Tunaishukuru serikali ya JPM, sasa bei ya sukari imeshuka hapa Dodoma

Ndugu zangu baada ya kupata shida ya muda mrefu sana kutokana na bei ya sukari kuwa juu sana mkoani Dodoma hatimaye bei ya sukari imeshuka ghafla kutoka 3000 hadi 2800 kwa kilo. Asante sana serikali ya Magufuli kwa kutukumbuka wanadodoma!!!
Hivi bei ya Choya pale Chadulu Mabasi Mawili itashuka au ndo itabaki ileile?
 
Hiyo tofauti ni ya kupongeza kweli? Really? Unakumbuka bei elekezi ni shilingi ngapi lakini??

Sawa tumesikia mkuu...ila hayo ndio matatizo ya ukada wa chama. Inaonekana mtu ukiwa "mfuasi nguli" wa chama cha siasa you risk big time to be enslaved in the way unavyofikiri, kuamua, kuona, ku-articulate, kuhukumu (judge) na kuongea juu ya mambo mbalimbali ya msingi na ya kitaifa.

Unaweza ujikute mtu na busara na akili zako unasifia au kuponda vitu ambavyo hata wewe mwenyewe mpaka unajishangaa kichwani kwako...implausible!! Tunaiona tofauti kubwa ya watu walivyo baada na kabla ya kuwa wanazi wa vyama vya siasa. Hii ni sababu kubwa inayofanya baadhi ya watu makini na ambao hawako tayari ku-surrender uwezo wao wa kufikiri na kutazama mambo kwa upana na uhalisia wake wawe wana sita sita sana kujiingiza kwenye active politics za kivyama. Vinginevyo, ukiwa ndani ya chama na mawazo tofauti lakini yenye lengo la kujenga utaitwa "msaliti".

Mimi nipo nipo kidogo kwenye huo unafiki wa siasa za kichama !! Spoken my mind...ngoja nisubiri povu sasa kutoka magharibi na mashariki.
 
Serekali tukufu ya ccm hongereni kwa kuwajal wananch Wa dodoma hizo ni fazila maana waliwachagua kwa kishindo sana
Lemutuzzzz atakuwa amefrah
 
Ndugu zangu baada ya kupata shida ya muda mrefu sana kutokana na bei ya sukari kuwa juu sana mkoani Dodoma hatimaye bei ya sukari imeshuka ghafla kutoka 3000 hadi 2800 kwa kilo. Asante sana serikali ya Magufuli kwa kutukumbuka wanadodoma!!!

huku kwetu mbeya ni 2500!!
 
2800/=unapongeza,, wakati sukari ilpanda kutoka 2000/= ,,kwa maamuzi yalikurupuka!
What did you just say?! Wewe utakuwa sio Mtanzania na ndio maana unashindwa kuona jitihada za Mtukufu Mheshimiwa Rais Tuliyeletewa na Mnyazi Mungu! Kutokana na upendo wake kwa watu hata wasio na shukurani kama wewe, Mtukufu Rais amefanikisha kushusha bei ya sukari kwa Sh. 200/= mziiima! Ni juzi tu hapa, ukiwa na elfu 3 unapata sukari peke yake but now, elf 3 ile ile unapata sukari kilo moja na fungu moja la matembele juu! Learn how to appreciate bhana kwanza ile sukari unayosema ilikuwa Sh.2000 haikuwa na ubora ile!
 
Wapinzani tujifunze kushukuru serikali hii ya chama cha mapinduzi inapofanya vizuri
 
Nilisema kuna wapumbavu watakuja kuishukuru Serikali kuwa imeshusha naona kuna omba omba wameshaanza
 
Ndugu zangu baada ya kupata shida ya muda mrefu sana kutokana na bei ya sukari kuwa juu sana mkoani Dodoma hatimaye bei ya sukari imeshuka ghafla kutoka 3000 hadi 2800 kwa kilo. Asante sana serikali ya Magufuli kwa kutukumbuka wanadodoma!!!
Utani wako ni wa ngumi na mkurupukaji
 
Jamani msameheni mtoa mada, hivi mtu anakula viwavi jeshi ,Kwel ataweza kunywa chai ?
 
Back
Top Bottom