Ushauri wa kichochezi: Rais Magufuli anzisha chama chako na uhame CCM

Napenda kuuliza hivi nuru na giza hukaa pamoja? Hivi ndivyo ilivyo ukitaka nuru lazima ukubali kuhama gizani uende huko kwenye nuru, Ndiyo maana mchana na usiku vinaachana, haiji tokea vikachangamana.....
My view....... Think more
 
naungana na wewe ndg tupa tupa kwa ushauri wako. Niukweli usiopingika kwamba Mh Rais yupo katika wakati mgumu sana wa kupambana na maadui walio ndani ya chama chake.

Hakuna jambo ambalo litatajwa leo ambalo halita ihusisha ccm moja kwa moja.

Sote ni mashahidi juu ya utungwaji sheria mbovu bungeni kwa kutumia wingi wao na maslahi yao.

Hapa ndipo tunapogundua kwamba hata ubakaji wa rasimu ya mzee wetu warioba bungeni kulitokana na mafisadi ndani ya chama wakiungwa mkono na wabunge wenye upeo mdogo wa kufikiri.

Hivyo ni vyema Mh Rais Akachukua Maamuzi magumu ya kuondoka ndani ya chama hiki, ili awezekuwa shugulikia mafisadi walio jazana ndani ya chama hiki vizuri.
 
18952999_1336014753161384_8429699997380893310_n.jpg
Sura kama kafumaniwa na mke wa mtu
 
Hata Mkapa na JK nao ni wazalendo sana tu,wasio wazalendo ni wale waliopinga hizi sheria na mikataba mibovu17 yrs ago
Probably Yes/No.
Ulikwisha jiuliza kwanini miti mikubwa mijini inapokatwa wakataji uanza na matawi,baadae shina? Lakini kwa wachoma mkaa wao either ubandua ganda LA nje LA MTi ili ukauke au kuukata MTi wote bila kutoa matawi.
 
WALIOTAJWA HADI SASA

1. MAAFISA wa TRA
2. AG A. Chenge (CCM)
3. AG J. Mwanyika (CCM)
4. DAG Felix Mrema (CCM)
5. Mkurugenzi Idara ya Mikataba..Mary Ndosi (CCM)
6. Kamishna Dalali Peter Kafumu (CCM)
7. Waziri Prof. Muhongo (CCM)
8. Waziri D. Yona (CCM)
9. Waziri A. Kigoda (CCM)
10. Waziri Karamagi (CCM)
11. Jaji Julius Malaba
12. William Ngereja (CCM)
 
Probably Yes/No.
Ulikwisha jiuliza kwanini miti mikubwa mijini inapokatwa wakataji uanza na matawi,baadae shina? Lakini kwa wachoma mkaa wao either ubandua ganda LA nje LA MTi ili ukauke au kuukata MTi wote bila kutoa matawi.

Kuna mawili kukata matawi unaufanya mti uwe imara zaidi.Mfano ukitaka muembe uzae zaidi unaukata majani yake ili ustawi zaidi.

Bado sijaelewa hasira kwa Lissu imeingiaje?
 
WALIOTAJWA HADI SASA

1. MAAFISA wa TRA
2. AG A. Chenge (CCM)
3. AG J. Mwanyika (CCM)
4. DAG Felix Mrema (CCM)
5. Mkurugenzi Idara ya Mikataba..Mary Ndosi (CCM)
6. Kamishna Dalali Peter Kafumu (CCM)
7. Waziri Prof. Muhongo (CCM)
8. Waziri D. Yona (CCM)
9. Waziri A. Kigoda (CCM)
10. Waziri Karamagi (CCM)
11. Jaji Julius Malaba
12. William Ngereja (CCM)

Naona Kalemani ameachwa hapo au hausiki?
 
Kuna mawili kukata matawi unaufanya mti uwe imara zaidi.Mfano ukitaka muembe uzae zaidi unaukata majani yake ili ustawi zaidi.

Bado sijaelewa hasira kwa Lissu imeingiaje?
Labda Lissu alikuwa anaukata mti alioukalia.
 
Hili wazo ni mbadala na linakubalika Rais Magufuli anatamani iwe hivyo kama alivyo fanya hayati Bingu wa Mutharika, tatizo kwetu ni mfumo wa chama ulivyo na unafiki wa baadhi ya viongozi wa chama na serikali, nadhani ni wakati wa Magufuli kulishawishi bunge libadili katiba ili apate kuongoza kwa mihura zaidi ya miwili ili lengo na ndoto yake ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati iwe imetimia.

Vinginevyo demokrasia tunayoendelea kuidai kwa kufanya uchaguzi baada ya miaka 5 itatuletea kiongozi mwingine asiye mzalendo atakayekuja kupuuza juhudi za Magufuli na kurejea tulipo toka, Umasikini wa nchi nyingi za kiafrika umejikita sana kwenye kitu wenzetu wanaita "Democracy"
 
Umejipambanua kuwa ni mtu tofauti kimaneno na kimatendo. Umekuwa ukisema ukweli na kufuatilia jambo kwa makini, undani na kwa dhati ya moyo wako. Tumekuwa tukikuzongazonga tu kwa manenomaneno pale ambapo unasema 'zaidi' ya yale ya kuyasema.

Hata wewe Rais unajua kuwa CCM ni chama chenye makandokando mengi. Kwakuwa chama ni wanachama, CCM haijawahi kukwepa kashfa zote za kifisadi tabgu kuanzishwa kwake hadi sasa. CCM inahusika na vyote ambavyo sasa unapambana navyo. Kila wakitajwa, ni makada.

Aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu wa Mutharika alitoa mpya kwa siasa za Afrika. Alichaguliwa Rais kupitia chama kiitwacho United Democratic Front mwaka 2004. Mwaka mmoja tu, mwaka 2005, Hayati Mutharika akaanzisha chama chake cha Democratic Progressive Party na akashinda uchaguzi kwa chama kipya.

Chema chajiuza! Hayati Bingu alihama kwakuwa mtangulizi wake katika Urais, Bakili Muluzi alikuwa akimuingilia katika utendaji wake kupitia uongozi wa Muluzi kwenye UDF. Mutharika alitaka kufanya mambo makubwa bila kuingiliwa.

Kutokana na 'kuchafuka' kwa kutosha na kutisha kwa CCM, nakushauri Rais Magufuli uunde chama chako na kuhama CCM. CCM inakugharimu katika kutenda kwako kwakuwa kila uchao utawakuta wale wale wakiwa wamefanya yale yale. Ndimo utakutana na watu kama Mtemi Chenge. CCM itakulazimu kuilinda.

Kuilinda CCM ni kulinda mabaya yake. Kuilinda CCM ni kupambana kimaneno na kimatendo na wakosoaji wake. Kuilinda CCM ni kuaminisha watu kuwa sasa CCM inajisafisha na 'inatubu' hata kama ni kwa tabu. CCM inakuchafua na inachefua. Walioaminiwa kichama na hata Bungeni ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.

Jambo la busara na lisilo na hasara ni kuanzisha chama chako na kuhama CCM. Wazalendo wenzako tutakufuata huko. Tutakurejesha Ikulu kwa nguvu zaidi na ukiwa unajiamini zaidi kwakuwa hautakuwa na 'urafiki'. CCM, ilipofikia na vinavyoendelea, haisafishiki wala hailindiki. Hata overhaul ni kupoteza nguvu tu.

Hama CCM mzalendo, linda mali za Tanzania yetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Inaisafisha vizuri tu, watabaki wazalendo pekee, wapiga dili wataondoka tu
 
Back
Top Bottom