Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,894
- 8,437
Binafsi nilikuwa nahisi kwamba Tundu Lissu anamchukia sana Hayati Magufuli hasa baada ya kile kisicho na ushahidi kuhusishwa kwake na Tukio la kushambuliwa Tundu Lissu.
Alichokifanya Tundu Lissu katika mazungumzo ya ufisadi wa bandari ya Dares salaam kuhusu JPM ni dhahiri kwanza hamchukii JPM pili ni mzalendo wa kweli, kitendo cha Lissu kusema Hayati Magufuli hahusiki na mikataba ya hovyo ya nchi yetu imeonyesha anamkubali linapokuja swala la uzalendo usiotia shaka katika kulinda rasilimali za nchi.
Tundu Lissu amebakiza kwenda Chato kulia kwenye kaburi la Magufuli na watanzania watamwamini na kumfanya awe Rais wao wa awamu ya 7.