Upinzani tuweni makini, kazi ya kutetea watenda maovu nchini haitatupeleka Ikulu

Lupyeee

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
2,683
2,820
Ni jambo la kusikitisha sana sisi wapinzani tumejipa Kazi ya kutetea kila mtuhumiwa tukizani ndio wananchi wanachotaka kumbe ndio tunashusha hadhi ya upinzani mbele ya wananchi!

Kitendo cha juzi cha upinzani kuungana na baadhi ya wabunge wa ccm, kutetea wauza madawa ya kulevya ni jambo la kusikitisha na kushitusha sana kwa usitawi wa upinzani nchini Tanzania.

Upinzani tujirekebishe jamii inatushangaa.!!!
 
Suala sio kupinga mapambano dhidi ya madawa hapa tunataka utaratibu utumike tena wa kishelia maana hawa wadudu, nawaita wadudu maana ni wauaji hatari wa Nguvu kazi, ukiwa na papara wanakushinda mahakamani maana wana hela nyingi sana za kulob kila watakapo,,,, ushahidi ulikuwa unazidi kupotea
 
Me Sijui kwanini wapinzani wanaogopa vitu vya kijinga
Wanadhani kwamba kuungana na serikali baadhi ya mambo watashuka chat kwenye siasa
Wanakosea Sana wapinzani
Upinzani ni ideology ambayo ipo tu Kwa wananchi wengi vichwani mwao
WATU hawawezi kuhama upinzani Kwa KUWA ETI upinzani umesifia mahakama ya mafisadi kuanzishwa
Upinzani uangalie agenda nyingine zitawafanya watanzania wasiwe na imani tena


Mfano ishu ya vita ya madawa wapinzani wangeacha hoja za sijui makonda kakosea sheria wenyewe wangeanzisha kampeni yao hata kama sio ya kuungana na serikali basi ya kutoa Elimu wote Kwa Pamoja wangejipatia Max nyingi Sana.. Sasa wenyewe wamekuja kumshupalia makonda kumbe watanzania wengi wanawachora tu. Upinzani msioogope watanzania wanajua mambo ya msingi ya kwenda nayo.. Sio lazima msifie viongozi waliopo kina magufuli mnaweza kuweka hoja nyingine nyingi tu.. Sema tatizo lingine ndo hivo Kuna zuio la kisiasa Kwa hiyo mnapopata NAFASI ya kuongea mnajikuta mnampaka rais Maneno machafu tena mnamshambulia Kwa hoja za kichoko mara sijui hajui KINGEREZA jaman Badilikeni lakini kwanza Badilisheni safu ya uongozi.. Imepwaya Sana.. SI mnaona CCM walivyo Wajanja wamempa pole pole uongozi sijui na Nani tena na nyie vijana wenu wapewe NAFASI kubwa kubwa huko chamani. Mwenyekiti kukaa karibu miaka 15 mnajichafulia
 

Sijaona mahali popote na siku yoyote, ambapo wapinzani (vyama vya upinzani) wamekuwa wakiwatetea watuhumiwa wa kuuza madawa ya kulevya, isipokuwa tu kama kuna legal procedures na haki ambazo zimevunjwa. Sidhani hata kama wewe ikitokea muda huu ukikamatwa na kuanza kutangazwa kuwa unadhaniwa kuhusika na makosa fulani, utafurahi! Ungependa kwanza uheshimiwe hadhi yako maana huwezi kupoteza hadhi yako kwa kutuhumiwa kutenda jambo fulani ambalo halijathibitishwa. Soma vizuri Katiba yetu Ibara 13(6). Hapo ndipo wapinzani wamekuwa wakitetea. Sasa kama unadhani kupiga kelele ili katiba iheshimiwe ni kutetea wauza unga, hilo ni jambo lingine, lakini kwa upande wangu naelewa hicho ndicho wamekuwa wakipigania - kuheshimu katiba na sheria za nchi katika kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya watuhumiwa.
 
Nimeshangaa Sana wapinzani Leo hii kujifanya wako upande wa Manji... Hahaha Manji huyu huyu mwana CCM ambaye kila deal tunaambiwa yumo.. Hadi niffah Leo hii anajifanya Manji anamjua Sana kwamba hawezi kuwa na kesi ya madawa.. Jamani upinzani angalieni mambo mengine sio.. Huyuhuyu Manji ambaye amekuwa CCM miaka yote kafanya mingapi kuwahujumu upinzani chaguzi za 2005 na 2010.. Leo hii kwenu mzuri kisa tu hii ni serikali ya magufuli. Asee Fikirieni kidogo tu.. Mtaona nini t unamaanisha msiwatetee nyie waacheni kama wameajiri watu wengi waacheni serikali ipate hasara si hii serikali hamuipendi?
 
Wewe wapaswa kuuelewa muktadha wa tukio lile, hakuna anayetetea wauza madawa ya kulevya bali wabunge walichopigania pale ni kutetea hadhi ya mhimili wa bunge
 
utawala washeria ndiyo unapiganiwa
 
Point yako ni ipi sasa, maana umechanganya mambo 20 kwa wakati mmoja.
 
Maswali ya msingi kwa vyama vya upinzani:
1) Je, viongozi wake wanaheshimu Katiba ya vyama vyao?
2) Je, vina mikakati sahihi, na tekelezi za kupambana na maovu katika jamii ambayo CCM imeshindwa tangu tupate uhuru?
3) Je, kuna mifano hai, katika halmashauri za miji zinaongozwa na upinzani, kuonesha jamii jinsi ya utawala bora na kufuata sheria? Kwa mfano mapambano ya madawa ya kulevya DSM, kabla ya kushutumu staili ya RC Makonda.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 

Mkuu umeandika jambo la maana sana.....bila ya shaka wewe ni miongoni mwa wale wachache wanaotumia vichwa vyao vyema.......

 
Mpinzani yupi katetea wauza unga, mtaje, kama huna jina hata moja toa upuuzi hapa.
 

Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa upinzani wa aina hii utatuvisha pale CCM walipotukwamisha......
 
Mpinzani yupi katetea wauza unga, mtaje, kama huna jina hata moja toa upuuzi hapa.

Hukuwa na sababu ya kumtusi.....hili ni jukwaa huru......kama yanavyoheshimiwa mawazo yako.....ndivyo na wewe unapaswa kuheshimu maoni ya wengine....hata kama yanakinzana na utashi wako......
 
Hatukutetea wauza bwimbi bali tulipinga utaratibu uliotumika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…