Ushauri wa kichochezi: Rais Magufuli anzisha chama chako na uhame CCM

WALIOTAJWA HADI SASA

1. MAAFISA wa TRA
2. AG A. Chenge (CCM)
3. AG J. Mwanyika (CCM)
4. DAG Felix Mrema (CCM)
5. Mkurugenzi Idara ya Mikataba..Mary Ndosi (CCM)
6. Kamishna Dalali Peter Kafumu (CCM)
7. Waziri Prof. Muhongo (CCM)
8. Waziri D. Yona (CCM)
9. Waziri A. Kigoda (CCM)
10. Waziri Karamagi (CCM)
11. Jaji Julius Malaba
12. William Ngereja (CCM)

Na hawa wote ni wana Chadema.
 
WALIOTAJWA HADI SASA

1. MAAFISA wa TRA
2. Ex - AG A. Chenge (CCM)
3. Ex - AG J. Mwanyika (CCM)
4. DAG Felix Mrema (CCM)
5. Mkurugenzi Idara ya Mikataba..Mary Ndosi (CCM)
6. Ex - Kamishna Dalali Peter Kafumu (CCM)
7. Ex - Waziri Prof. Muhongo (CCM)
8. Ex - Waziri D. Yona (CCM)
9. Ex - Waziri A. Kigoda (CCM)
10. Ex - Waziri Karamagi (CCM)
11. Jaji Julius Malaba
12. William Ngereja (CCM)

Halafu rais anauliza ni nani aliyeturoga?

Jibu; [HASHTAG]#CCM[/HASHTAG]
 
18952999_1336014753161384_8429699997380893310_n.jpg

Ha ha haaaaa

Hii picha inanichekesha...:D:D:D
 
Umejipambanua kuwa ni mtu tofauti kimaneno na kimatendo. Umekuwa ukisema ukweli na kufuatilia jambo kwa makini, undani na kwa dhati ya moyo wako. Tumekuwa tukikuzongazonga tu kwa manenomaneno pale ambapo unasema 'zaidi' ya yale ya kuyasema.

Hata wewe Rais unajua kuwa CCM ni chama chenye makandokando mengi. Kwakuwa chama ni wanachama, CCM haijawahi kukwepa kashfa zote za kifisadi tabgu kuanzishwa kwake hadi sasa. CCM inahusika na vyote ambavyo sasa unapambana navyo. Kila wakitajwa, ni makada.

Aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu wa Mutharika alitoa mpya kwa siasa za Afrika. Alichaguliwa Rais kupitia chama kiitwacho United Democratic Front mwaka 2004. Mwaka mmoja tu, mwaka 2005, Hayati Mutharika akaanzisha chama chake cha Democratic Progressive Party na akashinda uchaguzi kwa chama kipya.

Chema chajiuza! Hayati Bingu alihama kwakuwa mtangulizi wake katika Urais, Bakili Muluzi alikuwa akimuingilia katika utendaji wake kupitia uongozi wa Muluzi kwenye UDF. Mutharika alitaka kufanya mambo makubwa bila kuingiliwa.

Kutokana na 'kuchafuka' kwa kutosha na kutisha kwa CCM, nakushauri Rais Magufuli uunde chama chako na kuhama CCM. CCM inakugharimu katika kutenda kwako kwakuwa kila uchao utawakuta wale wale wakiwa wamefanya yale yale. Ndimo utakutana na watu kama Mtemi Chenge. CCM itakulazimu kuilinda.

Kuilinda CCM ni kulinda mabaya yake. Kuilinda CCM ni kupambana kimaneno na kimatendo na wakosoaji wake. Kuilinda CCM ni kuaminisha watu kuwa sasa CCM inajisafisha na 'inatubu' hata kama ni kwa tabu. CCM inakuchafua na inachefua. Walioaminiwa kichama na hata Bungeni ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.

Jambo la busara na lisilo na hasara ni kuanzisha chama chako na kuhama CCM. Wazalendo wenzako tutakufuata huko. Tutakurejesha Ikulu kwa nguvu zaidi na ukiwa unajiamini zaidi kwakuwa hautakuwa na 'urafiki'. CCM, ilipofikia na vinavyoendelea, haisafishiki wala hailindiki. Hata overhaul ni kupoteza nguvu tu.

Hama CCM mzalendo, linda mali za Tanzania yetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam


Hivi tumekuwa na roho ngumu za kinafiki kwa nini? nimemsikia kada mmoja wa ccm akihojiwa Redio Tanzania au TBC akidai wale wote waliotajwa na tume ya pili waondoke haraka kwani wataendelea kupaka chama matope.

Hivi kwa nini hatupendi kusema ukweli na matokeo yake tunaendeleza unafiki? hao wote wanaotajwa hapo walikuwa ni viongozi na makada wa ccm amabo walikuwa wanasimamia kile kilichokuwa kinatekelezwa na serikali ya ccm na kupitishwa kwa miswaada ya dharula iliyoletwa na serikali ya ccm.

Sheria zote za uchimbaji madini na hata ile iliyopitishwa kwa hati ya dharula zilipitishwa kwa sauti za ndio na wabunge wa ccm tena wakiwakejeli na kuwapiga vijembe wabunge wa upinzani. Leo ingewezekana Rais kuwaomba radhi wananchi kwa niaba ya chama chake ambacho kimewaibia watanzania miaka yote maana hakuna chama kingine ambacho kimewahi kutawala nchi hii.

Hilo swala la kupitia upya sheria mbalimbali za madini ndicho Lissu na Mnyika wameyarudia mara zote wakadhihakiwa na wabunge wa ccm, hivi hizo sheria zinazoenda kufanyiwa marekebisho wabunge wa ccm watasema nini wakati walizipitisha kwa mbwembwe na kuwadharau wapinzani waliona hazipo vizuri?
 
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
 
Mafisadi sugu walioifirisi nchi hii hawafiki hata 20, na wana nguvu ndani ya CCM hadi leo. Magu kwa namna katiba ilivyo anaweza kuwashughukia pasi shaka kama akiamua. Hakuna mwana CCM yoyote anaweza kucheza na mamlaka ya Rais. Ni kazi ngumu mno kuisafisha CCM, wengi tulijua hii itakuwa kazi kubwa mno ndiyo maana wengi tuliondoka na EL. Kazi hii ni ngumu saana wacha tuone as long as its for our Nation interest, we pray for Magu, but i still hate CCM kwa kutufikisha hapa, after 20 yrs ndo tuna realize sasa umuhimu wa kujadili mikataba openly?
 
Katiba tu imemshinda sembuse kuhama ccm hizo ni kiki or political juggling hamna lolote karamagi chenge yona na kigoda kafa yote atatupiwa yeye amguse mkapa au kikwete aone its business as usual.
 
WALIOTAJWA HADI SASA

1. MAAFISA wa TRA
2. Ex - AG A. Chenge (CCM)
3. Ex - AG J. Mwanyika (CCM)
4. DAG Felix Mrema (CCM)
5. Mkurugenzi Idara ya Mikataba..Mary Ndosi (CCM)
6. Ex - Kamishna Dalali Peter Kafumu (CCM)
7. Ex - Waziri Prof. Muhongo (CCM)
8. Ex - Waziri D. Yona (CCM)
9. Ex - Waziri A. Kigoda (CCM)
10. Ex - Waziri Karamagi (CCM)
11. Jaji Julius Malaba
12. William Ngereja (CCM)

Halafu rais anauliza ni nani aliyeturoga?

Jibu; [HASHTAG]#CCM[/HASHTAG]

CCM ndiyo uchawi wenyewe.
 
Back
Top Bottom