Uchambuzi wa maudhui: Wimbo wa "Seduce me" by Ali Kiba

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,237
Ikiwa wimbo wa Seduce me ulioimbwa na msanii Alikiba umetimiza mwaka mmoja leo toka uachiwe leo ni vyema tukachambua maudhui ya wimbo huu.

MAPENZI

Mapenzi ndiyo dhamira kuu ya wimbo wa seduce me, ni wimbo unahusu mwanaume anayemueleza msichana anayejaribu kuibua hisia za mapenzi na msanii (Ali Kiba). Msanii ametumia maneno ya kiingereza "seduce me like..." akielezea hali ya kuonesha mwenendo wenye nia ya kuibusha hisia za mapenzi baina ya msanii na mwanamke husika. Msanii anatumia maneno kama "cheza kidogo", " zungusha kiuno chako nioneshe..."
Msanii anaenda mbali zaidi kueleza jinsi asivyotulia katika mapenzi kwani kwake kuhonga majumba na magari ni kitu cha kawaida sana. Msanii anasema "najua kupenda, nagawa mavumba"

Pia msanii anasema "Na kama unataka wananiita heartbreaker" majina mengine ni "kipusa" . Msanii anamtaka mwanamke wake kuwa makini kwani yeye ni "pasua kichwa" katika mapenzi "be carefully sister"

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII

Msanii anamwelezea mwanamke kama chombo cha starehe na mtu anayependa pesa na vitu vya thamani kutoka kwa mwanaume. Ndiyo maana msanii anakiri kuwa anahonga mavumba na magari kwa kila mtu. Msanii anaamini kuwa hiyo ndiyo njia itakayomsaidia kumpata huyo mwanamke.

UDHAIFU KIMAUDHUI

Msanii anaamini kuwa pesa, magari na majumba ndiyo njia sahihi ya kumpata mwanamke. Hii inajidhihirisha kwa msanii kukiri madhaifu yake ya kutotulia kwake akiamini kuwa pamoja na hayo yote mwanamke atakubaliana naye. Imani hii siyo tu inapotosha jamii bali inafanya mapenzi kuwa magumu kwa watu wasio na uwezo kiuchumi.

Pili msanii anahamasisha na kusifia matumizi mabaya ya pesa na mali kwa starehe. Msanii anajisifu kuwa wanamwita "misifa" kwa kuwa anagawa pesa, magari na majumba. Hii inahamasisha jamii kutapanya mali.

KUFAULU KWA MWANDISHI

Mwandishi ameongelea dhamira ya mapenzi ambayo ndiyo inayowavutia zaidi si vijana tu na wazee wa siku hizi ambao ndiyo sehemu kubwa ya mashabiki wake.

MAONI YA MHAKIKI

Mapenzi siyo pesa, majumba wala magari mapenzi ya kweli ni kupendana katika hali zote.
 
Bila shaka kila msoma post kimoyomoyo atakuwa amemkumbuka mwalimu wake wa kiswahili wa wakati huo
 
Hii ndiyo njia pekee ya kuongeza ufaulu kwa watoto wetu mashuleni waanze kuchambua fasihi simulizi baadala ya fasihi andishi kama hivi. Hongera, umenikumbusha sana, akina Kahigi Mulokozi na Kezilahabi.
 
Toa uo uchafu hapa,Leta uchambuzi wa vitabu vya fasihi Kama kilio chetu,watoto wa mama ntilie na vingine vingi ok be careful with your heart.
 
Back
Top Bottom