Polisi mkoa wa Pwani ongezeni Juhudi za kupambana na majambazi. Kwani hali ni mbaya kufuatia matukio ya wizi wa kutumia silaha. Hawa jamaa ni kama Pwani ndo wamefanya makao yao kwa sasa. Wanafanya wanachotaka na muda wanaotoka na kwa staili ile ile ya kuvaa kininja.
Wiki iliyopita Maeneo ya Misugusu zaidi ya familia tisa zimevamiwa kwa usiku mmoja. Wiki moja kabla tukio kama hilo lilitokea maeneo ya viziwa ziwa. Usiku wa kuamkia leo aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Liwale ameua baada ya kuvamiwa na majambazi ambao walimpiga risasi.
Baada ya kumua Former Liwale DC wakavamia nyumba ya jirani yake ambaye kwake wamefanikiwa kuchukua shilingi elfu 87,000 za kitanzania na kumjeruhi, kwa sasa amelazw Tumbi hospital.
Pwani hali inatisha na sijui huku tunakoelekea itakuwaje.
Ujambazi unastahili kuunduwa mamlaka mahususi kama ilivyo Ile ya madawa ya kulevya!?!Polisi mkoa wa Pwani ongezeni Juhudi za kupambana na majambazi. Kwani hali ni mbaya kufuatia matukio ya wizi wa kutumia silaha. Hawa jamaa ni kama Pwani ndo wamefanya makao yao kwa sasa. Wanafanya wanachotaka na muda wanaotoka na kwa staili ile ile ya kuvaa kininja.
Wiki iliyopita Maeneo ya Misugusu zaidi ya familia tisa zimevamiwa kwa usiku mmoja. Wiki moja kabla tukio kama hilo lilitokea maeneo ya viziwa ziwa. Usiku wa kuamkia leo aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Liwale ameua baada ya kuvamiwa na majambazi ambao walimpiga risasi.
Baada ya kumua Former Liwale DC wakavamia nyumba ya jirani yake ambaye kwake wamefanikiwa kuchukua shilingi elfu 87,000 za kitanzania na kumjeruhi, kwa sasa amelazw Tumbi hospital.
Pwani hali inatisha na sijui huku tunakoelekea itakuwaje.
Polisi siyo wapiga ramli hadi wajue yote hayo, ukiona mafanikio ya polisi, jua kuna jitihada za makusudi za wasio polisi.Ni kweli Polisi ifanye jitihada za makusudi kulitatua hili tatizo, Mfano hapo kata ya Kibindu Hivi karibuni mifugo imekuwa ikiibwa sana.
Wewe umeshauri niniMkoa wa pwani una mapori mengi,kama umefika rufiji umeona,mkuranga vilevile,
ila tatizo hawataki ushauri,ndugu zetu,polisi na serikali kwa ujumla.
Hakuna kitu rahisi duniani kama kuzuia uharifu,serikali lazima itafute na kutumia maarifa ya wananchi wake ili kukabiliana na changamoto kwenye jamii.Haimaanishi kwamba walioajiriwa serikalini ndio wana akili nyingi na wana uwezo wa kutatua matatizo ya watanzania wote ila mtaani napo kuna watu wenye akili za vipaji ambavyo vinaweza kulisaidia Taifa.