BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,810
Wataalamu wa afya wamesema tatizo la mvurugiko wa homoni ‘hormone imbalance’ ni chanzo kikubwa kwa mwanaume kukosa nguvu za kiume na mwanamke kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa.
Hata hivyo, wengi wamekuwa wakikimbilia kutumia dawa badala ya kuwaona wataalamu hali inayochangia kukuza tatizo na kusababisha kukosa kabisa nguvu za kiume na hamu ya tendo.
Hayo yamesemwa wakati uwepo wa dawa zinazouzwa mitandaoni hata mitaani zikidaiwa kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo kwa wanawake ambazo ni za kupaka, kumeza, kutafuna na kujifukiza.
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni katika mahojiano maalum, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya Kishiriki cha Sayansi Muhimbili (MUHAS), Fredrick Mashili alisema licha ya tatizo hilo kuwakumba zaidi wanawake, limekuwa likiwapata wanaume na ndiyo chanzo cha wengi kukosa nguvu za kiume.
Mtaalamu huyo wa fiziolojia ya homoni na mazoezi alisema mvurugiko wa homoni husababishwa na mambo mengi, msongo wa mawazo ukiwa chanzo kikuu.
Wanawake
Alisema wanawake wamekuwa wakikumbwa na tatizo la ukavu wakati wa tendo na wakati mwingine kukosa kabisa hamu na hiyo husababishwa na kutozalishwa kwa ute wa kutosha.
“Ute kwenye mzunguko wa mwanamke utengenezwaji wake na mabadiliko yaliyopo kwenye uke asilimia 99 yanafanywa na homoni, kwa sababu katika mzunguko wa mwanamke ule ute unabadilikabadilika kwa kiasi na kiwango jinsi ulivyo hiyo yote hutokana na homoni.
“Mzunguko huo unaweza kubadilishwa na msongo wa mawazo (stress) vpi kwa sababu za kisaikolojia inaingia kwenye ubongo inafanya mabadiliko yanayobadilisha mfumo mzima wa utengenezaji wa homoni,” alisema.
Dk Mashili ambaye ni daktari bingwa wa fiziolojia ya homoni alisema iwapo msongo wa mawazo utaathiri homoni zinazohusika na kazi hiyo kuna uwezekano wa kupungua kwa kasi ya utengenezaji ute na hii itachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwake.
“Stress ina nafasi kubwa, mwanamke anaweza akawa na mawazo kuhusu kazi, watoto, pesa chochote kile kinacholeta msongo kwa kiasi kikubwa kinaweza kuathiri mfumo wa homoni na kumpa msongo na kitu kikubwa kinachoathirika ni homoni,” alisema.
Hata hivyo, Dk Mashili alisema homoni ya estrogen inayochagiza hamu ya tendo huanza kutengenezwa kwa mwanamke akiwa na umri wa kati ya miaka 14 mpaka 15 na huanza kuisha kipindi cha kukoma kwa hedhi (menopause) anapofikisha kati ya miaka 45 mpaka 55.
Wanaume
Dk Mashili alisema mwanaume anapopata tatizo la kuvurugika kwa homoni kwa chanzo chochote kile, kinachoathirika ni hamu ya kibaolojia (biological sexual drive) ambayo humwendesha kupata nguvu za kiume.
“Mwanaume akiwa na stress hafikirii tendo la ndoa hivyo, ile hamu ya kibaolojia inakuwa haipo tena. Kuna watu wamejikuta wana tatizo kutokana na stress tu ambazo zimeharibu homoni na huishia kutafuta dawa badala ya kumuona mtaalamu,” alisema bingwa huyo.
Daktari huyo anasema kuna ulazima kwa wanaume kuuelewa huu mzunguko na kufahamu vitu vinavyoweza kuathiri ni homoni na kwenda kwenye afya ya uzazi ambacho ni kitu muhimu kukijua ili kutafuta tiba sahihi itakapohitajika.
“Unaweza kujiona una tatizo kwa sababu umekutana na hicho kitu kumbe ni kutokana na hicho kipindi. Hiyo huenda labda kuna kitu au vitu vimetokea katika maisha yako vimekusababisha hali hiyo ya kibaolojia na kuleta shida, vitu ambavyo vipo sana katika maisha ila wengi hawajui,” alisema Dk Mashili.
Alisema pamoja na vyanzo vingine vya kukosekana kwa nguvu za kiume ikiwemo magonjwa kama kisukari na presha, kuvurugika kwa homoni ya kiume (testosterone) humfanya mwanaume kutokuwa na hamu ya kibaolojia hivyo hawezi kuwa na nguvu za kiume sawasawa.
Matibabu
Akielezea matibabu ya tatizo hilo, Dk Mashili alionya isiwe kukimbilia kutumia dawa bali yaangalie kwanza msaada wa kisailokolojia.
“Hapa matibabu yake ni kutafuta namna ya kupambana na hilo tatizo kwa kuliondoa kwa kutumia wataalamu kulingana na vipimo. Kwa kiasi kikubwa ushauri unaweza kubadilisha kiwango cha homoni, kubadilisha ute au vyote na mambo mengi ambayo yanakuwa yanaendeshwa na homoni,” alisema Dk Mashili.
Mtaalamu wa afya ya akili na mwanasaikolojia kutoka Taasisi ya Mental Health Tanzania, Semeni Lukaga alisema matatizo kwa binadamu yeyote yanaenda kuathiri mwili kibaolojia.
Alitolea mfano mwanamke mwenye madeni mengi mfano ya vicoba ambaye hajui wapi atapata fedha akisema wengi hupata msongo wa mawazo ambao huwa chanzo cha kukosa hamu ya tendo la ndoa.
“Amekwenda kwenye vicoba kakutwa na hayo matatizo cha kwanza kitaalamu, mwili huwa unapokea matatizo kwa maana kuna ubongo ambao unatema zile sumu, kama ana hasira ina maana zile hasira kuna homoni za sumu ambazo zitatemwa na ubongo zitasambaa mwilini kupitia mfumo wa neva.
“Kama ni msongo wa mawazo utatembea mwilini na kusababisha hamu ya kula kupotea, utasababisha msisimko kutotokea kwa kuwa misuli haiwezi kufanya kazi, hivyo muunganiko wa matatizo na kutofanya tendo la ndoa vizuri au kutokuwa katika emotional attention ya mapenzi ni kubwa kwa mwanamke ambaye ana matatizo.
“Kwa sababu muda ambao kisaikolojia hata binadamu alivyo awe mwanamke au mwanaume linapoingia suala la hisia za kimapenzi ubongo hauhitaji nafasi nyingine huwa unatakiwa utanuke uzibe matundu yote sasa hawezi kufanya tendo la ndoa kama unawaza madeni ya vicoba au simu inaweza ikapigwa muda wowote,” anasema.
Tatizo la msongo wa mawazo likizidi anasema husababisha sonona ambayo baadaye huweza kuwa chanzo cha tatizo la afya ya akili.
Wizara ya Afya imesema idadi ya wagonjwa wa afya ya akili limekuwa likiongezeka, mwaka hadi mwaka.
“Mwaka 2018 tulikuwa na wagonjwa 357,799 waliotibiwa, mwaka 2019 walikuwa 380,000 na mwaka 2020 walikuwa zaidi ya 500,000,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Wizara ya Afya.
Chanzo: Mwananchi