Anthony Merinyo
Member
- Nov 11, 2009
- 27
- 8
Tundu Lissu is a member of Parliament just like Kigwangala. The parliament and the judicially are part of the government together with the executive. And this is the essence of democracy - the government of the people for the people and by the people through their representatives elected by the people.Does Tundu Lisu hold any position in a government as kigwangala!?
Our country is crumbling (trembling was understatement) as we speak and people like Lisu will only make things better than they currently are.
We all know why the government are afraid of him. He's real pain in a** to them. Unfortunately, they don't have any smart play left.
Government should let this associations Decide they're fate without any interventions.
Huruka--hulka......Bashite wengi CCM...Huruka/Tabia ya Lissu ndo inamfanya hafai kuiongoza TLS. Ataifanya TLS ni NGO ya CHADEMA, mwisho ivunjwe na serikali. He is just NOT the right person for the position !
We have other organs for that type of work such as the Tanzania Human Rights Society led by Lady Kisimbo.I'm mentally unrest for the kind of politics vs rule of law currently going on all over our territory! We need somebody from whatever organ (I suggest from TLS) to point a finger with resultant effect of separation of politics from rule of law! That person should have enough experience on both itches.
Lissu anafaa au hafai ilikuwa iamuliwe na wenye chama chao si serikali,ila naona viwanda vimeshindikana sasa tumeamua kuhangaika na vitu vidogo vidogo sanaHuruka/Tabia ya Lissu ndo inamfanya hafai kuiongoza TLS. Ataifanya TLS ni NGO ya CHADEMA, mwisho ivunjwe na serikali. He is just NOT the right person for the position !
Vote for Lisu you vote for democracy, you vote for another you vote for a dead law society. Be strong, be wise, be brave. Hatuna wanaume Tanzania?
Pambana lisu baba usijali maneno ya mbanduka ngozi inawezekana ugonjwa umehamia ndani ya ubongo,ubongo unabanduka kwa ndaniAnaandika Tundu Lissu
Waheshimiwa mawakili na wananchi wa nchi yetu. Nimesoma taarifa katika magazeti kadhaa ya leo kwamba Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison George Mwakyembe amenizuia kugombea nafasi ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS). Kama taarifa hizo ni za kweli basi naomba kuweka masuala yafuatayo wazi:
(1) Waziri wa Sheria na Katiba hana mamlaka yoyote, kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha TLS na kanuni zake, ya kuzuia ama kuruhusu mwanachama yeyote wa TLS kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya TLS. Hivyo, kama kweli Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo, basi huo utakuwa uthibitisho wa ama upungufu mkubwa wa uelewa wa Sheria au hulka ya ukiukaji wa sheria (culture of impunity) ambayo imeshamiri sana katika utawala huu wa sasa.
(2) Mamlaka pekee inayohusika na uchaguzi wa TLS ni Kamati ya Uteuzi (Nominations Committee) ambayo ilikwishafanya uteuzi wa wagombea wote kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa na Sheria na Kanuni za Uchaguzi za TLS. Mimi ni miongoni mwa wagombea ambao Kamati ya Uteuzi ilithibitisha kuwa na sifa na vigezo vya kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS. Kamati ya Uteuzi haijabadilisha na wala haiwezi tena kutengua uteuzi uliokwishafanyika kwa sababu za kisiasa kama za Dkt. Mwakyembe.
(3) TLS ni taasisi huru ya kitaaluma inayojitegemea na inayojiendesha yenyewe kwa mujibu wa Sheria na kanuni zake. TLS sio idara ya serikali au taasisi iliyoko chini ya mamlaka ya serikali au ya Waziri wa Katiba na Sheria au inayoitegemea serikali kwa namna yoyote ile katika kuendesha mambo yake. Uhuru huo wa TLS unatambuliwa na Sheria za Tanzania na mikataba wa kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama wake.
(4) Kwa vile mimi ni mgombea halali wa nafasi ya Rais wa TLS katika uchaguzi wa wiki ijayo, kwa sasa ninaendelea na kampeni za uchaguzi na nitaenda Arusha wiki ijayo kwa ajili hiyo.
(5) Kwa haya ya Dkt. Mwakyembe na kwa mengine ambayo yamejitokeza katika TLS siku za karibuni na ukimya wa wagombea wenzangu kuhusu masuala haya, ni wazi kwamba mimi ni mgombea pekee anayesimamia uhuru, heshima na hadhi ya TLS kama taasisi huru ya kitaaluma ya wanasheria katika uchaguzi huu. Mimi ni mgombea pekee anayeweza kuirudisha TLS katika misingi halisi ya kuanzishwa kwake na ya uwepo wake: kusimamia maslahi ya kitaaluma ya mawakili na kusimamia na kutetea utawala wa sheria. Mimi ni mgombea pekee ninayeweza kutetea maslahi ya mawakili kwa sababu sihitaji kuteuliwa na Rais kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Nawaombeni mniunge mkono kwa kunipa kura zenu mnamo siku ya uchaguzi tarehe 18 ijayo.Lissu