Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 108
- 195
Februari 6 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji. Mila hii ingawa inapingwa vikali, bado inaendelea kufuatwa na baadhi ya makabila.
Rhobi (sio jina lake halisi) ni binti wa Kikurya aliyekuwa akisoma katika shule moja ya msingi mkoani Mara. Binti huyu alikuwa na ndoto ya kuwa daktari katika siku zijazo, hivyo alijitahidi sana katika masomo yake ili kutimiza ndoto hiyo. Lakini, ndoto hiyo inakatizwa ghafla baada ya baba yake kuamua kumuoza kwa mahari ya ng’ombe 15. Kutokana na amri ya baba, binti yake huyo alikeketwa, lakini alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu kupita kiasi.
Yaliyompata Rhobi yamewapata wasichana na watoto wengi wa kike, kupoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kufanyiwa ukeketaji. Kuna baadhi ya wanawake wanashikilia mila hii na kutaka iendelee. Brenda Declan (sio jina halisi) ambaye kwa sasa ana miaka 37 hivi, ni mmoja wa wanawake wanaopenda mila hiyo iendelezwe. Brenda alikeketwa na kuolewa akiwa na umri mdogo sana. Brenda anayetokea kwenye jamii ya Wamasai na mama wa watoto watano, anasema tayari amewakeketa watoto wake wote wa kike, kwa sababu mila hiyo ni nzuri na inampa mwanamke hadhi katika jamii.
Takwimu za Taarifa ya Demografia na Afya za mwaka 2012 nchini Tanzania zinaonyesha kuwa, pamoja na jitihada za kutokomeza vitendo hivyo, bado kuna mikoa mitano nchini Tanzania ambayo inaongoza kwa ukeketaji. Mikoa hiyo ni Manyara inayochukua asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha asilimia 41, Mara asilimia 32 na Singida asilimia 31. Lakini inaaminika kuwa, matukio ya ukeketaji yanaendelea kupungua.
Mfano, wilaya ya Simanjiro ilikuwa inaongoza kwa ukeketaji katika miaka kadhaa iliyopita, lakini kutokana na juhudi kubwa kuelimisha jamii ya huko kuhusu athari za ukeketaji, mila hiyo kwa sasa haiendelezwi kwa kiasi kikubwa, ingawa bado kuna wale wanaopenda kuhakikisha watoto wao wa kike wanapitia kitendo hicho. Jambo hilo lilifanikiwa kutokana na kutolewa kwa elimu kwa wazazi, walezi na hata wanafunzi kuhusu athari za tohara kwa watoto wa kike.
Serikali ya Sudan nayo imepitisha sheria inayotoa adhabu kali kwa atakayekutwa akifanya mila hiyo. Umoja wa Mataifa umesema, asilimia 87 ya wanawake nchini humo wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 49 wamefanyiwa mila hiyo yemye madhara makubwa kwa wanawake na wasichana.
Ukeketaji una madhara makubwa sana kwa mwanamke, kwani wataalam wa afya wanasema, athari za ukatili huo hutokea wakati wa kujifungua kwa mwanamke kuchanika kwani maumbile yake yanakuwa yamekaza na njia ya uzazi haifunguki yenyewe. Athari nyingine inayotokana na mila hii ni kwamba baada ya kufanyiwa kitendo hicho, binti anaweza kuvuja damu kwa muda mrefu, na hata kusababisha kifo. Pia mwanamke aliyekeketwa anaweza kupata maambukizi mara kwa mara katika njia ya haja ndogo, lakini kubwa zaidi, anakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa kama vile UKIMWI, kwa kuwa kifaa kimoja kinatumika kuwafanyia ukeketaji wasichana zaidi ya mmoja, bila kufanyiwa usafi.
Ni kwa mtazamo huu, tunaamini kwamba taasisi husika zitajitahidi kuchukua hatua kuhakikisha kuwa mtoto wa kike analindwa kutokana na mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati. Umefika sasa wakati wa kutunga sheria inayowalinda wanawake dhidi ya ukeketaji, sheria ambayo itaweza kuhakikisha kuwa hakuna nguvu wala vitisho vitakavyotumika kumlazimisha mtoto wa kike kukeketwa, kwani uhai wake unastahili kulindwa. Elimu pia iendelee kutolewa kwa wazazi, walezi, watoto wenyewe wa kike n ahata viongozi wa kimila na mangariba ili waweze kufahamu athari ya vitendo hivyo kwa mtoto wa kike na kuachana na mila hiyo potofu. Tukishirikiana kwa pamoja, tutahakikisha tunalinda haki isiyopingika ya mtoto wa kike.