Tunashabikia kutumbua majipu, mtumbuaji naye kaambukizwa jipu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Wataalam wanasema kuwa jipu hutokana na mchafuko wa damu kwa lugha nyepesi ya kiswahili. ila kitaalamu majipu yanasababishwa na bakteria wanaoitwa Staphylococcus ambao wanakua juu ya ngozi na baadaye wanaingia ndani kupitia matundu ya vinyweleo/michubuko au jeraha. wataalam wengine wanasema kuwa majipu hayaambukizi na wengine wanasema yanaambukiza kutokana na hawa bakteria kuweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. nisiwachoshe na habari za kitaalamu zaidi.
magufuli aliingia na kauli mbiu yake ya kutumbua majipu. huyu ni kama mama ambaye watoto wake wengi wameathirika na majipu kiasi kwamba sasa amekuwa mtaalamu wa kutumbua majipu na amekuwa akitamba kijiji kizima kuwa yeye anatumbua majipu. kitu kimoja huyu mama anasahau ni kuwa anapoteza muda mwingi sana kutumbua majipu badala ya kutafuta nini chanzo cha hayo majipu?
ni aibu kama mama huyu atakuwa anatembea na pini/sindano standby akimwona mtoto anajipu anajisikia raha kumtumbua/kumkamua. lakini anashindwa kuelewa ni kwa nini familia yake wote wana majipu? je kama familia ina majipu haiwezekani naye akawa ni jipu? haiwezekanai naye akawa ni chanzo cha majipu? kiuhalisia kwa mama mwenye nia ya dhati ya kuisaidia familia yake asingesubiri tu aone jipu akatumbue. then akae tena litokee jipu akatumbue. angefikiria namna ya kukomesha kabisa majipu. na huwezi kukomesha majip kwa kuyakamua na kutumbua tu. wanasema pia majipu huwa yanatabia ya kuhama. kuna majibu yanayoweza hama usoni na kuhamia utosini au hata sehemu za siri.
haya ya sehemu za siri wengi huwa hawapendi kuyaweka wazi. so huyu mama mtumbuaji majipu je anatumbuaje haya? lakini na pia kuna ambayo huhama au huhamishwa kwenye harakati hizo za kutumbua majipu. huhamia sehemu nyingine ya mwili. je huyu mama anafanyaje katika hilo?
Dr Magufuli ni wakati wa kuangalia nini chanzo cha haya majipu. inawezekana ni mfumo wa chakula hapo kwenu, mazingira yenu, ustawi wenu,maisha yenu. sasa hali hiyo imetengeneza majipu kwa familia nzima nawe pia una kuwa na majipu lakini kwa kuwa huwezi tangaza kwa watu unabaki na majipu yako kimya kimya mpaka yanapokupasukia.
nini chanzo cha majipu? shughulika na mfumo huo ili usipoteze muda mwingi kutumbua majipu wakati kuna kazi nyingi za ujenzi wa taifa. na watanzania sasa wamekuwa standby wakisubiri kwa hamu kusikia nani tena anajipu akatumbuliwe. lakini isije ikawa wanaonekana sana kuwa na majipu ni watoto wa kambo lakini watoto wa mama mkamaji hawa hawakamuliwi au kutumbuliwa hadharani. ila hupewa dawa za kutuliza maumivu au kuyapoteza polepole huku wakiendelea na maisha yao kama kawaida.
ndiyo. mbona kuna watu walisemwa kuwa ni mizigo? wamerudi tena kwenye mfumo huu huu.. tulidhani kuwa sasa ungesafisha nyumba nzima na kuleta fenicha mpya ,nguo n.k kumbe lengo halikuwa hilo. lengo lilikuwa ni kuwatumbua watoto walioonekana kuwa si wako ili sasa uwalete watoto wako. tunajua huu ndio mfumo wa nyumba mbovu yoyote ile.
mama/baba komesha majipu kuanzia kwenye mzizi na pia tofautisha majipu na chunusi. tumefikia hatua watanzania hata ukimkamua mtu chunusi tunashangilia tunasema unatumbua majipu. mbona kuna majipu makubwa kabisa hujayagusa? hayo yanaonekana yamevimba sana na kuwa kansa katika ngozi za watoto wako na ndugu zako. hayo ungeyatumbua kwanza ungeachana na kukamua chunusi. halafu ungetafuta dawa ya kukomesha majipu.
 
Back
Top Bottom