AbaMukulu
JF-Expert Member
- Jan 1, 2018
- 2,053
- 3,582
Mechi ya Mbeya City na Yanga ilichabangwa Jumapili (juzi). Matokeo yalikuwa 1-1. Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kumekuwa na malumbano kuhusu hatma ya mchezo. Shida ilianza uwanjani dakika za mwishoni. Yanga walilalamika kuwa Mbeya City walikuwa 10 uwanjani na kipa wao jumla 11, wakati tayari walikuwa na kadi nyekundu.
Ni kweli, beki wa Mbeya City, Ramadhani Malima, alitimuliwa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 67, baada ya kumchezea isivyofaa, Juma Mahadhi wa Yanga.
Kipindi Malima anatolewa nje, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotupiwa kambani na Raphael Daud.
Mbeya City kupitia kwa Iddy Suleiman 'Ronaldo', walisawazisha bao dakika ya 90+2, yaani dakika 90 zilikuwa zimekwisha, kwa hiyo zilizokuwa zinachukua nafasi ni za nyongeza kama zilivyoamuliwa na mwamuzi. Katika mchezo huo refa Shomari Lawi aliongeza dakika 6.
UTATA ULIPO
Refa aliongeza dakika 6, ila mchezo ulikwenda hadi dakika ya 90+8. Dakika ziliongezeka kwa sababu golikipa wa Mbeya City alilalamika maumivu ikabidi atibiwe ndani ya dakika za nyongeza.
Dakika ya 90+6, kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa 'Fusso', aliongoza benchi la ufundi kumlalamikia mwamuzi wa mezani, mwenye kusimamia rekodi za mchezo kuwa Mbeya City walikuwa 11 uwanjani licha ya mchezaji wao mmoja kupewa kadi nyekundu.
Nilimsikia Nsajigwa akizungumza na mtangazaji wa Azam TV baada ya mchezo. Alisema japo hakuwa na uhakika ila mshambuliaji wa Mbeya City, Uliud Ambokile alifanyiwa mabadiliko lakini alirejea uwanjani.
Ni kweli, Ambokile alitolewa dakika ya 90+5. Wakati mabadiliko yanafanyika, alikuwa nje akitibiwa. Hivyo, inawezekana kocha wake alipokuwa anafanya mabadiliko ya kumpumzisha yeye hakujua.
Taarifa zinasema kuwa Ambokile alipomaliza kutibiwa, aliomba kwa mwamuzi kuingia uwanjani na alimruhusu. Joram alikuwa uwanjani kwa nafasi ya Ambokile ambaye naye alirejea uwanjani. Hivyo Mbeya City wakawa 10 ndani na kipa wao 11 kamili wakati walikuwa na kadi moja nyekundu.
Hivyo, Yanga wana hoja kuwa Mbeya City walikuwa wengi kinyume na ilivyopaswa. Hoja hiyo ndiyo ambayo inaleta maneno kuwa Yanga wamekata rufaa na wanadai wapewe pointi zote tatu japo walitoka sare ya 1-1.
JE, YANGA WASTAHILI POINTI 3?
Jawabu lipo ndani ya sheria 17 za mpira wa miguu ndani ya uwanja, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Kwa ufupi unaweza kuita Sheria 17 za Fifa. Hapa nieleze kuwa nikisema uwanjani namaanisha ile sehemu yenye kuchezewa mpira (football pitch).
Katika sheria 17 za Fifa, utata wa mchezo wa Mbeya City na Yanga unamalizwa na Sheria Namba 3 ambayo inazungumzia Idadi ya Wachezaji. Sheria inagusa maeneo manne. 1. Mchakato wa kufanya mabadiliko ya wachezaji. 2. Uwepo wa mtu wa ziada ndani ya uwanja. 3. Goli likifungwa kukiwa na mtu wa ziada ndani ya uwanja. 4. Idadi ya chini ya wachezaji.
Kwa vile hoja ya Yanga kuwa Mbeya City waliongezeka wakati wa kufanya mabadiliko, kwa mchezaji aliyebadilishwakurejea uwanjani. Na kwa kuwa wanadai wapewe pointi tatu kwa kuwa City walizidi, inanipasa kuchambua kipengele cha kwanza mpaka tatu.
Tukianza na mabadiliko; sheria inasema kuwa mabadiliko yatafanyika mpira ukiwa umesimama. Refa msaidizi ataonesha ishara, refa uwanjani atamruhusu anayetakiwa kutoka atoke kisha atamruhu wa kuingia. Anayeingia hataingia mpaka wa kutoka awe ametoka.
Mchezaji anayetoka halazimiki kutokea katikati ya uwanja, anaweza kutoka popote ili kuokoa muda. Refa pia anaweza kumwelekeza mchezaji atoke palipo na ukaribu ili kuokoa muda. Mpira hautaanza kama mabadiliko hayajakamilika.
Kama mchezaji anayetakiwa kutoka atagoma, refa ataamua mchezo uendelee na aliyetakiwa kuingia hataingia. Mabadiliko ya wakati wa mapumziko hutakiwa kukamilika kabla ya kipindi cha pili kuanza. Na kama ni mechi ya kuongeza muda (extra time), basi yafanyike kabla mpira kuanza upya.
ONGEZEKO LA MTU UWANJANI
Ikiwa kuna mtu asiyehusika na timu anakuwa uwanjani wakati mpira ukichezwa, refa anaweza kusimamisha mchezo. Hata hivyo, refa ametakiwa asisimamishe haraka endapo mtu huyo atakuwa hajaingilia mchezo. Refa anaweza kuacha mpira utoke au udakwe na kipa ndiyo atasimamisha mchezo ili amuondoe uwanjani huyo mtu.
Ikiwa mtu huyo anakuwa ameingia uwanjani na moja kwa moja ameuingilia mchezo. Hapo refa itabidi asimamishe mchezo haraka na kumtoa nje. Mtu huyo akishatoka, refa atadundisha mpira pale ulipokuwa mara ya mwisho alipopiga filimbi ya kusimamisha mchezo.
Endapo ofisa wa timu (kocha au ofisa yeyote wa benchi la ufundi) ataingia dimbani. Refa atasimamisha mchezo. Hata hivyo, refa anaelekezwa asisimamishe mchezo kama ofisa huyo wa timu hauingilii mchezo. Mpira ukitoka au kudakwa ndipo refa asimamishe mchezo na kuagiza ofisa husika atoke.
Refa amepewa mamlaka ya kumuondoa ofisa husika katika mazingira ya uwanja aende akatazame mpira jukwaani, kama anaona ofisa huyo ni tatizo kubwa zaidi. Kama refa anakuwa ameusimamisha mchezo ukiwa unaendelea, ataudundisha pale alipousimamishia.
Mchezaji nje ya dimba ni pamoja na mchezaji majeruhi aliyetolewa nje kutibiwa au ambaye hajaanzishwa kucheza ila yumo kwenye orodha ya wachezaji wa akiba. Mchezaji akitolewa nje kutibiwa hataruhusiwa kuingia uwanjani mpaka kwa ruhusa ya refa.
Ikitokea mchezaji aliyetolewa nje kutibiwa akiingia uwanjani bila ruhusa, refa atasimamisha mchezo ili kumuonya kwa kosa alilofanya na akiona kuna ulazima atamtoa nje. Refa anashauriwa asisimamishe mchezo kama mchezaji hasika hajauingilia mchezo.
Inapotokea mchezaji wa nje anaingia ndani ya uwanja kwa mabadiliko bila ruhusa ya refa. Atasimamisha mchezo na kumuonya kisha atamtoa nje. Refa pia anashauriwa kutosimamisha mchezo kama mchezaji husika atakuwa hajauingilia mchezo. Endapo mchezo utasimama, wakati wa kuanza, refa ataamuru mpira wa adhabu upigwe kuelekea goli la timu ya mchezaji husika.
GOLI NA MCHEZAJI WA ZIADA UWANJANI
Goli likifungwa, kabla ya mpira kuanza refa akagundua kulikuwa na mtu wa ziada uwanjani kipindi goli linafungwa, atalikataa goli kama 1. Mtu huyo wa ziada aliingilia mchezo 2. Huyo mtu wa ziada akiwa mchezaji, mchezaji wa akiba, mchezaji aliyetoka kwa mabadiliko au ofisa wa timu iliyofunga goli.
Ikiwa goli litafungwa na refa atagundua kuwa kulikuwa na mtu wa ziada uwanjani kipindi goli linafungwa, atalikubali goli kama 1. Mtu huyo hakuingilia mchezo 2. Mtu huyo ni mchezaji, mchezaji wa akiba, mchezaji aliyetoka baada ya kubadilishwa au ofisa wa timu iliyofungwa goli.
Ikitokea goli likifungwa, refa akalikubali na mpira ukaanza, kisha refa akagundua kulikuwa na mtu wa ziada kipindi goli linafungwa. Atasimamisha mchezo na kumtoa nje ya uwanja mtu wa zaidi. Hata hivyo, refa hashauriwi kusimamisha mchezo kama mtu aliyeingia uwanjani kimakosa hajauingilia mchezo.
Baada ya hapo, refa hapewi mamlaka ya kufuta goli, isipokuwa ameagizwa kutoa taarifa kwa mamlaka ya mashindano kuhusiana na tukio husika.
NANI ANAPATA NINI?
Baada ya kuchambua sheria, tunaona kuwa kulikuwa na makosa ya wachezaji wa Mbeya City kuzidi. Ambokile alirejea uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko. Je, aliingia kwa ruhusa ya refa? Kama ndivyo basi refa alijichanganya.Hakupaswa kumruhusu mchezaji ambaye alishatolewa.
Je, Ambokile aliingia uwanjani bila ruhusa ya refa? Ikiwa ipo hivyo, ilitakiwa refa amtoe nje na kuagiza adhabu ndogo ipigwe kwenda Mbeya City kama angesimamisha mchezo. Kuhusu Joram, kumbukumbu zote zipo kwamba aliingia kwa ruhusa ya waamuzi wote.
Joram aliingia dakika ya 90+5, hivyo Ambokile atakuwa alirejea dimbani kuanzia dakika ya 90+6 au zaidi. Ikumbukwe kwamba goli la Mbeya City lilifungwa dakika ya 90+2. Kwa maana hiyo, hakukuwa na mtu wa ziada uwanjani kipindi goli la Mbeya City linafungwa.
Nani anapata nini? Ipo wazi kuwa kama Mbeya City wangesawazisha goli kipindi wakiwa na mchezaji wa ziada uwanjani, kisha refa asingeona, lakini akaripoti kwa mamlaka ya mashindano, ingewezekana City kunyang'anywa pointi yao moja waliyopata kisha Yanga kupewa pointi zote tatu.
Goli lilifungwa kabla ya mgogoro husika. Uamuzi ulikuwa kumtoa nje ya uwanja aliyeingia kimakosa na kama ingebidi, ingepigwa adhabu ndogo. Hivyo ndivyo sheria inasema. Kwa hiyo hakuna namna Yanga wanaweza kupewa pointi tatu. Itakuwa ni tukio la kuchekesha kama itaamuliwa hivyo.
Mbeya City kama timu au Ambokile binafsi wanaweza kupewa adhabu nyingine lakini si kunyang'anywa pointi moja waliyoipata.
Nimeona nichambue hili baada ya kusoma upotoshaji ama wa makusudi au bahati mbaya kwa kutokujua. Kuna wanaosema Yanga watapewa pointi tatu. Wengine eti kuzidi uwanjani ni kosa la mwamuzi, kwamba hata mchezaji aliyezidi angefunga goli bado lingehesabiwa. Dooh! Tupeane breki jamani.
Ameandika Luqman MALOTO