USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Aisee hivi Jakaya amepewa ukuu wa UDSM kwa kipi ?? Kuna kila sababu ya kubadilisha sheria inayokataza Rais wa Nchi asifunguliwe mashtaka ,huyo alitakiwa awepo kwenye house of arrest mpaka tunapo ongea hivi sasa,kama Magufuli dhamira yake ni ya dhati aanze na kufuta hiyo sheria then anyonge watu kama kumi hivi ndio mambo mengine yaendelee ,vinginevyo anampigia mbuzi gitaa
 
Wazalendo wako wengi nchi hii, lakini tatizo liko kwenye mambo ya itikadi tuu. Mfano mleta mada akijulikana itikadi yake iko tofauti na chama tawala basi hata ushauri wake utatupwa kule kwani ataonekana sio mzalendo.
Wanachosahau ni kuwa hao wakina Masamaki ndio wana pea hata kumi za mashati ya kijani na kwenye michango ya kujenga chama wanatoa mamilioni
 
hapo riz anaingiaje,maana?nasikiaga riz riz,Kumbe kina anderson ndo wanacheza deal bana
 
Aiseee.. Mkuu Asante kwa taarifa, Ila uwe makini.. Matajiri wanakuaga na mkono mrefu sana, as long as umeamua kumwaga unga.. Cha kufanya wewe Chukua hizo namba za Mh. Rais au Waziri Mkuu, SIO MUlugo.. Mwambie shida yako jamaa watakutana na wewe.. Utaheshimika sana, unafanya kwa maslahi ya taifa Letu... SISI WANYONGE, watoto wetu wasome Ktk mazingira mazuri, mama wajawazito wajifungue sehemu Salama.. Babu zetu Kule vijijini wapate barabara, umeme na maji safi.. Kila La kheri, Mungu akupe Maisha marefu yenye amani na furaha tele.
 
Taarifa nzito sana. JPM alikuwa mjanja sana wakati wa kampeni, alihakikisha mkwanja wa matajiri hauingiliani na kampeni yake yeye binafsi. Alijua madhara ya yeye kuwakaribisha karibu yake wale matajiri wetu (haswa wenye asili ya kiarabu na kihindi). Kama alivyosema siku ile alipoongea katika mwaka mpya wa mahakama, nchi ni lazima inyooke, kwa kuanzia ni huko juu.
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya
OIL COM ndio kinara.
Uzalendo wako ndio unaohitajika katika nchi hii. God bless you!!!
 
mwaka huu kuna wagonjwa w majibu inabidi uwazike na majipu yao yataponea hukohuko kaburini
 
mkuu Nataka kuamini kabisa kua upo ndani ya circles za hii biashara ya mafuta; corrupt agents wa tiss wapo hasa wale ambao hua wameingia kwa migongo ya wakubwa au jamaa zao ambao ni vizito katika idara kwani kuwajibishwa inakua ngumu kidogo ila kwa wale ambao wameingia kwa zali wengi ni wachapa kazi, taarifa zipo nyingi ila mfumo ni mbovu kuaccomodate actions kufanyika katika level inayotakiwa, hivyo basi jaribu kupeleka taarifa in details bila woga wala upendeleo. wengine sisi kipindi cha nyuma hua tulikua tunaandaa taarifa na ushahidi tutazidump katika eneo husika hapo unapunguza anonimity rather kumface mtu na kumpa taarifa. watu hawaaminiki ndugu yangu unaza dhani unampa mtu taarifa kumbe anazipeleka direct kwa mlengwa. corruption imekua tatizo uzalendo hakuna.
 
Na kwa ukweli huu waziri wa nishati, katibu mkuu wa wizara na mkurugenzi wa TISS bado wapo kwenye nafasi zao hawajajiuzulu tu!? Na hao oilcom na wengine walotajwa waripoti segerea magereza wenyewe. Ndiyo maana shule zetu Hazina vifaa na walimu wetu wa alipwa kiduchu. 70m kwa saa moja no kiinua mgongo cha walimu watatu waliofanya kazi miaka zaidi ya 25.
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.


Wewe wala usijali sidhani kama Raisi Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa hawayajui hayo uliyoyaeleza wanayajua sana kwanza wanayajua kabla hata WM hajaenda hapo kwenye hiyo mitambo ya mafuta na ndiyo maana unaona hawakuweza kumdanganya ingawaje yeye WM siyo mtaalamu wa mambo ya mafuta, alikuwa na data zote na hata ukifwatilia maagizo aliyoyatoa siyo ya mtu ambaye hakuwa amejitayarisha na asiyejua alichokuwa anakifanya!

Hata ukiangalia huyo Masamaki uliyemtaja alishachomolewa zamani na ana kesi hivyo ninaweza kukutoa hofu wanajua kila kitu na ni swala la muda tu kwani lazima ujue kwamba wahalifu nao pia ni werevu hivyo ni lazima kwenda nao kwa umakini na mwisho wa siku sisi tunachotaka na fedha zetu ninakwambia kwa Magufuli kila jiwe litafunuliwa kama alivyosema Mzee Slaa, hao akina Oil Com, Lake Oil wote wako kwenye radar utasikia tu mda siyo mrefu!

Hivyo wewe chill na relax Raisi na Serikali yake wanafahamu yote hayo na zaidi kuna sababu kwa nini Maswi aliletwa halafu akaondolewa baada ya kumaliza kazi yake hivyo sasa kazi ndiyo imeanza na haponi mhalifu yoyote yule amini usiamini!
 
Hii nchi imeoza hasa hawa watu wa kutoka bara la Asia ambao wanahodhi uchumi wa nchi ni mabingwa wa kukwepa kodi halafu mzigo wanabebeshwa raia. Naamini the so called TISS na wahusika wote wanapita humu au kupata hizi taarifa kwa namna moja au nyingine na kufanyia kazi. EWURA walikua hawajui kweli?
 
Mhe Rais tunakuomba ufanyike utaratibu wa kuajiri upya wafanyakazi wa TRA na BANDARI hao waliopo wanajua njama zote pangua pangua haitasaidia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom