Ushauri wangu kwa kijana wangu Mbwana Samata

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,974
Samatta: Huyu ndie anaefaa kuwa rafiki yako Aston Villa.

Kwanza natoa pongezi nyingi kwake Mbwana Samatta jana tumeona akicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Tim yake mpya ya Aston Villa. Na pongezi kwa Aston Villa kwa kukata tiket ya kucheza fainali ya Carabao Cup itakayopigwa katika uwanja wa Taifa wa England pale Wembley.

Wabongo wengi jana baada ya mechi kati ya Aston Villa vs Leicester City walikuwa wana ongea mengi na mengi ya wengi walikuwa wakimpa hongera Mtanzania mwenzao kwa kuweza kucheza kwa dakika 60+ Kabla ya kupatwa na majeraha yaliyomlazim kufanyiwa mabadiliko.

Kwa upande wangu baada ya mchezo ule niliondoka na jina la mchezaji mmoja tu. Jina hilo ni la Jack Grealish. Why? Utajua tu.

Hapa nataka Mbwana Samatta anisikilize kwa umakini sana. Mana nimegundua 'El capitano' wa Villa ndie amebeba ufunguo wa mafanikio yake ya uwanjani. Why? Twende mdogo mdogo tutaelewana.

Kwanza 'super star' wa nchi Mbwana Samatta anatakiwa awasahau kwa muda wazazi wake wa mpira kama Moses Katumbi aliemlea vizuri kiasi cha kumtengenezea mazingira ya kuitwa Mfalme ndani ya jiji la Lubumbashi akiwa na jezi ya TP Mazembe.

Pili, anatakiwa auweke kando kwa muda ukaribu wake na aliyekuwa kocha wa KRC Genk ambae aliishi nae vizuri kama mtu na anko wake hapa namjadili Hannes Wolf aliyempa maufundi ya kumfanya kuwa nyota ndani ya KRC Genk kiasi cha leo kusajiliwa na Aston Villa ya England.

Hapa pia anatakiwa amchukulie kocha mkuu wa Aston Villa Mr Dean Smith kama mzazi wake mpya akiwa ughaibuni huku John Terry amchukulie ni kama ngazi ya yeye kufikia kwenye ndoto zake zinazoishi moyoni mwake.

Bila ya Dean na Terry kuwa sehem ya maisha yake pale Villa Park nafikiri bado itamchukua Popa muda mrefu kufika Watanzania tunapomtegemea afike.

Turudi katika mzizi wa andiko hili... Kwa nini Mbwana Samatta nimemshauri ajenge urafiki wa uwanjani na Jack Grealish kuliko Marvelous Nakamba?

Wataalam wa mambo wamekuwa wakisema kuwa namba (takwim) hazidanganyi. Kama ndio hivyo hata mimi nimemdukua kiundani nimebaini katika kikosi kizima cha Aston Villa Jack Grealish ni mchezaji anaeibeba tim yake pakubwa.

'El capitano' Jack Grealish ndani ya kikosi chake ndie kinara wa magoli amezifumania nyavu mara 7 na ikumbukwe huyu sio mshambuliaji halisi ila ana cheza kama mshambuliaji anaetokea pembeni ama anacheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji ama anaweza kucheza kama mshambuliaji namba mbili.

Jack Grealish kwa upande wa kutoa pasi zilizotengeneza magoli 'assists' ndie kinara kwa Aston Villa amepiga pasi za goli 5 mpaka sasa. Je mmeanza kunielewa kwa nini natamani kuona Captain Diego akitengeneza combination ya uwanjani na huyu mtu hatari.

Jack Grealish ndie moyo wa timu ya Aston Villa Kama uamini unatakiwa ujue huyu ndie kinara kwa Villa katika kupiga mashuti katika goli la timu pinzani amefanya hivyo mara 46. Lakini katika mashuti yaliyo lenga goli kinara wao ni Wesley aliyelenga goli mara 18. Bado amjaiona nafasi ya Samatta kujenga urafiki kwa lazima na Jack Grealish?

Sababu nyingine ni kuwa Jack Grealish ndie kinara kwa Villa kwa kukokota mpira maeneo ya pili ya uwanja akiwa kafanya hivyo mara 77 anashika nafasi ya 14 katika EPL mpaka sasa. Na mikokoto 51 imefanikiwa ndani ya EPL anashika nafasi ya 9.

Sababu nyingine yenye sababu kwa +255 Champion Boy wetu kutengeneza urafiki hata kinafiki uwanjani na Jack Grealish ni kuwa yeye ndie kinara ndani ya EPL kwa kuchezewa madhambi akiwa amefanyiwa hivyo mara 106 huku akifuatiwa na Wilfred Zaha aliechezewa rafu mara 75, Maddison (71), Jordan Ayew (60) na Adama Traore amekula buti mara 52.

Jack Grealish kwa macho ya nje huyu ndie amebeba ridhiki ya magoli ya mtoto wa Mbagala rangi tatu. Kama miguu ya Jack Grealish itatengeneza ubia na mikimbio ya Mbwana Samatta nafikiri katika michezo 14 iliyosalia ya EPL tunaweza kumshuhudia kijana wa rais John Pombe Magufuli akifunga hata goli 10 ama zaidi ama pungufu ya hapo.

Jumla ya pasi mpaka sasa amepiga 893 na 'key passes' amepiga 53 na bado pasi zilizofika ni 762 hii ndio sabahu nyingine kwa Jack Grealish kuhusishwa na vilabu vikubwa kama Manchester United, Chelsea na Tottenham Hotspur. Ndiomana nataka aunde ka ushikaji na Popa ili wazungu washuhudie nyavu za kina De Gea, Becker na Beno zikitikisika.

Katika michezo 24 ya EPL kwa Aston Villa ni Jack Grealish na Douglas Luiz wamefanikiwa kucheza michezo 22 na muda alioutumikia kuivujisha jasho jezi ya Aston Villa ni dakika zisizopungua 1974 ndani ya EPL anashika nafasi ya 48.

Hi ni tafsiri ya kuwa Jack Grealish ni mchezaji aliye fiti kiakili na kimwili na ndiomana amecheza kwa ubora katika mechi nyingi na dakika nyingi kwa upande wa Aston Villa wanaopambana kulikimbia eneo la kushuka daraja.

Kwa sasa Aston Villa wanashika nafasi ya 16 wakiwa na alama zao 25 huku wamecheza michezo 24 na wamefunga goli 31 na wao wamefungwa goli 45.

Na wao pia awapo salama mana ukanda wa kushuka daraja umetenganishwa na alama 2 pekee. Nafasi ya 20 wapo Norwich City wakiwa na pointi 17 nafasi ya 19 wapo Watford wakiwa na pointi 23 nafasi ya 18 wapo AFC Bournemouth wakiwa na pointi 23. Na West Ham wao wapo nafasi ya 17 wakiwa na pointi zao 23.

Kiufupi Mbwana Samatta na Aston Villa ya Watanzania bado awapo sehem salama juhudi kujituma kujitolea kunahitajika kwao ili ndoto za Samatta za kucheza EPL ziendelee kuwa hai.

Kwa sababu hizo na nyingine unazozijua umeweza kujua ni kwa nini nahitaji kumuona Mbwana Ally Samatta akitengeneza 'partinership' ya nje na ndani ya uwanja na captain wa Aston Villa Jack Grealish.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hekima ya masikini haisikilizwi.

Huwezi kumshauri MTU anae uzidi hela ukoo wenu wote . Ni utovu wa nidhamu.

# Koma

# Next time usirudie tena
 
Bongo bana, mnaweza kuwa kwenye kikao unataka kutoa ushauri kama huu ukazuiwa ukihisiwa kutaka kuanzisha fujo. Utaletewa mirinda nyeusi ya moto bila kuulizwa unatumia kinywaji gani au unaweza kunyoosha mkono kutaka kuchangia ukashangaa mjomba yako anakufokea "kaa chini hatupo hapa kupiga punyeto" Wanaotuzidi hela hawatakagi tuwashauri
 
Back
Top Bottom