UDA: Hatujafilisika na hatuna dalili za kufilisika

Mtoa mada kama anajua uimara wa kampuni ya UDA kiuchumi angetuwekea Balance sheet na cash flow yake ili tuweze kuamua kama kweli hawako njiani kufilisiwa.haitoshi kutuambia kuwa wamenunua mabasi 200 kwa mkopo wakati hawana assets za kutosha kurudisha mkopo kwa ajili ya huo uwekezaji.Ile miaka ya bora liende watu hawatahoji imepita na sasa majipu yote yatatumbuliwa tu bila hata ganzi.
 
HIVI Wadau Yale Mabasi Ya Mwendo Kasi Yamenunuliwa Na UDA Kwa PESA Zake Au MKOPO, Ama Zimenunuliwa Na Serikali!!!?? Maana Barabara Tumeambiwa Imejengwa Na Serikali Kwa MKOPO Toka World Bank!!! Na Sijui MKOPO Huo Atalipa Nani!!? SERIKALI Au SAIMON GROUP!!!? NAOMBA Mnisaidie KUNIJUZA WADAU!!
Mkuu hilo ni deni litakalo lipwa na wajukuu na vtukuu vyetu
 
U
Yeah , huu utetezi wa Simon ni mwepesi sana. Kwa uzito wa tetezi kwamba UDA inafilisika , halafu ukatoa statement kwamba siyo kweli bali mtaji umekuwa kwa asilimia 5.000% , ni maelezo mepesi sana.
Kuna usemi usemao kwamba " data" / Takwimu hazisemi uongo. Weka takwimu ambazo zitasema ukweli kuliko maneno matupu yasiyokidhi haja. Simon akumbuke kuwa lisemwalo lipo
UDA ni private company na haiwajibiki kutoa mahesabu yake kwenu public. So hii yote msemayo ni majungu tu. Hesabu za Air Tanzania ambalo ni shirika la umma, unazijua?
 
''UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015''

Uda ilikuwa na mali nyingi,sio mabasi kuukuu tu. Nafikiri mmetumia hati za mali ya UDA ..viwanja.majengo n.k..kukopea .Sasa hizo fedha mlizokopa ni shilingi ngapi. na zimetumikaje ? Haya ndo maswali mnayotakiwa kujibu.
 
Ajabu ni kwamba hakuna mwizi duniani ambaye hakuwahi kujulikana. Wezi wanafikiri hawajulikani, wako kama kenge anayekimbilia majini akikimbia matone ya mvua. Wizi ni uongo, it is a negative energy. It has limits. Huyu aliyesema za mwizi ni arobaini alimaanisha kuwa mwizi hawezi kusurvive milele. Hapa UDA ndio arobaini yenu imekaribia.
Sio imekaribia tu. Naona imefika.
Dalili zake ndo hizi. maneno meeengi.
 
Shirika limekuwa kwa sababu ya pesa mlizowaibia watanzania,wewe Kisena na genge lako la familia ya viongozi.
 
Taarifa haina thamani ya mtaji wa kampuni kabla na baada,madeni wala gharama za manunuzi za mitambo,tunaaminishwa tu kwa kutajiwa imekuwa kwa 5,000%.Ni kama mipasho fulani hivi..
HIVI HIZI HESABU ZA ASILIMIA ZINAISHIA ASILIMIA NGAPI?
 
hawa si ndio waligushi mahesabu na bado wakalipa kodi pungufu hii statement yao kama kawaida itakuwa imeandaliwa na mhasibu ambaye htambuliki na bodi ya uhasibu
 
Taarifa hii inadhibitisha jinsi gani shirika hili linavyoendeshwa kijanja janja.
Inawezekanaje kampuni kubwa kama wanavyosema kuruhusu taarifa ambayo ina mapungufu ya kiuandishi iletwe mtandaoni.
Siamini kama hii taarifa imehaririwa. Na kama ndio mwandaaji na aliyehariri elimu yake na umakini wake unatiliwa mashaka.
Naomba wakanushe tu kwamba hii taarifa sio ya kwao.
Kuna mifano mingi naweza kutoa ila naanza na mmoja tu.

Hivi mwandishi na aliyehariri hajui tofauti ya ajili na ajiri? mara kadhaa karudia " kwa ajiri"
 
Back
Top Bottom