Usitapeliwe mitandaoni - Part 1

Nov 6, 2016
77
271
CHUKUA TAHADHARI ZIFUATAZO KUEPUKA KUTAPELIWA MTANDAONI

MAELEZO KWA VIDEO👇🏽



Na Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA

Kutokana na hali ya watu kuwa wanadhurumiwa mara kwa mara kwenye mitandao ninaanza kampeni ya kuwasanua watu kuhusu mbinu za hawa matapeli,

WAUZAJI WA BANDO
Pamoja na kwamba biashara hii bado sina utafiti wa kutosha kuhusu ufanyikaji wake lakini ninafahamu kwamba wezi wengi wa mitandaoni wamejificha humi.

UNATAPELIWAJE?
Ukishamtumia namba anaanza kukuzungusha kwamba line yako ina hiki na kile anakwambia umtumie namba nyingine, ya mtandao huo huo, jambo ambalo linakuwa si rahisi kwako, atakwambia sajili namba nyingine sasa hapo ndipo unapokata tamaa, na ukisajili namba nyingine mchongo unakuwa hivyo hivyo, inafikia mahali unachukia unaachana nae anasepa na pesa yako, akipiga huo mchongo week anapata hela ya kutosha.

CHUKUA TAHADHARI NA KUKUNUA BANDO

WATOA MIKOPO

Biashara za mikopo mitandaoni zipo lakini na wahuni wengi wamejipenyeza humo.

UNATAPELIWAJE?
Unapotaka mkopo utaambiwa weka sijui dhamana, au lugha yoyote ikimaanisha weka pesa kidogo upate nyingi , ukiweka umeliwa.

ACHANA NA MIKOPO MITANDAONI ISIPOKUWA KWA KAMPUNI ZINAZOJITANGAZA PROPER

TAHADHARI ZA UJUMLA

FANYA UTAMBUZI UFUATAO
1. JE MHUSIKA ANAFANYA BIASHARA KWA JINA LAKE AU JINA LILILOSAJILIWA. ( MFANO Comrade Ally Maftah, Jina lake halisi ni Ally Ramadhani Maftah, CAM STORE ni abreviation ya Comrade Ally Maftah na usajili upo )
2. JE MIAMALA MNAYOIFANYA INAENDA KWA JINA LA UNAYEFANYA NAE BIASHARA? ASIWE NI JUMA AKAFU WEWE UNATUMA PESA KWA ASHURA ( MFANO Comrade Ally Maftah UKIFANYA NAE BIASHARA UTATUMA PESA 0785670227 JINA LITASOMA ALLY RAMADHANI MAFTAH, AU KWENYE NAMBA ZA LIPA ZA CAM STORE AU KWA NAMBA 0762212623 JINA ALLY RAMADHANI MAFTAH JAPO HUWA SIPENDI KUTUMIA HII)
3. TUMA HELA KWA SIMU YAKO ISIWE KWA WAKALA ILI MESEGE YA MUAMALA UBAKI NAYO WEWE, NDIO RISITI YAKO NA USHAHIDI KWAMBA MLIFANYA BIASHARA
4. MCHUNGUZE MHUSIKA KAMA ANAFANYA BIASHARA NA KWENYE MITANDAO MINGINE SOMA NA COMENT ZA WATEJA WAKE KAMA HANA COMENT CHUKUA TAHADHARI KAMA HAFANYI KWINGINE ZAIDI YA WATSUP ACHA HIYO BIASHARA ( MFANO Comrade Ally Maftah ANAPATIKANA MITANDAO YOTE KWA JINA LAKE NA KWA CAM STORE NA TAARIFA ZAKE ZINAFANANA )
5. JE MUUZAJI ANAJIHUSISHA NA JAMII? CHAMA CHA SIASA? TAASISI YA KIDINI? TAASISI YA KIBIASHARA AU NI MFANYAKAZI WA KAMPUNI IPI? ( Comrade Ally Maftah ANAJIHUSISHA NA JAMII ANAO MARAFIKI WA KARIBA ZOTE WA DINI, WA SIASA, MATAJIRI, VIONGOZI, WASANII NA MAKUNDI KAMA WALEMAVU NK, UKIMFUATILIA UNATHIBITISHA )
6. MUUZAJI ANA OFISI WAPI? KAMA HANA OFISI ACHANA NAE ( MFANO Comrade Ally Maftah ANA OFISI ANAZOFANYIA KAZI TEGETA OPP THE ONE HALL, MIFUGO PLUS, KARIBU NA DARAJA LA KIJAZI - ORGANIC BRAIN, JANGWANI- KWA ASHAM NA OFISI NYINGI ZA PRINTING PAMOJA NA OFISI ZINGINE ANAAMINIKA )

NITAENDELEA KUWASANUA WANA KUHUSU HAWA MATAPELI

NDIMI Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
0762212623



👇🏽 MAELEZO KWA VIDEO
 
King of nyokonyoko na haujui hata kanuni za uandishi, hata ile basic knowledge tu hauna..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom