Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 8,468
- 14,952
Habarini. Mwaka umeisha na ni wakati wa kujitathmini usomaji wetu na kuhabarishana juu ya vitabu tulivyosoma. Hii ni njia nzuri ya kujua vitabu vizuri vya kusoma. Binafsi nimesoma vitabu vifuatavyo, wewe umesoma vitabu gani?
1. The storm before the storm: Kitabu kizuri sana hiki, kinazungumzia siasa za Roma kabla haijatoka kuwa jamhuri na kuwa empire. Kuna uhuni, usanii na visasi vingi sana. Lakini pia kuna mazuri mengi ambayo hata leo hatujayafikia.
2. How i found Livingstone: Hiki kitabu setting yake ni Tanzania ya leo. Kizuri sana kwa Mtanzania kukisoma. Kinahusu safari ya H. M. Stanley kutoka Bagamoyo kwenda Ujiji kumtafuta Dr Livingstone. Ukisoma hiki kitabu ndiyo utaelewa kwa nini yale maneno, "Dr livingstone, i presume," ni maarufu sana. kiliandikwa mwaka 1871, unakuwa kama umerudi kuishi na wanyamwezi, wagogo na watu wengine wa miaka hiyo.
3. The communist manifesto. Hiki ndiyo msingi wa ujamaa duniani. Kinaelezea jinsi mabepari walivyotokea, jinsi ubepari ulivyozaa makabwela, na jinsi makabwela watavyopindua mabepari na kuweka ukomunisti. Fasiri yake ya kiswahili ipo.
4. Bury my heart at wounded knee: Kinaelezea jinsi wahindi wa Marekani walivyoteseka wazungu walipoanza kuvamia maeneo yao kwa kasi. Kinasikitisha sana. Wahindi waliteseka kuliko hata weusi waliokuwa watumwa, maana lengo la wazungu lilikuwa ni kuwaangamiza kabisa.
5. The little prince: Hiki ni hadithi ya kutunga. Ni hadithi simple lakini ina maana kubwa sana. Kitabu cha kwanza kiliandikwa kwa kifaransa, kimetafsiriwa kwa lugha nyingi kiasi kwamba ni kitabu cha pili kutafsiriwa duniani baada ya Biblia. nacho tuliandaa tafsiri yake ya kiswahili.
6. Breaking the Mirror of heaven: Kitabu kizuri kwa mtu anayevutiwa na Egyptology. Kinazungumzia historia ya idara ya vitu vya kale ya Misri, jinsi ilivyoendeshwa kihuni chini ya Zahi Hawass na historia fupi ya Misri kwa ujumla.
7. The princess and the Queen: Hii ni hadithi fupi ambayo series ya House of dragons imebase.
8. The three body problem:
Hiki ni kitabu cha kwanza kwenye series ya SciFi Remembrance of earth's past. ni science fiction bora kabisa kuwahi kusoma. Hii ni tafsiri, originally kiliandikwa kwa kichina. wachina wanatoa kazi safi sana.
9. The dark Forest: kitabu cha pili kwenye hiyo series.
10. death's end: kitabu cha tatu na cha mwisho kwenye series hiyo.
11. A canticle for Leibowtz: Kitabu kizuri. Kinahusu maisha ya kasisi mmoja kwenye jamii ya ki-utopia mabayo imechoma vitabu vyote. Hiki bado sijakimaliza.
12.Chuo cha ustaarabu kitabu cha pili: hiki kitabu kiliandikwa na daktari mmoja mzungu huko Kenya miaka ya 1930'S. kilikuwa kinafundisha juu ya kilimo na ufugaji bora na utunzaji wa mazingira.
13. Visa na hadithi: kinasimulia visa na hadithi nyingi za kale. Kimeelezea kwa kina hadithi ya maisha ya Buddha.
14.Mlango wa Historia: kinaelezea historia ya zamani na hekaya zake.