Kuelekea 2025 Upendo Peneza ahamia CCM, awananga CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,521
4,380
Aliyekuwa Mbunge wa Vitu Maalum Chadema, Mweka Hazina wa Kanda ya Victoria na Mgombea Ubunge Jimbo la Geita kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndg. Upendo Peneza, amehamia CCM leo katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi.

peneza.png

Safari hii haijaanza ndani ya Wiki moja, imeanza ndani ya muda mrefu sana, nikafanya mawasiliano na Viongozi na hatimaye wakakubali kunipokea, Wiki hii niliitumia kama nafasi yangu ya kumshukuru Mungu kwa miaka 15 aliyonipa nikiwa Chama cha Upinzani (CHADEMA) na kumuomba anipe nguvu, anipe ustahimilivu, anipe hekima, anipe busara na nguvu za kutumika kwenye Chama changu kipya (CCM)"

"Nilijiunga na CHADEMA kwa sababu nilikuwa na kiu ya kutafuta mabadiliko ya kweli ndani ya Nchi yetu, nakumbuka baada ya Baba yangu kusikia kwa muda mrefu sana niko kwenye Siasa siku moja akaniita akaniambia nimesikia kwa muda mrefu, akanishauri niache Siasa, akanipa hela akaniambia faya vitu vingine achana na Siasa, nikaendelea, baadaye siku moja akaniita akaniambia Upendo nakuona una dhamira ya kweli ya kutumika kwa ajili ya Siasa, tukaongea na baadaye akanishauri akaniambia sawa umeamua kujiunga na Siasa kwa nini usijiunge na CCM?, sababu nilizompa za kumkatalia zaidi ya miaka 15 iliyopita nilimuambia Baba huku ninaona fursa ya kuwa sehemu ya kutafuta mabadiliko ndani ya Nchi yangu, Baba kidogo alichokuwanacho akanipa akasema endelea na unachokifanya, nimekwenda na kumwambia kuwa sasa naanza safari mpya na pia amenipa baraka zake, safari hiyo niliyoianza miaka 15 iliyopita nilitamani nilitamani kuona Tanzania yetu ikibadilika, Tanzania yetu ikiwa bora, lakini leo nikiwauliza nyie wana CCM mliopo hapa kwa ukweli kabisa bila ushabiki au Wananchi wengine mlioko hapa leo niwaulize, hivi CHADEMA mnatuelewa kweli?

CHADEMA IPO KWA AJILI YA KUTAFUTA MABADILIKO YA WANANCHI?
"Kweli (CHADEMA) tuko kwa ajili ya kutafuta mabadiliko ya Wananchi?, kweli tuko kwa ajili ya kubadilisha maisha ya Watanzania?, baada ya kujiuliza maswali hayo, nikimuangalia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tangu siku anapishwa, ukifuatilia nilikuwa na interview na BBC niliwapa hisia zangu za kweli kwa maneno aliyotamka, Mama alitamka na aliahidi kuleta Nchi pamoja, Mheshimiwa Rais alitamka kuwaunganisha Watanzania, Mheshimiwa Rais alitamka kufanya reforms, kwa lugha nyingine na rahisi ya kutamka ni kwamba Mwanamageuzi kwa sasa wa kweli ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na ninasema hivyo kwa sababu ameongea na ametenda"


RAIS SAMIA ALITOA MALIMBIKIZO YOTE YA RUZUKU ILIYOSUSIWA NA CHADEMA
Kuna mtu kuongea ili aonekane mwema, kuna mtu kuongea ili kutuliza Watu na kuna mtu kuongea ili kufanyia kazi yale aliyoyaongea, Mheshimiwa Rais alivyoingia madarakani kabla ya jambo lolote lile aliwatafuta Viongozi wangu wa Upinzani kwamba njooni, turudi tuitengeneze Nchi, njooni tuzungumze, hayo ilikuwa ni awamu ya kwanza ya kutafuta maridhiano, ikaenda ikaenda, safari hiyo ya maridhiano ambayo Wananchi mlikuwa hamuijui safari ile ilikufa, tukaanza safari nyingine mpya ya maridhiano, mnafahamu kwamba CHADEMA tumekuwa tunasusia ruzuku, lakini Mheshimiwa Rais akakubali kutoa hiyo ruzuku na sio tu kutoa ruzuku lakini pia malimbikizo yote ya ruzuku"

OFISI MPYA ZA CHADEMA ZIMETOKANA NA PESA ZA RUZUKU
"CHADEMA tumekuwa tukipata ruzuku ambayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, mwaka 2015 mpaka 2020 ilikuwa inafika mpaka milioni 300, ukijumlisha na hela za Wabunge wa Viti maalum na Wabunge wa Majimbo Kwa miaka yote ni almost 5 Bilion lakini tulikuwa hatuna Ofisi nzuri ya Chama, tumelipwa malimbikizo ya ruzuku, hiyo Ofisi mnayoiona (Ofisi mpya ya CHADEMA iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam) ni matunda ya Pesa za ruzuku, jengo jipya mnaloliona ni matunda ya Pesa zilizokuwa zimekataliwa sasa Chama kikapewa, Watu wakamegana Megan kidogo pale, kuna Watu walitaka matumizi yawe mengine lakini wakasema hapana, iwe imetosha tukanunue Ofisi sasa Chama kikapata Ofisi mpya ambayo leo ndo inatumika"

RAIS SAMIA NI MVUMILIVU NA MSTAHIMILIVU
"Tulikuwa hatuna uhuru wa kufanya mikutano iliyofutwa kwa tamko la Rais na Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) aliirusha kwa tamko hilohilo la Rais, kwahiyo Mheshimiwa Rais akaruhusu mikutano ya hadhara na jambo moja na kubwa ambalo Watanzania inabidi tujifunze kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, jambo moja kubwa kama mengine yatatushinda lakini inabidi tujifunze kama Viongozi ni kuwa na uvumilivu na ustahimilivu" -Peneza "Kwenye ile mikutano tumemsema kwa lugha za aina yoyote ile tunazozijuwa, kwa lugha za kebehi, kwa lugha za namna yoyote ile unayoweza kusema lakini Mheshimiwa Rais ameamua kuangalia kilicho cha muhimu"

RAIS SAMIA ANATAKA TANZANIA YENYE DEMOKRASIA
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa) amekuwa Chachu ya kutafuta mabadiliko ya kweli ndani ya CCM na leo hii tunaona amemchagua Mheshimiwa Katibu Mkuu (Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu mpya wa CCM) anayefanana na adhma hiyo, amegundua Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anataka Tanzania yenye Demokrasia, anataka Tanzania ambayo Watu wanaheshimiwa haki zao, anataka Tanzania ambayo Wananchi na wanaweza kufanya shughuli zao huku wakiheshimiwa na haki zao zikipatikana"

NDANI YA VYAMA VYA UPINZANI HAKUNA DEMOKRASIA
"Ndugu zangu kwa masikitiko makubwa sana, kwamba Vyama vya Upinzani Kwa asili vinapaswa kuwa jicho la Demokrasia lakini leo ukiangalia mienendo na matendo, hata leo unataka kupigania Tume Huru ya Uchaguzi lakini ukifuatilia yaliyoko ndani kwao unaweza ukashika kichwa, unasimamia ubadhirifu, fuatilia yaliyoko ndani unaweza ukashika kichwa kwahiyo mwisho wa siku unasema anayejiita jicho la Demokrasia na yeye anahitaji kuangaliwa"


VIONGOZI CHADEMA WAMEFANYA ULAFI NA UBADHIRIFU WA RUZUKU.
Na ndugu zangu jambo lingine ambalo wamegundua ni kwamba wamefanya biashara hiyo kwa muda mrefu sana, wamefanya biashara ya ulaghai kwa muda mrefu sana, wamefanya kwa ulafi mkubwa sana, wamenogewa lakini wameshtuka tayari 2024 hiyo inataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wameshtuka 2025 ni Kesho kutwa sasa kama huna uhalali kwa Watu unawafanyaje?, na unajuwa tena kwamba kuna biashara nyingine kule ya kufanya ubadhirifu kwenye ruzuku, wanataka ruzuku ya mwaka 2025 iwe nyingi halafu wanataka na huu Uchaguzi kidogo hali ichangamke, Uchaguzi ujao washinde sasa unaanzaje?, unawaingiza Watu Barabarani kidogo unapima joto kujuwa wamekuja wangapi ili kujuwa kama kamtaji bado kapo"
 
Siasa kama Mapenzi tu na Wabunge wa viti maalum kama Madanga(tabia za kimalayamalaya) tu wanahamia palipo na uhakika wa Pesa/teuzi.

Hoja ya chadema ya kuondoa mfumo wa viti maalum na kuwaingiza wanawake katika mchuono wa kawaida itasaidia sana kuondoa wanawake wa hovyo hovyo wenye tabia za kimalayamalaya bungeni.
 
Siasa kama Mapenzi tu na Wabunge wa viti maalum kama Madanga(tabia za kimalayamalaya) tu wanahamia palipo na uhakika wa Pesa/teuzi.

Hoja ya chadema ya kuondoa mfumo wa viti maalum na kuwaingiza wanawake katika mchuono wa kawaida itasaidia sana kuondoa wanawake wa hovyo hovyo wenye tabia za kimalayamalaya bungeni.

Ulitaka kesema "malaya wa kisiasa" kama alivyosema Mwalimu?.
WhatsApp Image 2024-01-22 at 14.00.24.jpeg
 
Aliyekuwa Mbunge wa Vitu Maalum Chadema, Mueka Hazina wa Kanda ya Victoria na Mgombea Ubunge Jimbo la Geita kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndg. Upendo Peneza, amehamia CCM leo katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi.

#TunaendeleaNaMama🇹🇿
#KAZIINAENDELEA
#VitendoVinaSauti🇹🇿
#CCMIMARA
Covid -19 wote ni CCM, wanashindwa kukabidhiwa kadi kwa sasa maana itabidi CHADEMA iteue wapya, but inafahamka hata na mtoto mdogo.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Vitu Maalum Chadema, Mweka Hazina wa Kanda ya Victoria na Mgombea Ubunge Jimbo la Geita kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndg. Upendo Peneza, amehamia CCM leo katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi.

#TunaendeleaNaMama🇹🇿
#KAZIINAENDELEA
#VitendoVinaSauti🇹🇿
#CCMIMARA
Safi, watampa na hela ya kula?
 
Ni haki yake ya Kikatiba. Mwacheni awe huru. CHADEMA siyo mama yake na CCM pia siyo mama yake. Siku akiona na CCM hakumfai ana uhuru wa kuhamia hata UPDP ya Mhe. Dotuvwa a.k.a mzee wa Kiwanda cha sihala au kwa Mhe. Hashim Rungwe almaarufu mzee wa Ubwabwa.
 
CHADEMA watabaki wasiojitambua tu na wavuta bangi kama Mdude Nyagali ambaye kichwani hazisomi.
Nimengalia profile yako , umejiunga 2022 baada ya kufeli MEMKWA, sikushangai maana ilimradi ule kwa shemeji yako na uende chooni na kula huna lingine, zaidi shukuru TASAF inawapatia fedha ya mahindi muweze kuona kesho.
 
My Take
Kama una akili huwezi Baki kwenye chama Cha malalamiko 🤣🤣

=======

Aliyewahi kuwa mbunge wa viti maalum wa Chama cha Demokrasa na Maendeleo @ChademaTz
mkoa wa Geita, Upendo Peneza, ametangaza kujiengua na chama hicho na kujiunga na @ccm_tanzania
kuanzia sasa.

Peneza ametangaza uamuzi huo Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi.

Aidha, Peneza amepingana na wito wa Mwenyekiti wa CHADEMA @freemanmbowetz
wa kuitisha maandamano ya kupinga muswada wa sheria za uchaguzi ambayo yamepangwa kufanyika Januari 24, mwaka huu.

EATV
 
Back
Top Bottom