Ushauri kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama juu ya vyombo vya usafiri wa Umma

nshimiyimana

Member
Oct 18, 2014
40
25
Mimi ni Mtanzania mzalendo napenda kutoa ushauri kwa vyombo vyetu vya usalama kuimarisha ulinzi wakati wa things katika vyombo vya Usafiri wa Umma. Kuhusu usafiri wa anga naipongeza Serikali kwa kuimarisha ulinzi nikitolea mfano Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere Airport ambapo ukaguzi wa mwili ( Full body scanning) hufanywa kwa wasafiri kutambua silaha au chochote kilichopo mwilini kwa sababu za kiusalama .Hivyo ndivyo inavyofanyika pia katika nchi nyingine.

Nikirudi kwenye vivuko, treni, mabasi ya mwendo kasi ukaguzi wa namna hii haufanyiki ilhali vinabeba watu wengi. Kivuko kinabeba watu wasiopungua elfu Mbili mfano kivuko chetu cha MV Kigamboni, treni watu sijui idadi, tukirudi kwenye mwendokasi hali ni hiyo hiyo ambapo basi moja lina uwezo wa kubeba abiria wapatao120 Watanzania na wageni kwa kwa nauli ya Tsh 650/= binafsi naona usalama wa chombo na abiria unakuwa hatiani endapo mtu mwenye silaha au kifaa cha kutishia usalama ataamua ataamua kutishia au kukitumia ukiachilia mbali wizi kutoka maungoni unaofanyika hasa katika vituo vya mwendokasi kituo cha Fire (Faya) na kwingineko mida ya asubuhi wakati wa kugombania kuingia katika mabasi haya japo wizi huu haufanyiki sana ndani ya mabasi kwa kuwa kuna kamera.

Uwepo wa vifaa hivi utanipa amani mimi kama msafiri na mdau wa vyombo vya usafiri wa Umma.

Huo ndio ushauri wangu nina imani utafika kwa wahusika wenye dhamana ya Ulinzi na Usalama na jambo hili au pengine kuna mikakati imeandaliwa basi ijumuishe mawazo haya ili kutokomeza vitendo vya kihalifu .

Nakaribisha michango ya kujenga bila lugha ya matusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…