali ya wananchi kwa nini hatupewi nafasi?

Hotuba ya Leo ya Spika umeisikia?

Maoni ya wabunge umeyasikia? Hasa halima na peter?

Kwa nini hawakuleta hoja, bunge liazimie mambo kadhaa ili kuishinikiza serikali kuchukua hatua?

Mifumo yetu ndiyo inalifunga bunge.


Mfano, hivi Mme bwege si mtumwa WA mkewe?
 
Hoja yake ni kwamba tuna Bunge ambalo ni "mtumwa" anayehitaji kukombolewa! Anahitaji uhuru zaidi. Yaani, tubomoe mfumo wa Bunge na kuujenga upya.
Sawa, je ni takwa LA watanzania?

Inawezrkana hawaoni ninachokiona Mimi.

Tutaujenga vipi huo mfumo?

Tueleweshane
 
Katiba imetafsiri vizur haki zetu lkn ikaweka mipaka ambayo haiathiri haki ya mwingine.

Tunaposema bunge letu lina utumwa tunapata maswali
Je,nani anatumikiwa ?
Kivipi linatumika kwa kuelekezwa na mtawala au vinginevyo?
Kama bunge ni Mali ya wananchi kwa nini hatupewi nafasi?

Hotuba ya Leo ya Spika umeisikia?

Maoni ya wabunge umeyasikia? Hasa halima na peter?

Kwa nini hawakuleta hoja, bunge liazimie mambo kadhaa ili kuishinikiza serikali kuchukua hatua?

Mifumo yetu ndiyo inalifunga bunge.


Mfano, hivi Mme bwege si mtumwa WA mkewe?
Haina noma faza
 
Back
Top Bottom