Kaka. Una idea ya biashara chuoni. FANYA!
Utapata mafanikio katika baadhi ya biashara na utafeli katika biashara nyengine. Huu ndio muda wa kujifunza ujasiriamali.
Mimi nilivyokuwa chuoni nilikuwa naenda DAR likizo na kuzunguka katika maduka wanazouza good quality refurbished PC. Nawapigia washikaji na kuwauzia. Wanatuma pesa na nilikuwa nikiwaletea. Faida ilikuwa nzuri sana.
Nilinunua printer na nilianzisha ki stationary kwangu (kipindi ambacho wanafunzi wachache walikuwa wanamiliki printers). Wino ulivyokuwa ukiisha nilikuwa nikiuza printer hizo (sikuwahi kununua wino kwani niligundua bei za wino ni ghali kuliko printer mpya).
Nilikuwa nikiagiza flash discs (enzi hizo flash disks zilikuwa ghali sana) online na ku supply madukani.
Nikajifunza web design na kuwatengenezea makampuni ya tours websites kwa bei rahisi (bei rahisi wakati huo ilikuwa ni $300 (hela nyingi sana kwa mwanafunzi wa chuo)). Nilikuwa nina install windows na software wakati ambapo mafundi walikuwa wana charge pesa nyingi kufanya hivyo.
Kama unavyoona passion yangu ilikuwa katika mambo ya computers japokuwa nilisomea degree ya udaktari.
Hivi sasa ninaendesha kampuni yangu yenye kuwasaidia wafanyabiashara kupata wateja kwenye mtandao (still computer related stuff).
Tafuta PASSION yako na ufanye biashara kama MWENDAWAZIMU.
Usiogope kufeli.
Hata kama utapoteza pesa zote. USIOGOPE!
Hapo ndipo utajifunza.
That's how you win! That's how you grow!
Good Luck