Wakuu habari za wakati.....!
Unaambiwa kwa mwenzako sikia ila omba yasikukute, Mimi yamenikuta na ni kitu ambacho sikuwaza.....! Iko hivi
Nina mwanangu wa kike kamaliza kidato cha nne mwaka huu kafaulu vizuri kwa div 1 kali tu...! Lakini cha ajabu amegoma kata kata kwenda shule akidai anataka kuolewa, na amemleta huyo mchumba hadi nyumbani ili taratibu zingine zifuate.
Sasa wakuu nimeshauri na kumsihi sana aachane na mawazo hayo azingatie masomo lakini imeshindikana....!
Na hasa ukizingatia ni mtoto wa kike, nimeona haina haja ya kumlazimisha sana kitu ambacho hataki..! Maana hata nikimzuia ipo Siku ataolewa tu....! Ngoja nimuache aende kupambana kwa alichokiamua...!
Ila wasi wasi wangu kama nikiamua kukubali kumuoza vipi siwezi kuchukuliwa hatua kwa kuruhusu aolewe akiwa amefaulu? Na ndo kwanza ana miaka 18, namuona bado mdogo kuingia kwenye ndoa...! Nashangaa ujasiri wa kulazimisha kuolewa kautoa wapiii....!
Sheria inasemaje kuhusu msichana aliyemaliza kidato cha nne akaamua kwa hiari asiendelee na shule, na kuamua kuolewa? Ushauri wenu muhimu sana wakuuu