TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Kwa Ufupi sana niseme, Afrika na Tanzania ikiwemo, miaka ya 1950 hadi 1990 kulikiwepo na Juhudi kubwa sana za Kudai uhuru, haki na Demokrasia. Jitihada hizi ziligharimu sana, kwa maana ya maisha kuharibiwa, mali na hata uhai wa wengine waliokuwa mstari wa Mbele wa Mapambano.
Mapambano ya Kudai Uhuru na Haki, Hayakuwa hasa mapambano ya Kudai Barabrara za Lami, maana Angola, Namibia hiyo vilikuwepo! Mapambano hayo hayakuwa Kudai kuwepo kwa Ndege mpya kwani SA sio tu walikuwa na Shirika la Ndege maarufu bali waliunda ndege, Magari na Vifaru. Mapambano haya hayakuwa ya Kutaka flyovers za mijini maana Pretoria na Johannesburg na Namibi hizozilijaa.
Mapambano haya hayakuwa ya Kudai Uwepo wa Panadol au Chloroquine hospitalini, Ingawa hayo yalikuwa ni ya Muhimu. Mapambano hayo yayakuwa ya Kudai mifumo ya maji maana mifumo ya maji ya Wajerumani na Waingereza ilikuwa The best!
Kumbe Tulimwaga damu kudai nini? UHURU, HAKI, DEMOKRASIA na Kuthaminiwa UTU wetu! Ati Leo Viongozi wanaolipwa Kututumikia Katika Taifa wanataka Tuwalipe sio kwa Mishahara tu Bali kwa Sarafu ya Uhuru wetu na Demokrasia yetu, Mbanu! Tena anataka Malipo hayo apewe kwa sera ambazo zimeshidwa, zinazopewa Budget ya asilimia 3% Nikitoa Mfano wa Sera ya Viwana ambapo Cherehani nne na Msishangae Mbuzi ya kukuna nazi vinazinduliwa na kuhesabika kama "viwanda" Masikini wa shetani"
SERIKALI:
Serikali ya Magufuli inafanya mambo mengi ya Moja kwa moja Ikiwa ni Pamoja na 1) kuzuia mikutano ya siasa, hivi je sheria inaruhuru leo hii kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa? Na kama jibu ni ndio, je chama hicho kitawezaje kushiriki Uchaguzi 2020 iwapo mikutano ya siasa kinachoweza kufanya ni ike ya kampeni ya 2020?
2) Huna aibu Kumzuia Lowassa aliyeshinda Arusha, Dar es salaam, Moshi, Mbeya etc ambako pengine hata kura tatu maeneo hayo hukupata ati Lowassa au Mbowe akiwa kama Mwenyekiti wa Taifa hawezi kufanya mikutano kwa ajili ya Kukijenga CHAMA chake, lakini wewe Unatumia kisingizio cha Urais ambao Ulishakushinda tangu mapema, kujenga CHAMA chako kwenye maeneo hayo! Tena kwa siasa chafu sana na zilizojaa hila?
BUNGE:
Ndugai ni Speaker Mnafiki na Wa hovyo kupata kutokea Africa! Swala la Adhabu ya Mnyika, Halima Mdee na Ester Bulaya. 1) Ndugai, hivi iwapo Wewe unaweza kumfungia Mbunge kwa Muda wowote? Unataka Kutwambia Unaweza kwa adhabu, kufuta Ubunge wa Mbunge kwa Kumpa adhabu Mbunge ya Miaka mitano, Tena kwa Kutumia Kura za Wapinzani wa Chama cha Mbunge huyo!
2) Kwa Mtindo wako wa Kutumia Kura za CCM waliojipa wingi Bungeni kwa Kuiba kura! Ni lini unadhani Mpinzani atapata haki kwa adhabu hizo? Kwa wingi wa Wabunge wa CCM, Ni hekima gani inakupa uhakika kuwa ipo siku watapiga kura kumwadhibu Mbunge mwenzao kwa Kumtusi Mbunge wa Upinzani au Kukiuka taratibu za Bunge? Nachoona ni kuwa hawatasita kuwaadhibu Wabunge Principled wa CCM kama Hussein Bashe!
MAHAKAMA:
Ni nani anaamini sababu ya Magufuli ya Kumteua Kaimu Judge haina lengo la Unafiki wa kishetani wa Obstraction of Justuce, kwa Kumweka Judge kwenye Makucha ya Vitisho Kuwa asipofanya atakavyo Ataondolewa? Kuwepo na Kaimu Judge ni Lengo chafu na Ovu la Kupokonya Uhuru wa Mahakama na kuushikilia Mikononi mwa mtu Mmoja, Waziri wa Sheria na Katiba amabaye Nilimwona ni ovyo na mwenye Ngebe uchwara anaweza kutetea kwa umilele jshetani huu, Lakini ukweli Utabaki ni Rais Mwovu sana, anayeweza muwa na Utamani na Kutekeleza Azma ya kutaka kuikanyaga Mahakama chini ya Miguu!
Ni kwa sababu hii Nasema Kuwa Uhuru, Haki na Demkkrasia Tanzania, Vinashambuliwa, Na Vinashambuliwa na Aliyekabidhiwa Mkuki na Ngao Kuvilinda, sasa ameamua kutumia Mkuki na Ngao Kuvitangazia Vita! Ati iwe ni Malipo yake ya Kununua Vibonbardiar, Kutekeleza Programs za Kikwete za Reli Pana, na Kuzindua Flyover miradi aliyoianza Mh. Kikwete!
Magufuli, Kama Mshahara, Chakula, Mavazi, Unavyopewa na Watanzania habikutoshi Unataka Ulipwe kwa Sarafu ya Uhuru na Demokrasia, Hilo haliwezekani, bora Ujiuzulu waachie wengine watakaoridhika na Mshahara wa Kawaida.
Magufuli, Kama Zulia Jekundu unalowekewa from Time to time halikutoshi, na Unataka Zulia la Katiba na Utawala wa Katiba, ati tukutandikie hivyo Uvikanyage viwe ndio badala ya zulia Mkuu nakwambia Patachimbika! Sana na sio Kidogo!