Leo Jumamosi 28.5.2016 ndio siku ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, michuano mikubwa kabisa na yenye uhondo wa pekee duniani kwa ngazi ya vilabu.
Fainali hii inazikutanisha timu mbili toka Spain na pia katika jiji moja la Madrid, ambapo Atletico Madrid uso kwa uso na Real Madrid pale katika uwanja wa Guiseppe Meazza au San Siro ndani ya jiji la Milan.
Atletico watachagizwa na wachezaji wao mahiri Griezmann,Torres, Koke, Saul huku idara ya ulinzi ikiwa chini ya jemedari Diego Godin.
Kwa upande wa Real wao watategemea zaidi Ronaldo, Bale, Modric bila kumsahau shujaa asiyeimbwa Casemiro.
Nani kucheka baada ya mpira kuisha kati ya Diego Simeone kocha mwenye mbinu za kukaba zaidi AU Zinedine Zidane kocha mwenye mbinu za kushambulia zaidi. Ikumbukwe hii ni mara ya pili timu za Madrid kukutana kwenye fainali hii ambapo mara ya kwanza Atletico alifungwa, Je leo watalipa kisasi??
Mechi ni saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki na itaonyeshwa kupitia Super Sport 3 ( SS3 ).
Tukutane hapa kwa live updates!!
cc:
Th Name Belo Jimena Aleyn everlenk PNC 1 rubaman Mentor na wengineoo
====================================================================
Full time:
*Real Madrid 1-1 Atletico Madrid ( After 120 minutes)
*Real Madrid won 5-3 on penalties.