Habari zenu wadau wenzangu!
Naombeni mnisaidie wenye uelewa kidogo na uwakala wa tigopesa na mpesa,maana mimi nimekuwa wakala sasa yapata miezi sita ila kuna suala ambalo nakuwa silielewe kwenye hii biashara,maana naweza nkapiga mahesabu yangu ya kufunga siku halafu kesho asubuhi nakuta pesa pungufu nkifungua mahesabu,je kuna usanii wowote ambao mawakala wenzangu mnahisi yashawahi kuwatokea kama suala hilo langu,inawezekana labda kwenye system wakanifanyia figisu figisu halafu wanachukua pesa bila kufahamu mimi wakala??Au ni usanii tu ambao kijana wangu wa kazi anaweza akawa anaufanya halafu mimi nahisi ni figisu za tigopesa na mpesa,maana napata loss ya laki kwa siku muda mwingine!
Mwenye uzoefu msaada wakuu wenzangu