Unaweza kujilinda kwa kutumia akili, macho, na masikio

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,313
2,641
Habari wakuu natumai mpo sawa na majukumu yanasonga nafsi yangu inanisukuma kuandika jambo ambalo pengine akitokea mwandishi mzuri linaweza kutusaidia sana


Mwili unahitaji ulinzi 24 hrs ndio maana kuna baadhi baadhi ya viungo mungu kaviweka na sio kwa lingine ila ni kulinda eneo husika mfano kope za macho huwezi kuingiwa na kitu chochote machoni chenye kuhatarisha macho kabla kope hazijahisi hatari na kulinda jicho kuna uwezekano mkubwa kope huona adui wa jicho kabla hata jicho halijaona, vipo viungo viingi mungu katupa ili vitusaidie
Kwahiyo mwili una jilinda wenyewe kwa karibu 75%
Bahati mbaya 25% inahitaji akili kushirikishwa

Kuna hatari nyingi tunakumbana Nazo katika maisha kwa UZEMBE MKUBWA nitatoa mfano mmoja
Embu fikiria upo zako mtaani bar sokoni ama popote kwenye mikusanyiko ya watu baada ya mizunguko yako unakuja kugundua kuwa mfukoni mwako umeibiwa pesa ama ndani ya gari lako umeibiwa vitu vyako kama nyaraka,laptop na ama tu gari lote limeibiwa unajua baadae asilimia kubwa ya watu walioibiwa baadae wakikaa na kutuliza akili hujicheka na kujiona wao ni wazembe? Hujiona wazembe kulingana na jinsi ambavyo alivyoibiwa kitoto kabisa ,baadae sana hujuta hata kwa kukipa adhabu kichwa kwa kukipiga piga huku akikisuka suka na kujifyonza kwa kutokusaidia kuepusha wizi ambao umetokea
Swali: je? Tufanyeje ili tujilinde kwa kutumia akili zetu?

Jibu: akili nyingi za binaadamu ni kile kitendo cha Ku control mambo mengi kwa wakati mmoja mfano nimeona wanawake wengi wanaweza kuwa anamsuka mwenzie huku bega limebana simu anawasiliana na mtu huku macho nayo yanatazama TV na kila kitu kikaenda vizuri bila kuathiri jambo lolote

Hivyo basi popote pale ulipo elewa macho yako mawili yanauwezo wa kuona sehemu moja tu uliyo kusudia hasa mbele ya uso lakini nyuma na mbele yako kuna macho zaidi ya 4 ama zaidi ya mia moja yanakutazama wewe kwa lengo tofauti tofauti
Kwa kuwa unayo macho mawili unaweza kuyalazimisha jicho moja likaangalia kushoto na lingine kulia lakini pia macho yako lazima yawe mepesi kukagua usalama wa eneo kwa kuwachunguza watu wote waliyopo mbele yako ama nyuma yako nyuma yako unaweza kuyashirikisha Masikio kusikiliza ya nyuma na dalili zote za hatari macho yakabaki mbele kuangalia usalama wa mbele kuna msemo unasema kumjua adui yako ni nusu ya ushindi chukulia mfano wewe unatoka huko na mwizi anatoka kule mwizi kapanga ukipishana nae tu akukabe kama utayatumia vizuri macho yako unaweza kumgundua adui yako mapema kabla haja kuzuru na ukimkazia macho mwizi sio mwizi tu hata mbwa huwa wanaghairi kufanya madhara


Niishie hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…