Ubongo kids: Kipindi bora zaidi kwa watoto

Mwanangu anakipenda sana, nikirudi tu kazini anachukua simu anaangalia hicho kipindi, kina mafunzo mengi kwa mtoto.
 
Nampenda sana kibena na akili, sina hakika kama ni watu wawili tofauti coz huwa naona kama wanafanana
Usiombe unikute ninavyoiwahi akili (kwetu tunaiita hivyo hahahahaaaaaa)
Huyu jamaa Frank kajua kutushika hadi watu wazima.
 
Nimekuwa na mazoea ya kutazama kipindi hiki kila Jumamosi nikiwa na watoto wangu.Hakika wanangu wanakifurahia.

Na muda wa kipindi ukifika kama sipo nitatafutwa tu na hao watoto tutazame wote maana kikishaisha ni mrundikano wa maswali kutoka kwa watoto.

Kipindi hiki kimechochea udadisi wa kielimu kwa wanangu. Kinawasaidia kufahamu vile wasivyoelezwa kwa vitendo shuleni hasa baada ya mitaala ya elimu ya Msingi kuharibiwa vibaya sana.

Nawasihi wazazi wenzangu na watoto wenu kuhakikisha unaweka utaratibu wa kutazama vipindi hivi kila Jumamosi kupitia Channel ya TBC.

Pia mjitahidi mpate DVD za series za Ubongo kids.
Inasemekana hizo katuni zinatumia alama ya mapenzi ya jinsia moja alama ambayo ni Rainbow flag yaani bendera ya upinde wa mvua ambayo inafahamika duniani kote kuwakilisha mapenzi ya jinsia moja....sasa kama ni kweli hivyo vikatuni vina alama hiyo ni kwa kiasi gani watoto wetu wako salama? Je, hatuoni tunapromote mapenzi ya jinsia moja ikiwa hayo yanayosemwa ni kweli?
 
Nimejaribu kufananisha hizi TV programmes mbili za watotokwa mwanangu

Nikagundua anapendelea kuangalia barney and Friends kuliko Ubongo Kids ya nyumbani Bongo.

Nikazi kusupport cha nyumbani kisicho na quality

Nawaomba Ubongo Kids mjiongeze sana
Utakufa mdomo wazi aisee.... shame on you
 
Back
Top Bottom