Umeshawahi kwenda kupima ngoma na partner wako halafu yeye akakutwa na virusi?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
905
1,406
Wakuu habari za mida hii, leo nimepata shock ya kubwa sana ambayo sijawahi kutana nayo before.

Ni hivi for the past few months baada ya kupima virusi vya ukimwi na kukuta sina niliamua kuanzisha utaratibu wa kupima na kila binti ninaetaka kuchapa kabla sijaenda kuchapa.

Kautaratibu haka niliamua kukaweka baada ya kugundua kuwa siwez kutumia condom maana nikivaa tu jamaa yangu huwa hasimami kutokana na kutopata utamu halisi mwisho wa siku huwa naishia kuomba game ipigwe kavu tu.

Basi kuna huyu mtoto matata sana kwa uzuri wa sura na umbo niliwahi kuwa nae ktk mahusiano miezi kama saba hivi iliyopita na niliachana nae aliponipiga kibom cha kumnunulia samani za ndani akidai alizonazo sio zake ni za rafiki yake ambae anarudi kutoka safar na anataka samani zake,nikaona hapa hapakaliki nikapiga chini mzigo.

Juzikati huyu binti akaanza tena kusumbua kwa vimeseji vya mahaba na vipicha vya uchokozi whasap, binti ana chura wa maana kwelkwel namm ndio ugonjwa wangu nikaona why not nisirudi tena niwe najilia vitu pendwa tena,nikamuuliza siku hz unafanya mishe gani akaniambia siku hz ni barmaid,kakengele ka hatari kakagonga kichwani kwangu maana barmaids nawajua walivyo mtelemko(nimewahi kula kama watano hivi kiulaini mno).nikamwambia binti tutaenda kupima kwanza lakini siku ya siku nikajikuta naghairi tu sikwenda kukutana nae.

Juz binti akanichokoza tena nikaona isiwe tabu nikamwambia Leo tukapime then nikamfumue,Leo asubuhi roho ilisita sana nikamtumia msg ya uongo kwamba nimepata dharula lakini baadae mizuka ya show ikanipanda baada ya kukumbuka ukubwa wa kalio lake na utamu wake kwa ujumla ikabidi kwenye saa kumi na nusu nimstue twende tukapime nikale mambo.

Tukiwa garini akaniambia anatakiwa kazini saa moja so ikabidi tutafute hospital fasta,ya kwanza tukakuta ina kipimo cha mtu mmoja tu,tukahangaika kutafuta nyingine kwa saa nzima bado kidogo nighairi maana tulipishana na lodge nyingine kweli nikicheki paja lilivyonona nikawa napagawa kweli muda unaisha na hospitali haionekani.

Baada ya kutafuta sana tukaelekezwa hospitali flani nikalipia tukapima jamaa kabla hajatoa majibu akatuhoji maswali kadhaa kujua mahusiano yetu yakoje mwisho akatupa majibu,nanukuu"brother majibu yako yanaonyesha hauna maambukizi lakini kwa upande wa Dada hapa kuna shida kidogo"dah hii statement sitaisahau,kilichofata akamwambia Dada majibu yanaonyesha una virusi vya ukimwi na akatuonyesha kipimo.

Sote tulistuka mno ikabidi nilipie binti apimwe tena na kipimo cha pili kikatoka vilevile HIV type 1,dah ikabidi tuondoke,tulipokuwa ktk gari japo alikuwa analia nilimdadisi kiasi akaniambia alipata bwana mmoja kati ya wateja wake wa bar akasex nae Mara mbili,anasema alimwambia wapime jamaa akagoma lakini mwisho akaamua kusex nae.

Nikamshauri asikate tamaa kesho aende bochi hospitali akapime tena apate uhakika maana pale wanapima kwa damu kubwa ila dah I'm in shock,nyege zote zimeisha kabisaa naona kabisa nimeponea tundu la sindano maana nisingeipata ile hospitali nilikata shauri nikapige hivyohivyo maana alishanihakikishia kwamba huwa anapima Mara kwa Mara na eti nisingemwambia mm tukapime asingenipa penzi Leo na angenihisi tofauti,hayo tuliyaongea wakat tunatoka ktk hospitali ya kwanza ile namm nikaamini kama anatahadhar hivyo yuko vizuri ila nikapime nae tu kutimiza wajibu lakini kumbe dah.

Ushauri wangu jamani tuepuke zinaa,ikishindikana tumia condom,ikishindikana Pima na mhusika kwanza na hata vile viporo vya siku nyingi ukitaka kupasha Pima nae kwanza usiamini yuko sawa kwa muonekano au maneno yake kwamba yuko makini na anapima Mara kwa Mara.

Asanteni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sanaa jamaa ila ili uwe salama usimwamini yeyote utakuja kufa bure.

Mwaka jana nilimpata mdada mmoja hivi mzuri nae kwa nyuma mmashaalah basi nikavuta geto kama kawaida yangu huwa sikai bila zana chumbani nami kupiga bila ndomu never forever hata uwe mzuri kama bayonz.

Basi mzee nikavuta ndomu nikaanza kuchapa .kawaida mimi naweza nikachapa hati lisaa bila kupees nikala mzigo hatarii mara demu akaanza kulalamika oooohhh ndomu imechoka tubadilishe mi nikaitoa kuandalia kwenye kibox kumbe ilibaki moja tu hiyo hiyo duuu na mzuka ukawA upo juu sasa nikawa kati demu anataka tumalizie gemu.ndomu j
Hamna dukani mbali....duuu

Si akaanza kuvuta mshine ili kuingiza bila kinga mwee akili inaniambia chapa tu nyingine inaniambia kausha wewe hamna kitu jibu likanijia hakuna namna nikairudie ile ile niliyoitoa nikaiva tena kw umakini nikazamisha mashine hata dakika haikuchukua nikapees hatari goli tamu balaa

Basi siku mbili zikapita nikamuomba tukapime ili tuwe tunaminyana kach kavu iseee demu ni positive kuja kufuatilia kumbe alikuwa baimed daaHh hadi leo siamini namshukuru mungu sana kumutw negative so siku ile ningemsimiliza hali ambayo ningekuwA nayo now mungu anajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Duh aisee hongera kwa kuukwepa huo mtego


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bwana mdogo mmoja, katika harakati za kutafuta mtu wa kuishi naye Kama mke.

Alipigwa simu na mjombake aliyeko huko Iringa , jamaa alipofika kule akakabidhiwa msichana akala mzigo kavu.

Aliporudi Dar akatujulisha kuwa kwa mjombake kakabidhiwa msichana yupo vzr , tukamuuliza vp uliua akatuyeyusha lkn wajuvi tulijua alimaliza.

Baada ya majuma kadhaa binti naye akaja Dar kutembea kwa jamaa yake, alimfikisha mpaka kwangu. Waliendelea na maisha ya Dar ,Iringa mpaka dada akawa mjamzito wakaelekea nyumbani kwao bwana.

Mama wa mshikaji wangu alikuwa ni nurse hivyo akawachukua mpaka hosp kwa ajili ya vipimo na yule binti aanze kliniki.

Daaah, jamaa alikuja kunisimulia kuwa majibu , yalikuwa binti ameathirika yy yuko salama.

Jamaa ananiambia alilia Sana ,lkn binti alikuwa mkavuuu, zaidi ya Kauzu.nikamwambia yawezekana yy alikuwa anayajua matatizo yake kabla.

Hivi ninavyotoa stori hii ni muda mrefu umepita, binti keshatangulia mbele za haki pamoja na kichanga.

Jamaa ni mzima wa afya , yapata miaka zaidi ya 10 Sasa.
 
Wewe umekua naye kwa muda gan na mpaka Mnaachana kila mmoja alikua salama kabisa ..

Tukichukulia kua mliachana wote mkiwa salama kabisa...... tangu muachane, ni miez saba imepita nasasa ndio mmekutana na mkapanga kupima????....... Nijibu ilo swali kwa ajili ya watu wajifunze kitu hapa.





Inawezekana kabisa, Kitendo chako cha kumkimbia kilimfanya awe Malaya.

Biblia unasema ivi, ukimuacha mwanamke umemfanya awe Mzinzi.

"What is yours will always be yours no matter what "
 
Mimi nilitongoza Demu akakubali ,yupo fresh mnoo akaniambia muda wowote nikimwitaji niwe free,Nikamwomba tukapime ,mada ikabadilika kuwa anamtu wake hivyo nimsamehe hakuniambia mapema hivyo kuwa na mm haiwezekani.
Nikaamua kupita pembeni.

Wa pili nilipiga mara moja na Ndomu bao moja nataka tuendelee akagoma akasema ana aleji na Kondomu,basi nikamwambia Tukapime tuwe huru akakubali Kila tukipanga analeta sababu kabanwa na majukumu .alamu ikalia kichwani mwangu nikakazania zaidi akanibadilikia akaniuliza- unataka Tukapime kwa sababu gani Utanioa ? Nikamwambia Ndiyo .
Alichoniambia hayupo tayari kuolewa siyo Leo au kesho wala keshokutwa.
Nikamsihi basi tuinjoyi kwani yy ana aleji na Ndomu amekaa kimya mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mimi nimemuacha demu sababu ni kupima tu,nna demu wangu mzuri tu ana weusi wa kawaida tu ila tako la haja kuasi akipita lazima ugeuke.Bas bana kama ujuavyo wanaume tumeumbiwa tamaa nikajikuta natongoza demu mwingine mweupe sana then mwembamba ,tukaanza kutoka pamoja matembezi nikiwambia aje kwangu anagoma kisa anadai ni karibu sana na kwao labda twende guest,basi siku zikasogea nikawa mvivu kuomba mzigo maana nna sehemu napata mpaka ikafika hatua yule binti akaondoka pale akaenda kuishi kwingine na akaniahid atakuja kulala kwangu baada ya wiki moja.nikakubali ila nikapanga mbinu za kumuingia ili akubali kupima kabla ya kuja,nikampanga then nikamtumia pesa ili aende akapime then aje na hayo majibu yake na mimi nimuoneshe yangu.siku ikafika nikaona yupo kimya nikamuuliza akadai alitamani kuja ila ameona uvivu kwenda kupima,basi mi nikamlaumu then nikamwambia kesho yake aende ila kama asipoenda mi ni mtu mzima nitakua nimeshapata jibu kwamba hataki.siku ilipofika pia akawa kimya basi mi nikampotezea mazima maana sikua tayari kuweka bond uhai kisa penzi
 
Sitaki kabisa demu wa Iringa. Wa kwanza nilimpata lakini kwakuwa mi ni jasusi nikawa nacheki post zake Facebook nikaona comments mbili tofauti kwenye post tofauti. Moja ilisema "tushampoteza mtu hapo" nyingine nimesahau, nikawazamia wale walocomment wakanambia kazaliwa nao. Ukiona binti hataki mazoea na watu alokuwa nao au kusoma nao shtuka.

Mwingine chuo hapa nikawa natoka nae outing, naenda ghetto kwake na anakuja kwangu. Nikajipanga nimtokee maana alinivutia na tulielewana. Nikaja shtuka anataja Iringa, nikamchunguza mwili na mwonekano alert ikawaka kichwani. Siku moja akanambia nimsindikize kwa daktari wake wa ngozi nikajua sijakosea kumuwazia vile.
 
Kwa kipindi hiki, ni vyema Sana kuwa na vipimo vya Ngoma muda wote, ukikutana na mtu zoezi Hilo ndiyo kitu cha Kwanza.
 
Nilidate nae kwa miezi kama mitatu hivi kabla sijaachana nae na tulipima nae siku ya kwanza wakati nataka kupiga then tukaanza mahusiano,baada ya kuachana tumekaa mbali mbali taklibani miezi saba hv, baada ya kuachana nae niliendelea na utaratibu wa kupima kila ninapotaka kuwa na mtu na ndio maana hata yeye tulipotaka kulianzisha tena ikabidi tupime kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…