Uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam kufanyika tarehe 22 Machi, 2016

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza Machi 22 kuwa ndiyo kitafanyika kikao cha Baraza la Madiwani wa Dar es Salaam kujadili ajenda moja ya uchaguzi wa meya.

Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM, katika Mahakama Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene hivi karibuni, alisema zuio hilo ni batili na kuagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya uchaguzi huo kabla ya Machi 25.

Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana alisema jana kuwa uchaguzi huo utafanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee.

Alisema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ikiwamo kusambaza barua kwa viongozi wa vyama husika na wajumbe watakaoshiriki kikao hicho
Huyo mjamaa ni kaimu kwani, yule jamaa anaitwa kabwe kwani alienda wapi maana kama vile ndo alikuwa mkurugenzi wa dar
 
tupe source ya taarifa yko mkuu....
IMG-20160316-WA0012.jpg
 
Sina Hakika ni kitu gani kinasababisha uchaguzi kupigwa danadana kiasi cha kufanana na mchezo wa sanaa ya kuigiza.
 
Hapa naona kuna tatizo, wamepanga katikati ya wiki Kimkakati, anaglieni sana muda wenu ndugu Ukawa, nafikiri kutakuwa na kamatakamata na kesi kuendelea. Ila haya ni maoni yangu.
 
Hapa naona kuna tatizo, wamepanga katikati ya wiki Kimkakati, anaglieni sana muda wenu ndugu Ukawa, nafikiri kutakuwa na kamatakamata na kesi kuendelea. Ila haya ni maoni yangu.
Halima Mdee,Kubenea,Waitara na wengine wanawezakua Mahakamani muda huo.
Siku ya jumamosi wameona haifai tena.
This is a booby trap!
 
Watakuwa wanahangaika bure kama mbinu ndo hiyo watakuwa wameshafeli
Hapa naona kuna tatizo, wamepanga katikati ya wiki Kimkakati, anaglieni sana muda wenu ndugu Ukawa, nafikiri kutakuwa na kamatakamata na kesi kuendelea. Ila haya ni maoni yangu.
 
Back
Top Bottom