Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
202
Khofu hutumika kama mbinu ya kuwanyamazisha watu, kuwapora haki zao, kuwalazimisha kufanya mambo yenye maslahi na anayejenga khofu na pengine kupunguza uwezo wa kufikiri kwa yule anayetiwa khofu.

Khofu ikizidi kwa yule anayekhofishwa huongeza ujasiri na humfanya kufanya mambo makubwa kuliko anayotarajia yeye kuyafanya.Mfano kama utakhofishwa kwa fimbo kwa maana utachapwa viboko kama hutaweza kuruka ukuta wa mita mbili ni kweli hutaweza kufanya hivyo.Lakini simba akija utashtukia upo upande wa pili wa ukuta,kwa maana kuwa hofu kubwa huondoshwa na khofu ndogo.

Historia inaonesha kuwa kwa vipindi tofauti yamekuwepo makundi tofauti yenye malengo tofauti ambayo yamejenga khofu kwenye jamii ya watanzania na kuweza kuyatekeleza malengo yao.

Miaka ya 1977 kabla ya mimi kuzaliwa nasikia kulikuwa na kundi la wanyonya damu kundi hili lilikuwa linachukua watu na kuwaua kwa malengo mbalimbali.

Miaka ya 1990 tulikua na kundi la komandoo yosso,ambao walikuwa wakipora mali kwa wananchi na kuwajeruhi kwa mapanga.

Miaka ya 2000 tulikua na kundi la panya road,ambalo nalo lilikua na lengo la kupora mali kwa wananchi na hivi sasa huko Tanga kuna kikundi cha watoto wa ibilisi ambacho kinapora watu mali na kufanya uharibifu mwingine.

Hivi karibuni limezuka kundi la watu waovu kwa jina la “Wasiojulikana”.Kundi hili la kijinai na la kihuni kama vilivyowahi tokea makundi mengine limekuwa likitumia mbinu mbali mbali kuwadhuru na kuwapora mali zao wananchi kwa kuwateka,na kuwafanyia mambo mabaya kinyume na taratibu za nchi.

Ndugu msomaji wa makala hii,nitoe tanabahi kuwa serikali yeyote duniani ina uwezo mkubwa sana wa kumfikia raia yeyote au mtu asiye raia ambaye yupo ndani ya nchi na nje ya nchi.

Uwezo huu wa kumfikia unatokana na mashirikiano kati ya serikali pamoja na uwekezaji wa serikali katika masuala ya usalama.

Zipo nchi ambazo sitazitaja zinazotumia makundi ya kigaidi kuangamiza watu katika nchi zingine,zipo serikali zinazotumia majambazi kuwaua watu kwa maslahi ya watawala bila kufahamika.

Pili sina shaka kuwa wananchi wanafahamu kuwa vyama vingi pamoja na asasi za kiraia ni ridhaa ya serikali,hivyo serikali kwa nanmna yeyote haiwezi kuwa mstari wa mbele katika kudidimiza demokrasia ya kweli nchini.

Dhamira ya kuwa na vyama vingi ilisukumwa na serikali na sio wananchi waliohitaji kuwepo kwa vyama vingi nchini pale kura ya maoni juu ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi ulipofanyika mwaka 1992.

Tatu serikali ina taasisi zake za kukabiliana na wavunjifu wa sheria,hivyo kama mwanasiasa au raia anavunja sheria zipo taratibu makususi za kukabiliana na wanasiasa hawa.

Mifano ipo mingi ambapo serikali imekua ikipeleka wanasiasa mahakamani na mahakama kuamua juu ya mashitaka ya kisiasa au wanasiasa.

Nne kutokana na uwezo wa hili kundi,ni wazi kuwa ufanyaji kazi wake ni wa kisomi na unatumia mbinu za kisayansi kutekeleza uovu wao.

Miongoni mwa mbinu inayotumika ni kuaminisha umma kuwa kuna uwezekano wa jeshi letu la Polisi kuwa ndilo linalojihusisha na kundi hili ili watu wasiweze kuwaza nje ya box kufikiri zaidi na kufahamu kundi hili.

Hivyo tuondoe mkono wa serikali kwenye hili kundi la kihuni,na tujaribu kuangalia ni wapi hili kundi linaweza kuwa linatoka.Kwa lugha ya kiusalama tuna sema tunapunguza duara la watuhumiwa.

Mtuhumiwa namba moja anaweza kuwa uholela uliopo katika vyombo binafsi vya ulinzi pamoja na kuwepo nguvu ndogo ya uhakiki wa walinzi katika makampuni binafsi na vyama vya siasa.

Mfano,mimi na wewe tunaweza kujiuliza kuna mtu anajua idadi ya walinzi wa chama mfano CHADEMA?Kabla ya uchaguzi 2015 kulikua na makundi maelfu na maelfu ya blue guard walienda wapi?

Walinzi wa chama cha CHADEMA maarufu kama Blue Guard wanatokana miongoni mwa wanachama wa chama ambao kwa namna moja au nyingine wanapata nafasi hizi sio kwa kufuata utaratibu maalumu.

Wananchama hawa hawana uhakiki juu ya tabia zao,hawana uhakiki juu ya matendo yao ya nyuma katika matukio ya kijinai.Mapendekezo ya nani awe katika kundi hili la walinzi wa chama yanafanyika kwa vigezo vya kimwili ambavyo ni uimara wa mwili na uwezo wa kutumia silaha.

Pili kuna viongozi wa upinzani wanatoa ushuhuda wa makundi ya watu wasijulikana,mfano matukio mengi yanayotokea kwa viongozi wa vyama mbalimbali yana uhusiano na masuala ya kisiasa,mfano wapo viongozi wa CCM waliwahi kuuliwa huko kibiti mkoa wa Pwani na Mtwara,Pia wapo viongozi wa vyama vya upinzania waliowahi kutoa tahadhari kwa serikali juu ya kutishiwa kuuwawa kutokana na kutofautiana na viongozi wa Chama,Mfano Zitto Kabwe aliwahi kuwatanabahisha Chadema kuwa hatokufa kirahisi kama alivyokufa Chacha Wangwe.Kwa maana kwamba Chadema hawawezi kumuua kirahisi kama walivyomuua Chaha Wangwe

Tatu kuwepo kwa visasi vinavyotokana na madhambi mengine.Wanasiasa kama walivyo raia wengine wapo wazinzi,wapo watu wanaodhulumu wenzao na wapo watu wasafi.Mambo ya uzinzi yanaohusiha kutembea na wake za watu kwa baadhi ya wanasiasa yameongezeka na kusababisha madhara makubwa hata mauaji.

Mara nyingi watu wamekua wakitekwa na kufanyiwa matendo mabaya na baadae kuja kugundulika ni visasi vya masuala ya uzinzi.Wapo watu wanaotekwa na kupigwa kwa kudhulumu watu wengine.

Matukio ya kutekwa watu yamekua yakitangazwa na viongozi wakuu wa kisiasa wakishirikiana na wanaharakati.Mfano wa matukio ambayo yamekua yakitangazwa ni lile la upotoshaji alilolitangaza Zitto Kabwe akishirikiana na wanaharakati Maria Sarungi na Fatma Karume juu ya kutekwa na wasijulikana Professor Asad.Matukio haya ya kutengeneza yamekua yakiwapa umaarufu viongozi hawa kutokana na kutokuchukuliwa hatua.

Wasiojulikana wanaweza kuwa wajejificha ndani ya vyama vya siasa,serikali na vyombo vyake vya usalama vifanye uchunguzi maalumu kuwatambua hawa watu.

==
Pia soma
- Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

- Tanzania sio Kisiwa cha amani tena, ni baada ya kufuga watu Wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Hivi wewe bado unawafikiria hawa wasiotakiwa wajulikane ukitaka kuwajua watu wasiojulikana dai tume huru ya uchaguzi maana tutawajua tu hata ikipita miaka 10
 
Ktk nchi ya Gambia Wasiojulikana ni watu ambao selikari yao wenyewe imewakabidhi au imewamilikisha silaha za kivita kwa maslahi ya kisiasa.

Na ktk awamu zilizopita nchini Gambia kundi hili la waliokabidhiwa silaha walipewa kazi ya ujambazi. Na kwasasa ujambazi wamesimamisha, ndio maana hutosikia ujambazi ukitokea, kwanini?!?! Kwa sababu wamepewa majukumu mapya. Majukumu hayo ni kuwanyamazisha wale wenye maoni tofauti na serikali nchini kwao.
 
Ktk nchi ya Gambia Wasiojulikana ni watu wasiojulikana ni wale ambao selikari yako wenyewe imewakabidhi au imewaomilikisha silaha za kivita kwa maslahi ya kisiasa.

Na ktk awamu zilizopita nchini Gambia kundi hili la waliokabidhiwa silaha waliopewa kazi ya ujambazi. Na kwasasa ujambazi wamesimamisha, ndio maana hutosikia ujambazi ukitokea, kwanini?!?! Kwa sababu wamepewa majukumu mapya. Majukumu hayo ni kuwanyamazisha wale wenye maoni tofauti na serikali nchini kwao.
Umilikishwaji wa silaha za kivita unafanywa hata kwa makundi kama blue guard na green guard,hoja yangu hapa inalenga kuwasaka hawa watu ndani ya vyama.Kuna watu ndani ya vyama waliona mafunzo ya kijeshi na wanatumika kuichafua serikali. Ni vema kuwakamata hawa watu ili nchi iwe na sifa nzuri
 
Ktk nchi ya Gambia Wasiojulikana ni watu wasiojulikana ni wale ambao selikari yako wenyewe imewakabidhi au imewaomilikisha silaha za kivita kwa maslahi ya kisiasa.

Na ktk awamu zilizopita nchini Gambia kundi hili la waliokabidhiwa silaha waliopewa kazi ya ujambazi. Na kwasasa ujambazi wamesimamisha, ndio maana hutosikia ujambazi ukitokea, kwanini?!?! Kwa sababu wamepewa majukumu mapya. Majukumu hayo ni kuwanyamazisha wale wenye maoni tofauti na serikali nchini kwao.
Nchini Gambi sio!
 
Back
Top Bottom