Tuwashangae vijana au tumshangae Dr. magufuli?

Ndengaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
7,366
13,219
Wakati Mhe. Rais akidai kushangazwa na vijana kucheza Pool Table asubuhi. Je; Vijana nao waonyeshe mshangao wao kwake kwa kitendo chake cha kuwapa wastaafu ajira za ukuu wa mikoa huku wao na Degree zao wapo mtaani wanacheza pool table?
 
Wewe jamaa una akili nyingi sana na umewaza sana.. Kama said mek meksheli mkuu wa mkoa mpya wa kilimanjaro huyu angepumzishwa tu hana shida yoyote.. Mma kilango kama mbunge miaka kibao angeacha aende kumlea mzee malechela .. Kwanza kijana wao bilionea tupp downtown anazimake.. Kina vijana kibao ambao ni zaidi ya Makonda hawajapewa tu hizi opportunity.
Ccm ni ile ile
 
Kwa kweli ni shida, kijana una saluni, una stationary, una wedding au una biashara yeyote inayotegemea umeme asubuhi hakuna umeme hadi jioni afu hutakiwi uwe kwa pool, sasa wanataka hawa vijana wawe wapi?
 
Kiukweli mm sijawahi kumkubari huyu Jamaa anasema hapa kazi tu wakai wakuu wa mikoa walio wengi ni wastaafu. Mstaafu maana umri wa kazi umekwisha anawapisha vijana wafanye kazi.Sasa Lumumba buku saba watafanya kazi gani wakati kutwa wanashinda kwenye korido za Lumumba
 
Tafiti zinaonesha tuna tatizo la ajira linalotokana na kukosa ubunifu wa kujiajiri, kukosa mitaji, nafasi za ajira kushikiliwa na wanaotakiwa kupumzika au wenye vyeo zaidi ya kimoja, na kukosa miundo mbinu ya kiuchumi inayowafikia hata walio vijijini. Hatua muhimu inayopaswa kuchukuliwa na awamu hii ni kutatua hayo yote badala ya kulikuza lile moja la kukosa ubunifu ambalo kimsingi haliwahusu wote wasio na kazi. Na suluhisho siku zote linahitaji maono.
 
Tatizo la rais wetu anataka awe kama nyerere,
lakini huo wakati wa ukomunisti ulishapita zamani.

Hakuna tena mashamba ya kijiji kama enzi za sokoine kwamba vijana wataswagwa kwenda kulima
 
ifike wakati maswala kama hayo yakihuni huni yawe makosa na wanaokamatwa jela. huko kwenye pool vijana ndo wanatumia madawa na bhangi. pia ndo baadhi ya centre za majambazi.
USITEGEMEE KUWA KILA JAMBO LA MAENDELEO LITAKUSAIDIA BALI LITAKUUMIZA KWA UPANDE FULANI NA MATOKEO MAZURI BAADAE.
 

Kabisa mkuu. Swala la ubunifu linawahusu zaidi hao ambao ndio wameshikilia mamlaka na nafasi mabalimbali, wao ndio wanatakiwa wawe wabunifu zaidi, wao ndio wenye mamlaka na resources zilizopo, kwa hiyo wao ndio wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya hawa wasiokuwa na ajira wala kipato, lakini badala yake wazee wengi bado wameshikilia nafasi mbalimbali kwa karne kadhaa, lakini hakuna ubunifu wowote walionyesha kwenye hizo idara walizokalia, hakuna uazlishaji unaonekana, hakuna maendeleo, na kikubwa zaidi hawajasaidia kuzalisha ajira...na kwa aibu kabisa bado wanaendelea kushikilia hizo nafasi au kuzawadiwa mamlaka ya juu zaidi!!!!
 
Swali nikalime wap sina shamba sina mbegu sina jembe nikalime lami
 
Wakati Mhe. Rais akidai kushangazwa na vijana kucheza Pool Table asubuhi. Je; Vijana nao waonyeshe mshangao wao kwake kwa kitendo chake cha kuwapa wastaafu ajira za ukuu wa mikoa huku wao na Degree zao wapo mtaani wanacheza pool table?
Grow up. I believe someone like you was just attending classes bodily and finally came out of school with nothing between your ears. Truly, if you have a degree, must you wait for Magufuli to give you a job? I think education awakens the sleeping giant in you, that is creativity. So, if you have a genuine education you should be the last one to complain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…