Uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM Taifa haki itendeke

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,104
2,549
Kuna taarifa kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais mstaafu Jakaya Kikwete ataachia madarakani hivi karibuni japo kwa shingo upande.Kuna taarifa pia mwenyekiti mpya atapatikana mwezi Juni mwaka huu pale utakapofanyika mkutano mkuu maalumu wa chama hicho.

Cha kusikitisha hakuna mchakato wowote wa kidemokrasi ulioanza mpaka sasa hivi wa wanachama kutangaziwa kuwania nafasi hiyo,kuchukua fomu,kutafuta wadhamini,kufanya kampeni nk! Kuna tetesi kwamba nafasi hiyo anataka kupewa Rais Magufuli eti ni utamaduni wa chama hicho Rais kukabidhiwa uenyekiti wa chama Taifa.

Kwenye katiba ya CCM hakuna kipengele kinachozungumzia utamaduni,CCM wapeni haki wanachama wenu kugombea nafasi wanayoitaka acheni figisu figisu.
 
 
Issue ya uenyekiti taifa ccm inaeleweka miaka yote, ya nini kushupalia shingo na sababu zipo tangu enzi za mwalimu J.K.
Hii mada haina miguu wala kichwa
 
Wacha ashike huyohuyo mzee wa majipu ili atumbue majipu sugu yaliyoko huko ccm maana tunaoumia ni wote wenyewe vyama na wasio na vyama
 
Mkuu unaweza kuwa point lakini hiyo point haiko sahihi!!
Utaratibu wa CCM uko wazi kabisa!
Mchakato wa kumpata mwenyekiti wa chama unaanza pale wana-CCM wanapochukua form za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa uraisi kupitia CCM! Hilo naamini unalifahamu fika japo unataka kupotosha watu hapa!! Ni mchakato huo unaoitwa wa kumtafuta mgombea uraisi kupitia CCM Na mwenyekiti ajae wa CCM ambao angalau unaakisi DEMOKRASIA kuliko mchakato wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania!
Sasa unaposema mchakato wa kumchagua mwenyekiti wa CCM kwa sasa sijui Kama umeshasahau ule mchakato wa kukatana pale Dodoma?? Ambako kuna jamaa alipokatwa akahama Na chama???
 
Mchakato wa kumpata mwenyekiti wa chama unaanza pale wana-CCM wanapochukua form za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa uraisi kupitia CCM! ...
Aisee? Kwa hiyo hakutakuwepo zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa mgombea uenyekiti kwa sababu tayari alishachukua na kurudisha wakati ule wa kugombea nafasi ya urais?
 
Mbona kipindi ya lowasa hakuacha wanachama tuamue?

Mna hofu na magufuli mnaanza kuleta figisu figisu.
 
Aisee? Kwa hiyo hakutakuwepo zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa mgombea uenyekiti kwa sababu tayari alishachukua na kurudisha wakati ule wa kugombea nafasi ya urais?
Hicho ulichoandika ndio jibu sahihi!
Hukutakiwa kuweka alama ya kuuliza kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…