Ushauri wangu kwa LATRA, RPC na RTO Morogoro

Sean Paul

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
1,311
3,239
Habari wana bodi.

Mimi ni mdau wa sekta ya usafirishaji na katika observations zangu nimegundua tatizo na nashauri watajwa hapo juu katika mkoa wa Morogoro kama ifuatavyo.

Manispaa ya Morogoro iliamua kuhamishia mabus madogo yote yanayokwenda nje ya mji yawe yanaanza safari zake stand ya Mafiga. Ni uamuzi mzuri japo una changamoto zake. Lakini ninachotaka kushauri mimi si suala la stand kuwa wapi, bali vibali vya kufanya usafirishaji.

Mimi nashauri NOAH, ALPHARD na HIACE zipigwe marufuku kusafirisha abiria kutokea Manispaa kwenda kokote nje ya mji. Hata Moro-Dakawa wakatazwe. Kwanini?

Kwanza, vigari hivi ni hatari sana kwa usalama vinapokuwa barabarani. Noah ya kawaida inabeba watu 8 (pamoja na dereva) lakini kwenye safari nyingi za Moro-Dumila, Gairo, Turiani n.k wanabeba abiria 10 na dereva anakuwa wa 11. Hii ni hatari mno kiusalama.

Pili, vigari hivi vingi vimekaidi amri ya kuanza safari Mafiga. Vinajificha pale Msamvu kwenye kituo cha Mafuta (sitakitaja) sababu najua mnakijua. Wanapakia abiria kwa kuiba iba. Kisha wanazunguka nyuma kama vile wanatoka Mafiga wanapita askari wa pale Msamvu wakiendelea na safari.

Tatu, madereva wengi wa vigari vile ni deiwaka vijana tu wasio na sifa za udereva wa abiria. Wengi wana leseni hadi class D au B. Kwa safari wanazofanya walitakiwa angalau C3.

Kwahiyo, toeni ruhusa kwa Coaster na zinazofanana na hizo kuepusha majanga na kuenforce sheria. Waigeni wenzenu wa Pwani na Dar, route ya Dar-Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri, Mohoro na kuendelea ni walishakataza matumizi ya hiace muda mrefu sana na kupunguza ajali nyingi, pia kuleta utulivu kwa abiria.

Naamini hili linawezekana na linatekelezeka. Wakati ni sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…