Umewahi jutia kwa kutomsaidia mtu?

ios 16

New Member
Sep 12, 2023
1
2
Nawapa salamu wanajukwaa, JF iendelee kuishi milele.

Naomba niingie kwenye mada, Je, umewahi kujutia kwa kutokutoa msaada kwa mtu ambaye alikuwa akihuhitaji na ulikuwa na uwezo wa kumsaidia lakini ukamuacha bila ya msaada wowote?

Hali hii imenikuta siku ya leo, lakini sitasimulia kisa cha leo bali kile cha takribani miaka kadhaa nyuma.

Ilikuwa hivi, wakati ninasoma masomo ya kidato cha tano na sita kwenye shule moja ya bweni nilikuwa na rafiki zangu watatu. Hawa urafiki wetu ulikuwa mkubwa sana japo nilikuwa na marafiki wengine ambao nao tulizoeana nao na kusaidiana mambo kadhaa kadhaa. Sasa katika rafiki zangu wale watatu mmoja alianza kusuasua kwenye masomo, ufaulu wake katika mitihani ya ndani ya shule ulikuwa ukizorota kwa kasi mno.

Awali nilijua uwenda baada ya kuachana na msichana ambaye alikuwa akijinasibu naye kwetu kwamba "tutaoana" alivyomuacha uwenda alipata shida kihisia iliyopelekea kupoteza muelekeo na niliamini angetengamaa baada ya muda mchache lakini hali haikuwa hivyo bado aliendelea kushuka tena kwa kasi kali. Kiush'kaji nilikuwa nikimpa 'moyo' na kumtaka asome kwa bidii na kumpa kampani na baadhi ya wadau wengine tukijaribu kusoma naye hasa hasa majira ya usiku, juhudi zilienda mbali kiasi cha kuongeza masaa kadhaa tukiwa tunamsaidia huyu rafiki yetu.

Baada ya kama mwezi alinifuata (rafiki) na kuniomba msaada kwa kuniuliza swali la kawaida tu, "brother, nimekwama nisomeje ili nitoboe?" kwa kipindi hicho kutoboa ilimaanisha kufaulu na kuingia chuo kikuu, niliona ni kama swali la kawaida sana na hata sikulipa uzito nikaishia kumwambia "Soma kwa bidii, piga msuli ile ile" baada ya hapo nikapotezea na kuendelea na mambo mengine, sikuwahi fikiri kwamba rafiki yangu angeweza kuwa na tatizo zito kiasi cha kunouliza swali lile ambalo nililichukulia kawaida tu.

Fast forward baada ya matokeo ya mtihani wa mock ya kidato cha sita kutoka rafiki yangu alipata division four ya mwishoni kabisa. Mara hii alirejea tena na kuniuliza swali lile lile ila niliishia kutoa majibu yale yale na kujazia mbwembwe nyingi nikidhani uwenda nilikuwa namsaidia kumbe haikuwa hivyo.

Baada ya matokeo ya kidato cha Sita kutoka rafiki yangu alipata division four tena na mimi binafsi nilijua uwenda angejiunga na diploma kwa cheti cha form four lakini wala haikuwa hivyo kwani alikuwa akiishi na bibi yake ambaye naye alikuwa akipata pesa kutoka kwa ndugu, hata soma ya rafiki yangu huyo hapo shuleni ilikuwa ya kubangaiza sana baada ya kuomba sana hela kwa ndugu ambao wengine walikuwa wakizima simu na hata kutopokea alipokuwa akiwapigia wakati wakuomba pesa za matumizi.

Kila nikikumbuka huwa nabaki kujilaumu sana na kujiambia uwenda kama ningemakinikia swali la msingi la rafiki yangu na kumsaidia labda angesimama kivyake na kufika chuo ambako naamini ndiko ilipokuwepo ndoto yake. Ila ya Mungu ni mengi mno.

Muwe na usiku mwema
 
Alinipigia simu na kuniambia mwanangu nakuhitaji nyumbani kuna jambo linanitatiza.
Kwakuwa nilikuwa naishi mbali na nyumbani nilichelewa kwenda kwa muda wa kama wiki. Wakati najiandaa kuwa kesho naanza safari ya kwenda saa nane mchana napigiwa simu ameshafariki.

Sijui hata ni kitu gani kilikuwa kinamtatiza hakuwawi kumwambia mtu yeyote na wala kuongea na yeyote. Labda ningewahi kwenda na kumsikiliza yawezekana tungekuwa naye hadi leo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom