Usaliti uliofanywa na Rais Magufuli juu ya matarajio ya walio wengi

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Mnamo mwaka 2015 kutokana na nchi ilipokuwa imefikia wengi tulitaka nchi iende UKAWA ( Umoja wa Kitaifa Wa Wapinzani). Kilichotokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Ni wengi hatukutarajia. Jaji mstaafu Lubuva ana swali la kujibu katika hili.

Hata baada ya matokeo kutangazwa jazba kwa wananchi ikapoa maana mshindi aliyepachikwa na NEC alikuwa msafi na mchapakazi na alionekana kutokuwa na mapenzi ya kichama yani chama tawala, alionekana ni mtu mwenye maslahi mapana kitaifa na alikuwa hana dosari au kashfa ya Rushwa na ufisadi.

Na mshindi huyo alikuwa ni JPM, Lowassa hakuwa chaguo la wananchi bali tokana na hali ya taifa (ufisadi nje nje, Rushwa nje nje, matumizi mabovu ya Madarakani, Huduma duni za kijamii, fedha ikawa sauti ya mtu, n.k) ilivyokuwa imefikia ililazimika watu wengi kuhamia upinzani na ndio maana kupata uchaguzi wenye ushindani mkubwa kutokea mwaka 2015.

Na hata chama tawala bila kutumia Dora, wizi wa kura na vyombo vya usalama, uchaguzi wa mwaka 2015 ndio ungekuwa anguko kuu lao.

JPM kupachikiwa uraisi haikutia hofu sana Kama ambavyo angepewa Bernard Membe, hata machungu ya matokeo ya uchaguzi yalivyotoka na kwenda kinyume na wengi tulivyotarajia kuwa Edward Lowassa ndie atakuwa mshindi wa kiti Cha uraisi, JPM akaonekana kuwa faraja na tarajio la wengi.

Usaliti wa JPM uliokuja kutokea baada kuapishwa kuwa Raisi.

1. Kutoa kauli kuwa hatofukua makaburi. Hii kauli ilitu-umiza wengi yani kwamba wakina Anna TIbaijuka, William Ngeleja, Andrew Chenge na mafisadi wengine hawatofikishwa mbele ya sheria kwa sababu tu hawajafanya uharifu huo kwenye serikali yake ya awamu ya tano.

2. Magufuli kuigawa nchi na kushindwa kulifanya taifa kuwa kitu kimoja. Toka JPM aingie Madarakani kuna mpasuko mkubwa wa kitaifa ameutengeneza na kuwajaza chuki watanzania chuki kisa tu siasa. Serikali yake imefumbia macho juu ya mauaji na utekejaji mwa watanzania waliofanyiwa vitendo hivi kwa kile kinachosemekana kumkosoa JPM au Serikali yake. JPM na viongozi wa chama tawala wamebaki kuhubiri amani yamkini hawaitendi amani Wala haki.

Hakuna uchunguzi wa kina na wenye mashiko umetolewa na serikali juu ya watanzania hawa Tundu Lissu (shammbulio ya kumtaka kumuua), Azory Gwanda (Uwepo wake alipo), Mohammed Dewji ( utekwaji wake), Ben Saa nane (Alipotelea wapi) n.k, pia mauaji ya kinyama ya viongozi wa vyama pinzani hakuna ripoti au taarifa yenye kuleta timamu na mantiki imetolewa na serikali ya JPM. Matukio haya yamekuwa yakigawa taifa na kupandikiza chuki kwa wananchi.
Vitendo hivi vimeongezeka kwa kasi tangu JPM aingie Madarakani na serikali yake.

3. Uminywaji wa Demokrasia nchini.Na hii imekuwa kinyume na matarajio tulio wengi tulitarajia Magufuli atatumia demokrasia iliyohainishwa kikatiba tupate kujenga taifa kwa pamoja ila imekuwa kinyume.
Tangu JPM na serikali yake iingie madarakani demokrasia katika tasnia na namna namna mbali mbali imekuwa ikiminywa wazi wazi.

>>Uhuru wa habari, waandishi habari na Vyombo vya habari, tasnia hii serikali ya Magufuli na serikali yake wameifanya tasnia hii kuwa ngumu katika utendaji na kuthibitisha sio tasnia salama kwenye serikali yake. Azory Gwanda mpaka hajulikani na alipo na hakuna uchunguzi wa vyombo vya usalama unaojieleza kuwa unaendeleaje kumtafuta. Mwandishi Kabendera kushinikizwa kukiri kosa lisilo lake. Hukumu ya Paul Makonda kuvamia kituo Cha Clouds Fm mpaka sasa haijafanyika. Bunge kupewa masharti ulushwaji wake kwenye Vyombo vya habari.

Leo hata ukiona mbunge au mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au kiongozi serikalinki anakula Rushwa au anafanya ufisadi au hawajibiki ukaseme ukaripoti kwenye Vyombo vya habari au uviite vipate tangaza habari,haviwezi fanya hivyo maana havina kinga na viongozi ndio wana Kinga, hii imedhirishwa wazi na serikali ya JPM maana kama mpaka Paul Makonda hajapata hukumu manaake ana kinga huyo na taarifa hiyo yenye ushihidi wa video ikatafsiriwa uvumi.

>>Uhuru wa kutoa mawazo na kujieleza. Tulitarajia JPM angetengeneza platform (uwanja mmoja) wa kusikiliza mawazo ya wananchi wake bila kujali anakosolewa kwa maslahi mapana ya taifa. Imekuwa Kinyume yake kila ataonekana kumkosoa au kukosoa au kutoa taarifa yote inayomhusu yeye au kumkosoa yeye Bali anatiwa mbaroni.

Abdul Nondo (mwanafunzi UDSM) lengo la kupiga picha na kuziweka mitandaoni zile hostel za Magufuli zilizojengwa na TBA kwa Bei nafuu, lengo la Nondo halikuwa kumhahibisha JPM juu ya zile nyufa zilitokea wakati jengo halina hata mwaka mmoja wa matumizi. Lengo ilikuwa kumuonesha JPM hii taasisi ya TBA sio ya kuaminika. Wakina Titho mpaka sasa kawatia mbaroni, Maxence Malo (JF founder) wanazidi kumuwinda kila siku bila mafanikio, iam Martin wa Twitter mpaka Sasa yupo ndani. Kigogo2014 serikali yake bado inamtafuta imtie mbaroni. Mange Kimambi pona yake kuwa Marekani la sivyo angekuwa hayati Mange Kimambi.

>> Uhuru wa vyama vya siasa. Toka JPM aingie Madarakani ameshiriki moja kwa moja serikali yake kuminya uhuru wa vyama pinzani na kununua viongozi wa vyama pinzani kwa kutumia mwamvuli wa kuunga mkono juhudi za JPM na serikali yake. Vyama pinzani kavinyima ufanisi na uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao na kueneza sera zao, huku Chama chake hakina sharti lolote na kinakuwa na ulinzi wa Vyombo vya usalama vikilinda mikutano yao au shughuli zao za kichama.

4. JPM kukengeuka kutoka mtendaji hadi kuwa mwanasiasa. JPM aliyekuwa naibu na waziri katika wizara za huko nyuma kabla ya hajawa raisi ni tofauti Sana na JPM raisi wa Sasa. JPM typically amekuwa mwanasiasa na sio mtendaji Kama huko awali alipokuwa akiongoza wizara. Tena Bora angekuwa mwanasiasa wa nchi zilizoendelea Kama Marekani au uingereza ambao huwa na maslahi mapana ya mataifa yao katika kila sekta na nyanja. Yeye amekuwa mwanasiasa wa kiafrika, wa kiafrika huangalia tumbo lake, watoto wake na chama chake. Mfano. Viongozi wa UVCCM Iringa na Arusha kwa kauli zile za kutaka Zitto Kabwe, mpaka Sasa JPM amekaa kimya. RPC wa Arusha kaenda kwenye kikao Cha CCM mkoa Arusha, anaongea wazi wazi kusema CCM na polisi lao moja, JPM mpaka Sasa hamna tako lolote hata kukemea hamna.

5. JPM kuamini yeye na CCM ndio wa kuleta maendeleo na mapinduzi ya kiuchumi. Kwenye kampeni aliahidi kushirikiana na viongozi au watanzania bila kujali itkadi ya aina yoyote. Kinyume chake baada ya kupata uraisi vyama pinzani wamekuwa maadui zake, maadui wa chama na taifa kiujumla hata Kama akiri kwa mdomo matendo yake yapo wazi. Bila kuwa CCM hupati na hatamu ya kuongoza, hata uwe na sifa Bora vipi. Chacha waitara baada ya kuhamia CCM ndio kapewa unaibu waziri. Anna Mghwira kapewa ukuu wa mkoa mpaka alipo jiunga CCM. Kitila Mkumbo nae kahamia CCM ndio kupata hatamu ya kuongoza.

6. Kubadili katiba na taasisi za serikali, alionekana Kama kiongozi shujaa ambae mwenye maslahi mapana ya taifa ambae angebadilisha katiba. Hata kwenye kamapeni alizungumzia swala la katiba lakini mpaka Sasa kimya hata kulizungumzia. Taasisi Kama ya msajiri wa vyama na NEC anaendelea kuzijenga kwa maslahi mapana yake na CCM.

Huyu ndie alikuwa anaweza kubadili Mambo mengi nchini, lakini kwa sababu nae amegeuka kuwa mwanasiasa wa kiafrika basi tutarajie kujengewa miundo mbinu tu, swala la kukuza ukuzaji wa uchumi tulisahau, katiba na NEC huru tusahau kabisa. Mifumo Bora ya kiutawala tuzidi kuota. Bunge huru na mahakama huru ibake kuwa ndoto yetu na tusichoke kuota. Upatikanaji wa haki haswa zinazovunjwa na CCM na viongozi wake tusahau kabisa.
 
Watu aliowaita mafisadi walikuwa wanalipwa mil 40 kwa mwezi yeye anajilipa bil 1.2 kwa mwezi.

Eti anawaita na kuwapa tausi ikulu ambao alisema mafisadi ndio wametufikisha hapa.

Yaani kama kuna mtu msaliti basi ni Magufuli, Ametengeneza Kila aina ya watu. majizi, vilema,masikini na wajane huu ndio utawala wa hovyo sana ktk historia ya taifa letu.

Viazi wanamuita yesu na wanataka aongezewe muda ili taifa liendelee kutengeneza wasomi wasio na kazi, kuvunja katiba, kuchota pesa za umma atakavyo, kuua uchumi na kuua watu.
 
Hii aibu sijui Watanzania wataificha wapi? Nchi iliyokuwa inasifika kwa kuwa na umoja, Amani,upendo na furaha leo tunajibanza kwenye uzalendo huku tukifanya ugaidi dhidi ya Wananchi.

Matendo maovu yanafanywa na vyombo vya Wananchi kwa gharama ya kodi zetu wenyewe.
 
wilson kaiser senior,

Pamoja na kuwa Covid 19 inaonekana kutokuwa fair hata hivyo bado naamini itafanya kitu kabla ya uchaguzi mkuu hapo october maana haiwezi ikasafisha duniani nzima Kisha watu wa ajabu ajabu wakabaki hapa Tanzania.
 
Semeni yote ila wale jamaa wapwani walioanza kuvamia watu na raia kuuawa Kila mara!!!! Ulikuwa Ni ugaidi unaingia Tanzania mara wamekamatwa amboni.pangoni .KWELI naishukuru serikali kwa kuwadhibiti. Sijui Sana Leo hi Rufiji kuko shwari mbona hamtoi pongezi ?
Mnalaumu tuuu toeni na hongera Basi
 
Yaani Umeandika ambacho Mpinzani Yoyote Anatakiwa Akitaje Jukwaani. Magufuli ni Kiongozi wa Hovyo Taifa limemshuhudia Mbabe asiye na Utu na Mwizi ndiyo maana Hapendi mambo ya Uwazi.
 
Mnamo mwaka 2015 kutokana na nchi ilipokuwa imefikia wengi tulitaka nchi iende UKAWA ( Umoja wa Kitaifa Wa Wapinzani). Kilichotokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Ni wengi hatukutarajia. Jaji mstaafu Lubuva ana swali la kujibu katika hili.

Hata baada ya matokeo kutangazwa jazba kwa wananchi ikapoa maana mshindi aliyepachikwa na NEC alikuwa msafi na mchapakazi na alionekana kutokuwa na mapenzi ya kichama yani chama tawala, alionekana ni mtu mwenye maslahi mapana kitaifa na alikuwa hana dosari au kashfa ya Rushwa na ufisadi.

Na mshindi huyo alikuwa ni JPM, Lowassa hakuwa chaguo la wananchi bali tokana na hali ya taifa (ufisadi nje nje, Rushwa nje nje, matumizi mabovu ya Madarakani, Huduma duni za kijamii, fedha ikawa sauti ya mtu, n.k) ilivyokuwa imefikia ililazimika watu wengi kuhamia upinzani na ndio maana kupata uchaguzi wenye ushindani mkubwa kutokea mwaka 2015.

Na hata chama tawala bila kutumia Dora, wizi wa kura na vyombo vya usalama, uchaguzi wa mwaka 2015 ndio ungekuwa anguko kuu lao.

JPM kupachikiwa uraisi haikutia hofu sana Kama ambavyo angepewa Bernard Membe, hata machungu ya matokeo ya uchaguzi yalivyotoka na kwenda kinyume na wengi tulivyotarajia kuwa Edward Lowassa ndie atakuwa mshindi wa kiti Cha uraisi, JPM akaonekana kuwa faraja na tarajio la wengi.

Usaliti wa JPM uliokuja kutokea baada kuapishwa kuwa Raisi.

1. Kutoa kauli kuwa hatofukua makaburi. Hii kauli ilitu-umiza wengi yani kwamba wakina Anna TIbaijuka, William Ngeleja, Andrew Chenge na mafisadi wengine hawatofikishwa mbele ya sheria kwa sababu tu hawajafanya uharifu huo kwenye serikali yake ya awamu ya tano.

2. Magufuli kuigawa nchi na kushindwa kulifanya taifa kuwa kitu kimoja. Toka JPM aingie Madarakani kuna mpasuko mkubwa wa kitaifa ameutengeneza na kuwajaza chuki watanzania chuki kisa tu siasa. Serikali yake imefumbia macho juu ya mauaji na utekejaji mwa watanzania waliofanyiwa vitendo hivi kwa kile kinachosemekana kumkosoa JPM au Serikali yake. JPM na viongozi wa chama tawala wamebaki kuhubiri amani yamkini hawaitendi amani Wala haki.

Hakuna uchunguzi wa kina na wenye mashiko umetolewa na serikali juu ya watanzania hawa Tundu Lissu (shammbulio ya kumtaka kumuua), Azory Gwanda (Uwepo wake alipo), Mohammed Dewji ( utekwaji wake), Ben Saa nane (Alipotelea wapi) n.k, pia mauaji ya kinyama ya viongozi wa vyama pinzani hakuna ripoti au taarifa yenye kuleta timamu na mantiki imetolewa na serikali ya JPM. Matukio haya yamekuwa yakigawa taifa na kupandikiza chuki kwa wananchi.
Vitendo hivi vimeongezeka kwa kasi tangu JPM aingie Madarakani na serikali yake.

3. Uminywaji wa Demokrasia nchini.Na hii imekuwa kinyume na matarajio tulio wengi tulitarajia Magufuli atatumia demokrasia iliyohainishwa kikatiba tupate kujenga taifa kwa pamoja ila imekuwa kinyume.
Tangu JPM na serikali yake iingie madarakani demokrasia katika tasnia na namna namna mbali mbali imekuwa ikiminywa wazi wazi.

>>Uhuru wa habari, waandishi habari na Vyombo vya habari, tasnia hii serikali ya Magufuli na serikali yake wameifanya tasnia hii kuwa ngumu katika utendaji na kuthibitisha sio tasnia salama kwenye serikali yake. Azory Gwanda mpaka hajulikani na alipo na hakuna uchunguzi wa vyombo vya usalama unaojieleza kuwa unaendeleaje kumtafuta. Mwandishi Kabendera kushinikizwa kukiri kosa lisilo lake. Hukumu ya Paul Makonda kuvamia kituo Cha Clouds Fm mpaka sasa haijafanyika. Bunge kupewa masharti ulushwaji wake kwenye Vyombo vya habari.

Leo hata ukiona mbunge au mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au kiongozi serikalinki anakula Rushwa au anafanya ufisadi au hawajibiki ukaseme ukaripoti kwenye Vyombo vya habari au uviite vipate tangaza habari,haviwezi fanya hivyo maana havina kinga na viongozi ndio wana Kinga, hii imedhirishwa wazi na serikali ya JPM maana kama mpaka Paul Makonda hajapata hukumu manaake ana kinga huyo na taarifa hiyo yenye ushihidi wa video ikatafsiriwa uvumi.

>>Uhuru wa kutoa mawazo na kujieleza. Tulitarajia JPM angetengeneza platform (uwanja mmoja) wa kusikiliza mawazo ya wananchi wake bila kujali anakosolewa kwa maslahi mapana ya taifa. Imekuwa Kinyume yake kila ataonekana kumkosoa au kukosoa au kutoa taarifa yote inayomhusu yeye au kumkosoa yeye Bali anatiwa mbaroni.

Abdul Nondo (mwanafunzi UDSM) lengo la kupiga picha na kuziweka mitandaoni zile hostel za Magufuli zilizojengwa na TBA kwa Bei nafuu, lengo la Nondo halikuwa kumhahibisha JPM juu ya zile nyufa zilitokea wakati jengo halina hata mwaka mmoja wa matumizi. Lengo ilikuwa kumuonesha JPM hii taasisi ya TBA sio ya kuaminika. Wakina Titho mpaka sasa kawatia mbaroni, Maxence Malo (JF founder) wanazidi kumuwinda kila siku bila mafanikio, iam Martin wa Twitter mpaka Sasa yupo ndani. Kigogo2014 serikali yake bado inamtafuta imtie mbaroni. Mange Kimambi pona yake kuwa Marekani la sivyo angekuwa hayati Mange Kimambi.

>> Uhuru wa vyama vya siasa. Toka JPM aingie Madarakani ameshiriki moja kwa moja serikali yake kuminya uhuru wa vyama pinzani na kununua viongozi wa vyama pinzani kwa kutumia mwamvuli wa kuunga mkono juhudi za JPM na serikali yake. Vyama pinzani kavinyima ufanisi na uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao na kueneza sera zao, huku Chama chake hakina sharti lolote na kinakuwa na ulinzi wa Vyombo vya usalama vikilinda mikutano yao au shughuli zao za kichama.

4. JPM kukengeuka kutoka mtendaji hadi kuwa mwanasiasa. JPM aliyekuwa naibu na waziri katika wizara za huko nyuma kabla ya hajawa raisi ni tofauti Sana na JPM raisi wa Sasa. JPM typically amekuwa mwanasiasa na sio mtendaji Kama huko awali alipokuwa akiongoza wizara. Tena Bora angekuwa mwanasiasa wa nchi zilizoendelea Kama Marekani au uingereza ambao huwa na maslahi mapana ya mataifa yao katika kila sekta na nyanja. Yeye amekuwa mwanasiasa wa kiafrika, wa kiafrika huangalia tumbo lake, watoto wake na chama chake. Mfano. Viongozi wa UVCCM Iringa na Arusha kwa kauli zile za kutaka Zitto Kabwe, mpaka Sasa JPM amekaa kimya. RPC wa Arusha kaenda kwenye kikao Cha CCM mkoa Arusha, anaongea wazi wazi kusema CCM na polisi lao moja, JPM mpaka Sasa hamna tako lolote hata kukemea hamna.

5. JPM kuamini yeye na CCM ndio wa kuleta maendeleo na mapinduzi ya kiuchumi. Kwenye kampeni aliahidi kushirikiana na viongozi au watanzania bila kujali itkadi ya aina yoyote. Kinyume chake baada ya kupata uraisi vyama pinzani wamekuwa maadui zake, maadui wa chama na taifa kiujumla hata Kama akiri kwa mdomo matendo yake yapo wazi. Bila kuwa CCM hupati na hatamu ya kuongoza, hata uwe na sifa Bora vipi. Chacha waitara baada ya kuhamia CCM ndio kapewa unaibu waziri. Anna Mghwira kapewa ukuu wa mkoa mpaka alipo jiunga CCM. Kitila Mkumbo nae kahamia CCM ndio kupata hatamu ya kuongoza.

6. Kubadili katiba na taasisi za serikali, alionekana Kama kiongozi shujaa ambae mwenye maslahi mapana ya taifa ambae angebadilisha katiba. Hata kwenye kamapeni alizungumzia swala la katiba lakini mpaka Sasa kimya hata kulizungumzia. Taasisi Kama ya msajiri wa vyama na NEC anaendelea kuzijenga kwa maslahi mapana yake na CCM.

Huyu ndie alikuwa anaweza kubadili Mambo mengi nchini, lakini kwa sababu nae amegeuka kuwa mwanasiasa wa kiafrika basi tutarajie kujengewa miundo mbinu tu, swala la kukuza ukuzaji wa uchumi tulisahau, katiba na NEC huru tusahau kabisa. Mifumo Bora ya kiutawala tuzidi kuota. Bunge huru na mahakama huru ibake kuwa ndoto yetu na tusichoke kuota. Upatikanaji wa haki haswa zinazovunjwa na CCM na viongozi wake tusahau kabisa.
Ukabila umekuwa mara nne.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom