Msomi Livelu

Member
Jun 21, 2024
24
30
Sisi tusio wasomi tunashunda kuwaelewa wasomi wetu hapa Tanzania. Kuna wakati wasomi wanakubali kuwa hatuwezi kupiga hatua bila ya kukopa, na ndio maana tunailalamikia Serikali kuweka mazingira wezeshi ili tukopesheke kwenye taasisi za kifedha.

Hii yote ni kukubali kuwa huwezi kuendelea bila ya kukopa. Na ni ukweli usiopingika kuwa ni watu wachache walio na mafanikio kiuchumi ambao hawajaingia kwenye njia hiyo ya kukopa.

Sasa unajiuliza mtu binafsi kukopa kwa maendeleo yake ni halali na serikali kukopa kwa maendeleo ya taifa ni Haram kweli?

Da jamani wasomi mnatuchanganya, na ndio maana huwa inakuwa vigumu sisi mavelu kuwafuata. Kifupi munakosa msimamo.
 
Back
Top Bottom