Ushauri kuhusu mkwe na matakwa yake

Waterlemon

Senior Member
Sep 2, 2016
137
178
Salamu wana JF,

Nimeamua kuja kupata maoni yenu wakuu kuhusu hili jambo ambalo linanikereketa moyoni.

Ni hivi waungwana, niko kwenye ndoa na mke wangu karibia mwaka wa pili huu. Nakaa mji wa mbali na wazazi na family wa pande zote mbili, na huku tulipo mie na mke wote tunafanya kazi. Mungu amejaalia ya kuwa amepata ujauzito tunatarajia kupata mtoto mwezi wa sita mwaka huu. Familia nzima limelifurahia hili.

Jambo la kukereketa ni kuwa mimi huwa napata safari nyingi za nje ya nchi kikazi mara kwa mara ambazo kawaida huwa zinanitoa huko kwa mda wa siku tatu mpaka wiki. Mara nyingi tukiwa sisi wawili tu nikiondoka kikazi kumuacha mke peke yake nyumbani huwa hamna tatizo. Tunaaminiana na tunaishi kwa harmony sana yaani hakuna ugomvi wala nini.

Tatizo kuna vipindi huwa ndugu zangu huwa wanakuja kukaa nami hapo nyumbani pamoja na mke wangu. Tena la zaidi wakija huwa wako katika harakati za kimaisha yaani mfano wamepata kazi karibu na nyumbani hivyo kujianzisha kimaisha huniomba kuja kukaa na mimi hapo nyumbani kwangu na mke wangu kipindi fulani ili wapate kujipanga na kutafuta mahala kwao. Tatizo katika harakati zangu za kikazi kipindi wakiwepo hapo nyumbani huwa naweza kupata safari ya kikazi na kuondoka.

Kiufupi nawaamini sana wadogo zangu wa kiume. Tumelelewa na kukuzwa kiheshima kwa desturi za kiislamu, na vile vile namuamini mke wangu. Tumepitia mengi kimaisha kiasi kwamba sidhani kama anaweza kutupa tulilonalo kirahisi rahisi. Hivyo hata nikiondoka kuwaacha, huwa hata sina wasi wasi kama jambo lolote baya linaweza kutokea huko nyumbani wakati sipo. Imani 100%

Tatizo ni mama mkwe. Kipindi hiki nasafiri kama ndugu yangu yupo nyumbani huleta malalamiko mengi sana na uchochezi mkubwa. Huwa analeta headache sana kama eti binti yake yaani mke wangu husukumwa kimaamuzi. Husema nafanya mambo bila kuangalia athari na ni kinyume na dini yetu ya kiislamu. Hataki ndugu zangu wakae nyumbani. Na kweli yako mafunzo ya dini yaliyogusia kuhusu swala hili na ni kweli mafunzo yanasema sio vyema maana shetani linaweza kuwa kati, lakini nami nimelipima ya namna gani nawajibika nifanye kulingana na hali halisi ilivyo.

Lakini kwa jinsi hili swala lilivyonishika inabidi nichukue maamuzi mazito. Maamuzi ambayo yanaweza kuleta kuchafuana na mama mkwe au kufanya mambo yatakayoletea kuonyesha sitoi msaada kwa ndugu zangu kama ninavyowajibika.

Sasa wakuu, mnalionaje nyinyi hili?

Shukrani waungwana.
 
Hongera kwa kuhakikisha nduguzo anapata msaada......... ila elewa ndoa ni ya watu wawili......yaani wawili tuuuu......hayo unaweza kuyamaliza kwa kuongea na mwenza wako kwa upendo na upole.....kumbuka ana uja uzito.....maana hiyo kitu huwa na mibalaaa..... ila ni mambo madogo mnaweza kuyamaliza bila maumivu............
 
Mama mkwe hataki nini?

Hataki ndugu zangu wa kiume wakae nyumbani wakati sipo. Jambo ambalo wakati mwengine huwa sina control nalo. Niwaambie nikiondoka nao waondoke. Au kiufupi nisiwachukue kabisa kukaa kwangu ... jambo ambalo linaonyesha kutokuwa na suppot au uaminifu hata kwa ndugu zangu wa damu wa kuzaliwa
 
Ukiachana na mama mkwe na suggestion zake mkeo yeye anasemaje juu ya hilo?

Mke anaelewa nini dhumuni lililopo moyoni mwangu na anafahamu udugu ni kusaidiana na maisha tuliyonayo inabidi iwe hivi. Tukiongea anaonyesha kuelewa ninalomueleza, lakini pressure kutoka kwa mama yake mzazi anaemuheshimu. Yaani akinitetea wanamwambia wewe ni push over... yaani upo kusukumwa sukumwa tu kimaamuzi
 
Mama mkwe yupo sahihi kwa mujibu wa dini. Mshukuru sana mama mkwe wako Kwa kukushauri kuzingatia dini inavyosema kulinga na mazingira hayo.
Jambo la kufanya ndugu yako wa kiume anapojipanga ili aamie kwake inabidi umsaidie Kivingine na si kukaa naye kwako. Hii ni kitokana na nature ya kazi zako.
 
kama mkeo yupo.na wewe huyo ma.mkwe mnyamazieni tu akiongea bla bla bla bla mjibu "sawa mama" endelea na yako
 
Ok! Zingatia misingi ya dini yako.
 
Kwani hiyo ni ndoa yako na mkeo au na mama mkwe??
Muelewesheni tu jamani.

Maisha yetu ya kiafrika ndivyo yalivyo ndugu kusaidiana, sasa waende wapi nawe ndio kaka yao na ndie mwenye uwezo wa kuwasaidia?
 

Shukran mkuu. Tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu
 
Kwani hiyo ni ndoa yako na mkeo au na mama mkwe??
Muelewesheni tu jamani.

Maisha yetu ya kiafrika ndivyo yalivyo ndugu kusaidiana, sasa waende wapi nawe ndio kaka yao na ndie mwenye uwezo wa kuwasaidia?

Hilo haswa ndio linalonigonga kichwa mkuu. Mama mkwe namuekea heshima kama anavyostahili na tutajitahidi kuchukua maamuzi ya kuzingatia. Mungu atuongoze njia zilizo njema
 
Unaishije na mama mkwe?!kila mtu akae kwake utashindwa hata kuangalia tv kifua wazi nyumbani kwako
 
Namuheshimu sana m kweo ila kwa Hilo muombe akae nje ya maamuz yenu kama mke n mume ikitokea ndugu wa kike wa mkeo wakija itakuaje
Bakia na msimamo wako mkuu as long as unaamin Hakuna lolote baya litakalotokea kuhusu hao ndugu zako
 
Namuheshimu sana m kweo ila kwa Hilo muombe akae nje ya maamuz yenu kama mke n mume ikitokea ndugu wa kike wa mkeo wakija itakuaje
Bakia na msimamo wako mkuu as long as unaamin Hakuna lolote baya litakalotokea kuhusu hao ndugu zako

Mkuu shukran kwa ushauri. Mungu akubariki
 
Wewe ni baba wa familia usiyumbishwe na maneno ya kipuuzi, anataka wakakae kwake au ukuwapangie wakati nyumba ipo!?? Fanya yako achana nae huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…