Ghost MVP

JF-Expert Member
May 19, 2022
438
731
Hivi karibuni kumeibuka Hoja nyingi juu ya uhalali wa Risiti za EFD, kwa sasa EFD ndio risiti maalumu ya Bidhaa kuuza na kununua popote pale Nchini. Lakini risiti hizi zina utata kutokana na uhalali wake.

TRA wana tovuti ya kuhakiki risiti hizi za EFD ambayo ni TRA RISITI lakini asilimia 80% ya risiti ukijaribu kuzi-hakiki hazionekani kwenye mfumo wa TRA. hasahasa risiti za Mabasi ya Mikoni, risiti za bidhaa madukani(baadhi) risiti za huduma mbalimbali.

Je, huu ni ubadhirifu au upigaji pesa ambazo hazipo kwenye rekodi ya Mapato katik ataifa letu, kama risiti unayo na haipo TRA inamaanisha haijakatwa VAT na hivyo taifa linaingia hasara. tunaomba TRA Tanzania mtusaidie tupate uelewa zaidi kwenye issue hiii.

Mdau kama unarisiti ya EFD hapo ulipo angalie ilipoandikwa RECEIPT VERIFICATION CODE kisha ingia kwenye link hapo juu ya ku verify utupe screenshort inachokuambia


====

Pia soma: Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
 
Maduka mengi ya electronics kariakoo Hayana usajili wa VAT.

Ukionyesha msimamo, wanakwenda kuku chukulia "duka la pili"

Duka la pili=Muuzaji wa hizo efd risiti. Ndio kazi yake
 
Karibu tukuhudumie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…