Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,371
ULINZI WA KIM JONG "KIDUKU".
Kama inavyofahamika dhahiri kuwa ni vigumu kwa mwanga wa mshumaa kudumu katikati ya upepo wa kimbunga unaoangusha maghorofa; vivyo hivyo ni vigumu hata kwa ‘inzi’ mwenye nia ovu kumsogelea Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Huyu ni kiongozi ambaye vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikimuelezea kwa namna ambayo imetofautiana sana na mtazamo wa Rais wa Marekani, Donald Trump na Mchezaji nguli wa Mpira wa Kikapu kutoka Marekani, Dennis Rodman’ waliokutana naye uso kwa macho na kushiriki naye ‘karamu’.
Huyu ni kiongozi wa nchi maarufu kwa kutengeneza makombora hatari ya nyuklia. Imewahi kudaiwa kuwa inatishia usalama wa dunia kwa kumiliki makombora hayo. Lakini utetezi wake ni kwamba kama nchi ndogo inayotishiwa na Marekani na washirika wake, imeamua kutengeneza ngao ya kujilinda endapo itaguswa. Eti, ni kama wale wadudu wanaotoa harufu mbaya ukiwagusa, usipowagusa hiyo harufu hautaisikia hata wakipita mbele ya pua!
Kim Jong-un, ni mrithi wa kijiti cha uongozi kutoka kwa baba yake, Kim Jong-ill aliyefariki Desemba 17, 2011.
Hivi karibuni, vyombo hivyo vya Magharibi viliripoti taarifa zilizosambaa kwa kasi kuwa Kim Jong-un yu mahututi na kwamba huenda ameshafariki dunia. Rais Trump alitofautiana na vyombo hivyo. Alionesha kutoamini taarifa hizo; na alitupa dongo kwa vyombo vya habari vya Marekani kuwa kama taarifa hiyo imetolewa na CNN hawezi kuwa na imani nayo kwa asilimia zote. Na kweli, taarifa zilizothibitishwa baadaye ni kwamba kiongozi huyo yuko hai na ana afya njema. Usiri wa maisha yake ni sehemu ya mbinu zinazotumiwa kumpa ulinzi mkali kiongozi huyo.
Ikumbukwe kuwa hata CIA na FBI wa Marekani hawana uhakika na umri wake ingawa amesoma katika nchi za Ulaya. Mwalimu mmoja aliyewahi kumfundisha Kim Jong-un nchini Uswizi, aliiambia BBC kwenye makala maalum kuwa ‘anahisi’ wakati huo alikuwa na umri wa miaka 14, lakini hana ukakika. Hii ni kutokana na usiri wa maisha yake. Hivyo, wanakadiria kuwa atakuwa na umri wa kati ya miaka 36 na 37.
Moja kati ya mambo yanayomtofautisha na viongozi wengi ni mtindo wa ulinzi wa kipekee. Kwanza ni walinzi wake kumi na wawili (12) ambao hulizunguka gari lake na kukimbia nalo wakati wote wakihakikisha hakuna kinachoisogelea gari ya kiongozi wao.
Walinzi hao ambao walionekana pia kwenye mikutano miwili ya awali kati ya Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump, nchini Singapore na Hanoi,Vietnam, huvalia suti nyeusi na tai. Unaweza kujichanganya udhani ni ‘waheshimiwa wabunge’, kumbe ni makomando hatari.
Michael Madden, Mkurugenzi wa Taasisi rasmi inayofanya ufuatiliaji wa uongozi wa Korea Kaskazini (North Korea Leadership Watch), na mmoja kati ya wachambuzi wa masuala ya ulinzi wa viongozi, pamoja na vyanzo vingine anuai wamechambua uwezo wa walinzi hao na jinsi wanavyochaguliwa kati ya watu milioni 28.5 wanaounda Jamhuri ya Watu wa Korea.
Walinzi hao binafsi wa Kim Jong-un wanaokimbia pembeni mwa gari lake ni sehemu ya kikosi maalum kinachoitwa ‘Central Party Office #6’ au kwa jina rasmi ‘The Main Office of Adjutants’.
The Main Office of Adjutants
Timu ya The Main Office of Adjutant huchaguliwa kutoka katika kikosi cha makomando wa Jeshi la Watu wa Korea Kaskazini (KPA). Hata hivyo, pamoja na sifa ya kuwa makomando wenye uwezo wa hali ya juu, sifa nyingine muhimu hutazamwa katika kumchagua mlinzi wa kikosi hicho anayetakiwa kuwa pembeni ya kiongozi mkuu wa nchi ambayo iko kwenye mzozo mkubwa wa kijeshi na mataifa mengi yenye nguvu duniani, hususan Marekani na washirika wake.
Moja kati ya vigezo hivyo ni pamoja na kuangalia kimo cha komando anayechaguliwa. Anapaswa kuwa na kima chenye uwiano unaoendana na kimo cha Kim Jong-un.
Pia, lazima komando anayechaguliwa awe na uwezo mzuri na usio na shaka wa kuona vizuri bila kutumia miwani.
Makomando hao wanaopaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia silaha, kupigana mitindo ya ‘martial art’, hupewa mafunzo mengine maalum na makali ili kuwapa uwezo zaidi wa kipekee tofauti na makomando wengine katika kumlinda kiongozi wao.
Hii inahusisha pia mafunzo ya kukwepa kunaswa na adui kwa namna yoyote na kuokoa mtu katikati ya maadui wenye silaha.
Kama ilivyo kwa makomando wengine, hupitia mafunzo ya uwezo wa mwili kukabiliana na mateso, mafunzo ya tabia na mengine. Lakini kwao huwa na ziada ya kutunza siri na hata kufa katikati ya mateso wakiilinda siri ya nchi yao. Msisitizo mwingine ni uwezo wa mlinzi huyo kutazama/kuona kwa haraka na kusoma eneo lote alipo kiongozi huyo, kubaini hatari na kusoma saikolojia za watu hata kwenye hadhara.
Hii ni tofauti kidogo na walinzi wengi wa wakuu wa nchi ambao huvaa miwani maalum myeusi yenye uwezo wa kuvuta taswira ya watu kutoka kwenye hadhara, kupiga picha na wakati mwingine kubaini vitu vya kielectroniki vinavyoweza kuwa tishio.
Lakini kwa walinzi hawa wa Kim Jong-un wao macho yao halisi yanatumika zaidi. Pamoja na uwezo huo, wana uwezo wa kuzima tishio ‘lolote’ kutoka kwa watu wa pembeni dhidi kiongozi huyo kwa kutumia mikono na miili yao, hata kama watu hao wana silaha!
Kati ya walinzi hao wanaokimbia wakitengeneza mzungunguko kwenye gari, lazima awepo kiongozi mkuu wa kikosi hicho kutoka katika ofisi yao kuu kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, akiongoza na kuratibu kwa kushiriki moja kwa moja. Hivyo, naye ni komando wa makomando mwenye mafunzo ya ziada anayefanya kazi kama maafisa wengine.
Ili kuhakikisha wanaaminika, walinzi hawa hufanyiwa uchambuzi wa hali ya juu wa familia zao na uzao wao, kwa kuangalia angalau vizazi viwili nyuma. Hii hufanyika kwa maafisa wengi hata nchi nyingine, kwa lugha ya kigeni huitwa ‘vetting’. Lakini inadaiwa kuwa kwa Korea Kaskazini ufuatiliaji wa familia huchukua muda mrefu na uchambuzi huwa mkali sana. Hivyo, wafanyakazi wengi katika ofisi kuu ya ulinzi wake ni watu wenye uhusiano na familia ya Kim, au ni watu wa karibu wa familia za watu wenye nafasi za juu Serikalini wanaoaminika.
Ofisi kuu ya ulinzi wa kiongozi huyo (Office of Adjutants) inaaminika kuwa na wafanyakazi kati ya 200-300 tu; na zaidi ya nusu ya wafanyakazi hao ni makomando ambao ni walinzi wake binafsi, wengine ni madereva na wafanyakazi wengine. Kazi yao kuu ni kumlinda Kim Jong-un tu. Kazi ya kuangalia usalama wa eneo alilopo, chakula anachokula au vitu anavyotumia ni kazi ya kikosi kingine hatari kinachoitwa the ‘The Guard Command’ au the ‘GC’.
‘The Guard Command’ au the ‘GC’:
Nimeona ni vyema nikueleze japo kwa ufupi sana kuhusu kikosi hiki cha ‘The Guard Command’ au GC, ili upate picha ya tofauti ya kikosi cha walinzi wake wanaomuangalia yeye moja kwa moja na hiki ambacho kazi kubwa ni kuangalia maeneo aliyopo na vitu anavyotumia.
Kama umewahi kusikia inaelezwa kuwa ‘kinyesi’, mate au jasho la Kim Jong-un hulindwa kwa gaharama yoyote…. Basi hiki ndicho kikosi chenye kazi hiyo.
The Guard Command inahakikisha hakuna kitu chochote kinachodhuru kitakachomfikia kiongozi wao. Na pia, hakuna kinachotoka kwenye mwili wake kitakachoingia mikononi mwa adui au mtu asiyehusika. Si unajua tena, teknolojia ya DNA ikipata chochote kinachotoka kwenye mwili wako inaweza kueleza mengi kuhusu wewe!? Huwezi kupata hata unywele mmoja ulioanguka bahati mbaya wa Kim Jong-un, kuna watu wako kazini kuulinda saa 24 siku zote 7 za wiki.
Kikosi hiki cha the ‘GC’ Huhakikisha usalama wa eneo la ofisi yake, nyumbani kwake au maeneo yote anayotembelea iwe ni ndani au nje ya nchi hiyo.
Kikosi hiki pia huitwa the ‘Supreme Guard Command’, hulinda familia ya kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini. Kwa mujibu wa historia, kikosi hiki kiliundwa mwaka 1964. Na kati yam waka 1970 hadi miaka ya 1990 kilikuwa sehemu ya kikosi cha ulinzi binafsi wa Kim Jong-Il (Baba yake Kim Jong-un), lakini alikifanyia mabadiliko kuepuka majaribio ya kumpindua. Aliwaondoa makomando wengi na kuanzisha kikosi kingine alichokipa jina la ‘2.16 Unit’.
Lakini kilirejea tena jina lake ‘Supreme Guard Command’, na mwaka 2018 kilikuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri na Kim Jong-un nje ya nchi kumhakikishia ulinzi.
Kikosi hiki pia huundwa na makomando ambao wamepitia mtindo uleule wa kufuatiliwa, kufanyiwa tathmini, kuhakikiwa na hatimaye kupitia mafunzo makali ya kimwili, kisaikolojia na kitaalam kama wale makomando wa ‘The Main Office of Adjutants’.
Mfano mzuri kwa wale waliofuatilia safari ya Kim Jong-un nchini Singapore, zilishuka ndege tatu kutoka Pyongyang, Mji Mkuu wa Korea Kaskazini kumsindikiza kiongozi wao, mbili kati ya hizo zilikuwa zimewabeba maafisa wa kikosi cha ulinzi kutoka ‘CG’.
Kikosi hiki chenye wanaume na wanawake, ndio waliokuwa walihakikisha usalama wa simu aliyokuwa akitumia Kim Jong-un na kumpa msaada wa ulinzi wa kimtandao kwenye kompyuta yake. Waliweka ulinzi mkali katika eneo la Hoteli ya St. Regis, ambapo Kim Jong-un alifikia.
Kadhalika, walihakikisha kila alichokula, kuvuta au kunywa nchini Singapore wanakipima kwanza kuhakikisha ni salama. Kikosi hiki pia kilikuwa na madaktari wawili wabobezi, mbali na madaktari wake.
Kwa ujumla, makomando kutoka kikosi cha GC, hutengeneza mzunguko wa pili baada ya makomando wale 12 wanaomlinda, ingawa mzunguko huu huwa hauonekani kwa uharaka. Pia, wakiwa nchini Korea Kaskazini huunda mzunguko wa tatu ambao unakuwa karibu na watu wanaojipanga katika maeneo anayopita kiongozi huyo.
Kwahiyo, wakati wale walinzi 12 wanaokimbia kuzunguka gari alilopo Kim Jong-un wakiwa kivutio cha macho ya wengi na taswira ya ulinzi wa kiongozi huyo, nyuma ya pazia huwa kuna mizunguko mingine miwili ya ziada isiyoonekana dhahiri ambayo ni huweka ulinzi mkali zaidi kuhakikisha hakuna hata ‘inzi’ mwenye nia ovu anayesogea karibu na kiongozi huyo.
Hii ni sehemu ndogo ya ulinzi binafsi wa Kim Jong-un, kiongozi mwenye umri mdogo unaosadikika kuwa ni kati ya miaka 36 na 37. Ingawa ukisoma kwenye wekipedia wameamua iwe 36 kwa maana kuwa amezaliwa mwaka 1984. Moja kati ya vitu adimu zaidi kupata nchini humo ni taarifa kuhusu Kim Jong-un na Serikali yake, hiyo ni siri kuu hadi wao wenyewe waamue kukupatia. Wananchi wanaishi ‘kizalendo’ kutokana na jinsi walivyofunzwa kuanzia utotoni kumheshimu kiongozi wan chi hiyo na Serikali. Ni nchi ya kikomunisti. Sauti ya Kim ni sauti ya kiongozi na huheshimiwa kama amri inayopaswa kufanyiwa kazi ipasavyo. Na karibu kila kijana hupewa mafunzo angalau ya msingi ya kijeshi.
Kwa makala kadhaa nilizowahi kuziona, kwa jicho la tatu wananchi wa Korea Kaskazini wanaishi maisha bora kuliko baadhi ya wananchi wa nchi kadhaa za Bara la Asia. Ingawa kinachosimuliwa sana mitandaoni kinaogofya kuhusu nchi hii, haina maana kuwa ndani ya Korea Kaskazini watu hawatabasamu. Kama ilivyo kwa nchi nyingi, wapo wanaotabasamu na wapo wanaolia.
Rais Trump ambaye awali aliwahi kukaririwa akimuita Kim Jong-un kuwa ni ‘mwehu’ na kumpa majina ya dharau kama ‘mtu mdogo anayemiliki makombora’, baad a ya kukutana naye na kufanya mazungumzo alibadili mawazo. Trump alisema amegundua Kim ana akili kubwa, anajua kufanya makubaliano kwa ajili ya nchi yake. Pia, Trump alisema Korea Kaskazini inaweza kuwa kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani endapo itaondolewa vikwazo.
Kim ameliongoza taifa hilo kuwa na silaha za hatari na ulinzi wa ajabu. Ni nchi ndogo ambayo idadi ya watu wake ni takribani nusu ya idadi ya wananchi wa Tanzania. Uhusiano wake imara na China na washirika wake pia ni moja kati ya mambo yanayowapa nguvu zaidi.
Video ikionyesha Kim Jong-Un akiwa na Vladimir Putin (Tazama ulinzi wake)
Zaidi: Bonyeza HAPA