Tunaendelea na Ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi Kwenye Sekondari Zetu - Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189

TUNAENDELEA NA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZETU

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, hadi leo hii lina jumla ya Sekondari 28. Kati ya hizo, 26 ni za Kata/Serikali na 2 ni za Binafsi (Madhehebu ya Dini). Tunajenga sekondari mpya kumi (10).

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameanzisha kampeni kabambe ya ujenzi wa maabara tatu (3) za masomo ya sayansi kwenye kila sekondari iliyoko Jimboni mwetu, zikiwemo zile za binafsi.

Wachangiaji wa ujenzi wa maabara:
Wachangiaji wakuu ni: Serikali yetu, Mfuko wa Jimbo, Mbunge wa Jimbo, Wanavijiji na Viongozi wao wakiwemo Madiwani.

Mafanikio ya kampeni hii:
(a) Sekondari zenye Maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia ni saba (7) - Bugwema, Bwai, Ekwabi (Wanyere), Ifulifu, Kiriba, Mugango na Nyakatende

(b) Sekondari zenye maabara mbili (2) na zinakamilisha maabara ya tatu ni tano (5) - Bulinga, Etaro, Makojo, Rusoli na Suguti

(c) Sekondari kumi na sita (16) zilizosalia zina maabara moja (1) hadi mbili (2) na zinaendelea na ujenzi wa maabara zilizokosekana.

Zipo Sekondari tatu (3) ambazo hazina maabara hata moja, nazo hizi zimeanza ujenzi wa maabara tatu.

Michango ya Wana-Musoma Vijijini:
Wazaliwa wa Musoma Vijijini na Wadau wengine wa Maendeleo wanaombwa kuchangia ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi kwenye sekondari zetu.

Wenye nia ya kuchangia wanaombwa wawasiliane na Viongozi wa Vijijini kwao, wakishindwa wawasiliane na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya yetu au Ofisi ya Mkurugenzi wetu (Musoma DC).

Picha ya hapa inaonesha:
Maabara ya Bwai Sekondari ikikamilishwa ujenzi wake.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 11.5.2024
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-10 at 22.32.06.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-10 at 22.32.06.jpeg
    48.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom