Jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga na kuimarisha Tanzania Mpya zitafanikiwa endapo utamaduni mpya wa Kitanzania utajengwa na kutiliwa mkazo.
Utamaduni huu ni wa kuwa na maadili ya Kitanzania (Tanzanian Ethics), yaani tujenge Adili ya Kitaifa ( Ethical Nationalism) badala ya kuimba tu Uzalendo (Patriotism).
Kwa kipindi Taifa hili lilipoifanya Elimu kuwa kipaumbele, iliundwa Wizara ya Elimu na Utamaduni.
Kwa kipindi hiki cha serikali ya Awamu ya Tano, kipaumbele ni kuimarisha Utawala Bora.
Hivyo ili kufikia lengo kuu la utawala bora inabidi iundwe Wizara ya Utawala Bora na Utamaduni. Kwa hiyo Mhe.
JPM na Timu yake na Watanzania kwa ujumla tuanze safari ya kujenga Utamaduni wa Utawala Bora unaoakisi (Reflect) matarajio (expectations), Historia na Tunu za Taifa la Tanzania.