Mimi ni miongoni mwa vijana 3000 tulioajiriwa mwezi June 2016 ,niliajiriwa na tume ya utumishi wa mahakama Tanzania kwenye mahakama ya wilaya nilipewa mkataba wa kazi na kuanza kufanya kazi na wenzangu tulioajiriwa kwenye kanda ya mahakama tulikuwa watu 348, tulipewa mikataba na barua za kazi na tulianza kufanya kazi baada ya kufanya kazi mwezi mmoja tulipewa barua za kusitishiwa ajira zetu kwa mda ili kupisha zoezi LA uhakiki wa watumishi hewa tulipowauliza maafisa utumishi wa mahakama kuwa lini wataturudisha kazini ?walitujibu kuwa uhakiki wa watumishi hewa ukiisha tutarudishwa kazini toka mwaka Jana mwezi wa sita 2016 tupo nyumbani hatupewi taarifa yoyote na wala hatujui hatima yetu tupo na mikataba ya kazi na barua za kupangiwa vituo vya kazi maisha yamekuwa magumu.
Kwa masikitiko makubwa mke wangu ameniacha katoro anasema kuwa nilimdanganya sikuajiriwa na serikali kwenye idara ya mahakama ameniachia watoto watatu wadogo mmoja ananyonya kisa mimi nimesimamishwa kazi kwa mda usiojulikana nimeaibika kwenye jamii maana niliaga na kuwatarifu ndugu zangu kuwa nimepata ajira kwenye mahakama sasa hivi ukoo unajua kuwa niliwadanya kabisa ukoo unaniongea vibaya kuwa niliwadanganya kuwa nimeajiriwa kumbe hakuna nalia sana na aibu hii iliyosababishwa na serikali majirani kila siku wananiulizia kuhusu ajira Yangu hii maana walijua kuwa nimeajiriwa nashindwa kuwajibu nini nalia tu rais magufuli ,katibu mkuu utumishi wa umma, waziri angellah kairuki mmenifanyia unyama huu mungu yupo.
Baada ya kupangiwa kazi kigoma nilipanga chumba nikahamisha na mizigo Yangu kutoka geita mpaka kigoma kwa gharama zangu niliposimamishwa kazi sikupewa pesa za kurudisha mizigo hiyo hivyo niliiacha kigoma na nikarudi geita na mke wangu na watoto wangu tulianza kulala chini ya cement maana magodoro tuliyaacha kigoma kwenye nyumba ya kupanga nimelala chini na mke wangu na watoto mpaka mke wangu ameshindwa kuvumilia maisha haya mwishoe kanitoroka nalia na watoto nifanyeje kisa nimesimamishwa kazi bila kosa bora wasingeniajiri nisingehamisha mizigo Yangu na ningeendelea na maisha na familia Yangu Kodi ya nyumba imeisha huko kigoma nilipoacha mizigo Yangu mwenye nyumba anataka kuuza vitu vyangu ili apate fedha yake ya kodi inauma sana tena .
Serikali imekoswa huruma kiasi hiki omba yasikukute haya yaliyonipata .