Ujasusi wa CHADEMA ni utapeli?

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
mala.jpg

Awali yoyote niseme tu naumia sana kuona kijana mwenzangu akiwa hajulikani alipo na kubwa zaidi pia haijulikani kama yu mzima au ameshatangulia, na kwasababu hii sitaki kulitumia jambo hili kisiasa sababu najua si vema kutumia masahibu haya kisiasa.

Lakini hii haimaanishi kuwa sitakiwi kukosoa au kusema juhudi za CHADEMA katika kumtafuta Ben kama zinawacha maswali badala ya majibu.

Nyote mtakuwa mashahidi, kulipotokea tuhuma za ugaidi na kufuatiwa na kesi ya ugaidi kwa Mh Lwakatare, tuliona hatua za haraka za CC ya CHADEMA katika kuhakikisha Mh Lwakatare hatiwi hatiani kwa makosa hayo.

Mabere Marando April 14, 2013 aliongea na vyombo vya habari kwa naiaba ya CC ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine aliweka hadharani mawasiliano ya simu ya watu usalama wa taifa, wanasiasa na vigogo wengine wa serikalini. Kwa ruhusa yenu naomba niweke sehemu ya TAMKO HILO CHADEMA alilolisoma Mabere kwa wanahabari kwa niaba ya CC ya CHADEMA.

NANUKUU

"Kwa mfano, simu ya Mwigullu Nchemba, namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.

Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.

Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna Mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari na Machi 6 mwaka huu."

MWISHO WA KUNUKUU.

Si hii hivyo tu, CHADEMA chini ya katibu mkuu Dk Slaa ilinasa mawasiliano ya barua pepe kati ya Zitto na Msacky na mawasiliano hayo kuandikwa na gazeti la mwanahalisi la jumatano ya Desemba 9, 2009, gazeti ambalo linamilikiwa na kada na mbunge wa CHADEMA. Kwa kusoma habari hiyo ya kubenea bofya link hii

Si hii hivyo tu, CHADEMA ilisambaza kitu kilichoitwa ripoti ya siri juu ya njama za Zitto kwa chama hicho, pamoja na mambo mengine, ripoti hiyo iliweka hadharani mawasiliano ya simu na miamala ya kifedha kati ya Zitto na watu wengi kama vile Mchange, Prof Kitila, Nyakarungu, na wengineo wengi.

Pamoja na kwamba RIPOTI hiyo CHADEMA kupitia Mnyika iliikanusha kuwa haijatoka kwake, lakini haiondoi ukweli iliwekwa kwenye mitandao na wanachama wa CHADEMA, na ilisambazwa na wanachama wa CHADEMA na wengine wakiwa viongozi wa CHADEMA. Hii ilitosha kuashiria kuwa ripoti hiyo iliandaliwa na CHADEMA.

Ni mwaka wa jana tu nyendo za Dr Slaa ziliwekwa hadharani kwa kusambazwa picha zilizotokana na video za CCTV zilizopo katika hoteli aliyofanyia press. Hii ina maana CHADEMA waliweza kupata video hizo kutoka katika camera za usalama zilizofungwa katika hotel hiyo.

Hii yote yamanisha nini? CHADEMA linapokuja suala la kufuatilia nyenendo za mtu hasa kwenye mawasiliano ya simu na baruapepe wamejipambanua kama magwiji na siku zote husifika kwa kuwa na uwezo mkubwa katika ujasusi na udukuzi na hili linadhirishishwa pasina shaka kwa TAMKO la CHADEMA la Aprili 14, 2013 lililosomwa na Mabere ambalo sehemu ya tamko hilo nimelinukuu humu.

Suala la Ben limefanya si kwamba CHADEMA ionekane chama cha kisichokuwa na utu lakini pia ni chama kilichojaa viongozi wanafiki. Na hili laonekana katika sura mbili.

Mosi.
Kama CHADEMA na makada wake wana uwezo huo ambao nimeueleza hapo juu, alafu Tundu Lissu akafanya press huku akitegemea status ya facebook ya Ben iliyotaja namba ya simu iliyo mtishia maisha, na huku itaka jeshi la polisi ifuatilie mawasiliano ya mwisho ya Ben, ni dhahiri kuwa chama hiki hakina nia au hakijafanya juhudi za dhati za kumtafuta Ben.

Hebu vuta picha, Lwakatare aliposingiziwa ugaidi, chama kilifanya uchunguzi wake takriban wa muda wa mwezi mmoja na kisha CC ya CHADEMA iliketi haraka sana na kuja na tamko lilosheheni vielelezo vya mawasiliano ya watu, na tamko lile kimsingi ndilo lilopelekea Lwatare kufutiwa mashitaka ya ugaidi.

Ukimya wa CHADEMA ulitakiwa uje na taarifa za kijasusi na kidukuzi zenye kuonesha kabla ya Ben kujulikana kupotea alifanya mawasiliano na watu gani, kwa njia gani, kama vile ya barua ya pepe, simu za kuongea, sms, massanger ya facebook, whatspp nk. Lakini badala yake wanatujia na ujumbe ambao tunaujua sanjari na kulipigia goti jeshi la polisi ili liombe mawasiliano ya Ben kutoka kwa kampuni ya simu.

Hivi, walivyodukua mawasiliano ya Zitto, Mwigulu, Zoka, Ludovick, na wengineo wengi waliomba kwa makampuni ya simu au polis? Kwanini kwa mawasiliano ya Ben iwe lazima waende polis au kwenye kampuni ya simu? Na kwa maelezo ya CHADEMA na Lissu ni kama vile wanaituhumu TISS kupotea kwa Ben, hivi kama kweli TISS wamehusika, ni sawa kwa CHADEMA kutegemea kupata mawasiliano hayo kwa msaada wa polisi? Kama si sawa, ni nini hasa asbabu ya CHADEMA isifanye kazi zake za kijasusi na kidukuzi na kutuambia waliowasiliana na Ben ili uwe msingi wa kujua Ben alipo?

Hadi leo Ben hajulikani alipo, na si kwamba chama kilikaa kwa muda mrefu tu, lakini pia ukimya wake umeonekana ni wa kipumbavu baada chama kutokuja na kitu kipya zaidi ya ujumbe wa vitisho aliotumiwa Ben ambao kila mtu anaujua!

Kiko wapi kitengo cha ujasusi cha CHADEMA? Vipi kwa Lwakatare walifanya kazi nzuri lakini kupotea kwa mtu katika mazingira tata washindwe? Vipi waliweza kunasa mawasiliano ya baruapepe kati ya Zitto na Msacky lakini mawasiliano ya Ben wapigie goti Polis?

CHADEMA hawaoni kuwa wanadhima ya kuhakikisha Ben anarudi akiwa mzima? Hawajui kuwa, kutaja mawasiliano ya Ben kutawatisha watekaji wake(kama kweli katekwa) wasimuue kwa kuhofia kubainika? Au kitengo hiki na chama kwa ujumla kinaona kupotea kwa Ben ni suala la dogo? Au Ben hapaswi kutafutwa kwa kutumia rasilimali za chama? Au hii ndio maana ya ule ukimya wa Mbowe? Kwanini CHADEMA imemtelekeza Ben? Au ndio kutumia watu mithili ya kondomu ukishaijaza madhii na manii unaitupa huku ukijuta kwanini ulivaa?

Pili.
Huenda mawasiliano ya kijasusi na kidukuzi yaliyokuwa yanawekwa na CHADEMA na makada wao dhidi ya mahasimu wao wa kisiasa yalikuwa ni siasa za majitaka na urongo kama urongo mwingine tu wa kusaka kiki.

Hawana uwezo wa kunasa mawasiliano ya watu na kwa kukosa uwezo huo ndio maana hadi sasa CHADEMA, familia, na UTG wanaipigia magoti polisi ifanye mawasiliano na kampuni ya simu ambayo Ben alikuwa anaitumia ili watoe mawasiliano ya Ben.

Kama kweli hili, ndiposa watanzania wajue kuwa, chama hiki kimejaa uzandiki, urongo, uchochezi na kila haina ya ghilba zenye lengo kujinufaisha kisiasa bila kujali madhara ambayo watanzania watapata kwa vitendo vyao hivyo.

Habari zao za kijasusi wakati mwingine huleta uchochezi baina ya watu na watu, au watu na tasisi za serikali au na serikali, na mbaya zaidi baadhi ya watu wanaziamini.

Bado swali labaki, kama wana uwezo wa kijasusi na kidukuzi, na kama taarifa zao kijasusi na kidukuzi zina ukweli, wanachelea nini kufanya udukuzi na ujasusi juu ya Ben? Je, kwa sakata hili la Ben, hakufanyi taarifa za kijasusi na kidukuzi zilizowahi kutolewa huko nyuma na CHADEMA kuwa za urongo na uchochezi????

MWISHO.
Inasikitisha sana wakati Ben wetu na rafiki yetu hajulikani alipo, mwajiri na bosi wake yuko busy kuhakikisha Msigwa na waitifaki wake wanapata vyeo vikubwa katika chama. Hivi ndivyo CHADEMA inavyolipa wema wa Ben, hivi ndivyo CHADEMA inavyowafunza wanachama wake, lakini nao akili zao kama nyumbu, haya yote yanaingilia mdomoni zinatokea kunjiko kama chakula hawana la kuelewa na wala hawana mazingatio.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 DSM.
 
View attachment 449833

Awali yoyote niseme tu naumia sana kuona kijana mwenzangu akiwa hajulikani alipo na kubwa zaidi pia haijulikani kama yu mzima au ameshatangulia, na kwasababu hii sitaki kulitumia jambo hili kisiasa sababu najua si vema kutumia masahibu haya kisiasa.

Lakini hii haimaanishi kuwa sitakiwi kukosoa au kusema juhudi za CHADEMA katika kumtafuta Ben kama zinawacha maswali badala ya majibu.

Nyote mtakuwa mashahidi, kulipotokea tuhuma za ugaidi na kufuatiwa na kesi ya ugaidi kwa Mh Lwakatare, tuliona hatua za haraka za CC ya CHADEMA katika kuhakikisha Mh Lwakatare hatiwi hatiani kwa makosa hayo.

Mabere Marando April 14, 2013 aliongea na vyombo vya habari kwa naiaba ya CC ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine aliweka hadharani mawasiliano ya simu ya watu usalama wa taifa, wanasiasa na vigogo wengine wa serikalini. Kwa ruhusa yenu naomba niweke sehemu ya TAMKO HILO CHADEMA alilolisoma Mabere kwa wanahabari kwa niaba ya CC ya CHADEMA.

NANUKUU

"Kwa mfano, simu ya Mwigullu Nchemba, namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.

Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.

Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna Mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari na Machi 6 mwaka huu."

MWISHO WA KUNUKUU.
Kwa kusoma tamko zima bofya link hii

Chadema Blog: TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA, LIMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, APRILI 14, 2013 NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA MWANASHERIA WA CHAMA, MH. MABERE NYAUCHO MARANDO

Si hii hivyo tu, CHADEMA chini ya katibu mkuu Dk Slaa ilinasa mawasiliano ya barua pepe kati ya Zitto na Msacky na mawasiliano hayo kuandikwa na gazeti la mwanahalisi la jumatano ya Desemba 9, 2009, gazeti ambalo linamilikiwa na kada na mbunge wa CHADEMA. Kwa kusoma habari hiyo ya kubenea bofya link hii

Siri za Zitto nje | Gazeti la MwanaHalisi

Si hii hivyo tu, CHADEMA ilisambaza kitu kilichoitwa ripoti ya siri juu ya njama za Zitto kwa chama hicho, pamoja na mambo mengine, ripoti hiyo iliweka hadharani mawasiliano ya simu na miamala ya kifedha kati ya Zitto na watu wengi kama vile Mchange, Prof Kitila, Nyakarungu, na wengineo wengi.

Pamoja na kwamba RIPOTI hiyo CHADEMA kupitia Mnyika iliikanusha kuwa haijatoka kwake, lakini haiondoi ukweli iliwekwa kwenye mitandao na wanachama wa CHADEMA, na ilisambazwa na wanachama wa CHADEMA na wengine wakiwa viongozi wa CHADEMA. Hii ilitosha kuashiria kuwa ripoti hiyo iliandaliwa na CHADEMA.

Kusoma ripoti hiyo bofya link hii

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE | Kilewo 2015

Ni mwaka wa jana tu nyendo za Dr Slaa ziliwekwa hadharani kwa kusambazwa picha zilizotokana na video za CCTV zilizopo katika hoteli aliyofanyia press. Hii ina maana CHADEMA waliweza kupata video hizo kutoka katika camera za usalama zilizofungwa katika hotel hiyo.

Hii yote yamanisha nini? CHADEMA linapokuja suala la kufuatilia nyenendo za mtu hasa kwenye mawasiliano ya simu na baruapepe wamejipambanua kama magwiji na siku zote husifika kwa kuwa na uwezo mkubwa katika ujasusi na udukuzi na hili linadhirishishwa pasina shaka kwa TAMKO la CHADEMA la Aprili 14, 2013 lililosomwa na Mabere ambalo sehemu ya tamko hilo nimelinukuu humu.

Suala la Ben limefanya si kwamba CHADEMA ionekane chama cha kisichokuwa na utu lakini pia ni chama kilichojaa viongozi wanafiki. Na hili laonekana katika sura mbili.

Mosi.
Kama CHADEMA na makada wake wana uwezo huo ambao nimeueleza hapo juu, alafu Tundu Lissu akafanya press huku akitegemea status ya facebook ya Ben iliyotaja namba ya simu iliyo mtishia maisha, na huku itaka jeshi la polisi ifuatilie mawasiliano ya mwisho ya Ben, ni dhahiri kuwa chama hiki hakina nia au hakijafanya juhudi za dhati za kumtafuta Ben.

Hebu vuta picha, Lwakatare aliposingiziwa ugaidi, chama kilifanya uchunguzi wake takriban wa muda wa mwezi mmoja na kisha CC ya CHADEMA iliketi haraka sana na kuja na tamko lilosheheni vielelezo vya mawasiliano ya watu, na tamko lile kimsingi ndilo lilopelekea Lwatare kufutiwa mashitaka ya ugaidi.

Ukimya wa CHADEMA ulitakiwa uje na taarifa za kijasusi na kidukuzi zenye kuonesha kabla ya Ben kujulikana kupotea alifanya mawasiliano na watu gani, kwa njia gani, kama vile ya barua ya pepe, simu za kuongea, sms, massanger ya facebook, whatspp nk. Lakini badala yake wanatujia na ujumbe ambao tunaujua sanjari na kulipigia goti jeshi la polisi ili liombe mawasiliano ya Ben kutoka kwa kampuni ya simu.

Hivi, walivyodukua mawasiliano ya Zitto, Mwigulu, Zoka, Ludovick, na wengineo wengi waliomba kwa makampuni ya simu au polis? Kwanini kwa mawasiliano ya Ben iwe lazima waende polis au kwenye kampuni ya simu? Na kwa maelezo ya CHADEMA na Lissu ni kama vile wanaituhumu TISS kupotea kwa Ben, hivi kama kweli TISS wamehusika, ni sawa kwa CHADEMA kutegemea kupata mawasiliano hayo kwa msaada wa polisi? Kama si sawa, ni nini hasa asbabu ya CHADEMA isifanye kazi zake za kijasusi na kidukuzi na kutuambia waliowasiliana na Ben ili uwe msingi wa kujua Ben alipo?

Hadi leo Ben hajulikani alipo, na si kwamba chama kilikaa kwa muda mrefu tu, lakini pia ukimya wake umeonekana ni wa kipumbavu baada chama kutokuja na kitu kipya zaidi ya ujumbe wa vitisho aliotumiwa Ben ambao kila mtu anaujua!

Kiko wapi kitengo cha ujasusi cha CHADEMA? Vipi kwa Lwakatare walifanya kazi nzuri lakini kupotea kwa mtu katika mazingira tata washindwe? Vipi waliweza kunasa mawasiliano ya baruapepe kati ya Zitto na Msacky lakini mawasiliano ya Ben wapigie goti Polis?

CHADEMA hawaoni kuwa wanadhima ya kuhakikisha Ben anarudi akiwa mzima? Hawajui kuwa, kutaja mawasiliano ya Ben kutawatisha watekaji wake(kama kweli katekwa) wasimuue kwa kuhofia kubainika? Au kitengo hiki na chama kwa ujumla kinaona kupotea kwa Ben ni suala la dogo? Au Ben hapaswi kutafutwa kwa kutumia rasilimali za chama? Au hii ndio maana ya ule ukimya wa Mbowe? Kwanini CHADEMA imemtelekeza Ben? Au ndio kutumia watu mithili ya kondomu ukishaijaza madhii na manii unaitupa huku ukijuta kwanini ulivaa?

Pili.
Huenda mawasiliano ya kijasusi na kidukuzi yaliyokuwa yanawekwa na CHADEMA na makada wao dhidi ya mahasimu wao wa kisiasa yalikuwa ni siasa za majitaka na urongo kama urongo mwingine tu wa kusaka kiki.

Hawana uwezo wa kunasa mawasiliano ya watu na kwa kukosa uwezo huo ndio maana hadi sasa CHADEMA, familia, na UTG wanaipigia magoti polisi ifanye mawasiliano na kampuni ya simu ambayo Ben alikuwa anaitumia ili watoe mawasiliano ya Ben.

Kama kweli hili, ndiposa watanzania wajue kuwa, chama hiki kimejaa uzandiki, urongo, uchochezi na kila haina ya ghilba zenye lengo kujinufaisha kisiasa bila kujali madhara ambayo watanzania watapata kwa vitendo vyao hivyo.

Habari zao za kijasusi wakati mwingine huleta uchochezi baina ya watu na watu, au watu na tasisi za serikali au na serikali, na mbaya zaidi baadhi ya watu wanaziamini.

Bado swali labaki, kama wana uwezo wa kijasusi na kidukuzi, na kama taarifa zao kijasusi na kidukuzi zina ukweli, wanachelea nini kufanya udukuzi na ujasusi juu ya Ben? Je, kwa sakata hili la Ben, hakufanyi taarifa za kijasusi na kidukuzi zilizowahi kutolewa huko nyuma na CHADEMA kuwa za urongo na uchochezi????

MWISHO.
Inasikitisha sana wakati Ben wetu na rafiki yetu hajulikani hayupo, mwajiri na bosi wake yuko busy kuhakikisha Msigwa na waitifaki wake wanapata vyeo vikubwa katika chama. Hivi ndivyo CHADEMA inavyolipa wema wa Ben, hivi ndivyo CHADEMA inavyowafunza wanachama wake, lakini nao akili zao kama nyumbu, haya yote yanaingilia mdomoni zinatokea kunjiko kama chakula hawana la kuelewa na wala hawana mazingatio.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 DSM.
wewe na ccm yako rudisheni rambirambi za wahanga bukoba.

swissme
 
Mwembe ukikosa maua husingizia mvua, kulikuwa hauna sheria ya mtandao lakini pia ilikuwa kosa kuingilia faragha ya mtu au mawasiliano ya mtu.
Ilikuwa kosa lakini ulikuwa ukipeleka mahakamani kesi kama hiyo kulikuwa hakuna kifungu kinachomtia mtu hatiani ndo maana ikaja sheria ya mtandao. Na hili ni tego kubwa sana kwa chadema na sitarajii kama watafanya kama kipindi kilichopita. Kumbuka chadema ina wanasheria nguli wanaojua nini cha kusema na kwa wakati gani
 
Huna hoja bali unarefer tu history!
Mazingira ya siasa za mwaka huu ni tofauti na yale ya mwaka 2013. Kuna cmmunications Authority na sheria ya mitandao,hawa wamezuia kabisa upashanaji wa habari. Kwa maana hio taarifa iliokuwa rahisi kuipata 2013 sio rahisi kuipata 2016 katika serikali hii babe isiyozingatia misingi ya democrasia na utawala bora.
 
kwa hiyo chadema ya sasa inahofu na mahakama?

wako wapi wanasheria nguli?

WACHA MANENO WEKA MUZIKI
 
Ilikuwa kosa lakini ulikuwa ukipeleka mahakamani kesi kama hiyo kulikuwa hakuna kifungu kinachomtia mtu hatiani ndo maana ikaja sheria ya mtandao. Na hili ni tego kubwa sana kwa chadema na sitarajii kama watafanya kama kipindi kilichopita. Kumbuka chadema ina wanasheria nguli wanaojua nini cha kusema na kwa wakati gani
kwahivyo wataka kusema chadema wanaogopa sana sheria ya mtandao kuliko kuogopa kumpoteza Ben???? nawaza tu,,, sababu najua kama watekaji wakijua mawasiliano yao yapo mezani,,,,, hakuna atakaye jaribu kumuua Ben, sanasana watamuachia haraka iwezekanavyo,,,,,
 
Huna hoja bali unarefer tu history!
Mazingira ya siasa za mwaka huu ni tofauti na yale ya mwaka 2013. Kuna cmmunications Authority na sheria ya mitandao,hawa wamezuia kabisa upashanaji wa habari. Kwa maana hio taarifa iliokuwa rahisi kuipata 2013 sio rahisi kuipata 2016 katika serikali hii babe isiyozingatia misingi ya democrasia na utawala bora.
Ujasusi ni pamoja na kupata habari zisizotakiwa kupatikana
 
Kiukweli hili swala la Ben limeleta sintofahamu kubwa.. Harafu siyo kawaida ya Chadema kuwa kimya kwa jambo kama hili.. Wabunge wao wapo kimya mr Mbowe naye hana time anajenga tu chama! Kama hamna jambo lililotokea
 
kwahivyo wataka kusema chadema wanaogopa sana sheria ya mtandao kuliko kuogopa kumpoteza Ben???? nawaza tu,,, sababu najua kama watekaji wakijua mawasiliano yao yapo mezani,,,,, hakuna atakaye jaribu kumuua Ben, sanasana watamuachia haraka iwezekanavyo,,,,,
Hivi unahabari kuwa juzi Tundu Lissu aliitwa polisi kuhojiwa kutokana na press conference yake na vyombo vya habari kuhusu hili suala la Ben!? Unahisi ni nini kitatokea kama watafanya kama unavyotaka wewe kifanyike ikiwa tu ile press conference ambayo hakutoa taarifa zozote za kijasusi mtu kaitwa kuhojiwa!? Hebu soma between lines mkuu halafu uone kama hoja yako ni sahihi
 
wanaogopa zaidi hili..... ulilolitaja kuliko kupotea kwa Ben????? ndio hoja yangu hiyo,,,lakini pia CHADEMA imefanya mangapi yenye kukiuka sheria na misimamo ya serikali??? mbona imefanya hivyo bila kuogopa???
 
Back
Top Bottom