Wanajukwaa,
Wakati umefika sasa sisi Watanzania (Wazalendo) kumuunga mkono rais wa awamu ya tano Mh. JPM ktk suala la Wageni kuajiriwa hapa nchini huku wakifanya kazi ambazo Wazawa (i.e. Watanzania wanauwezo wa kuzifanya). Mfano: Wapo wageni wanaofanya kazi kama HR Officers na unakuta yeye ndo anaendesha mchakato wa Ajira kwa Wazawa. Yaani yeye ndo ana-make decision wewe Mtanzania upate ajira au usipate.
Sehemu nyingine hasa viwandani wapo wageni wanaofanya kazi kama technicians, wanachomelea ama kufanya kazi za kawaida sana kama kupeleka na kuchuka barua posta, kupeleka fedha bank, wapishi, kunua nyanya sokoni n.k. Halafu mbaya zaidi unakuta ni wachoyo sana hataki kabisa ku-share ujuzi na Watanzania. Yaani muda wote wanaongea lugha zao za kienyeji (Mf Kihindi maana siyo siri hili lipo wazi kabisa). Hata raia wa nchi za kiafrika wanatbia hiyo ya ubinafsi.
Hatupaswi kulifumbia macho hata kidogo maana ukiangalia kazi nyingi zinazotangazwa kwenye mitandao au magazeti ya nje, utakutana na condition (Masharti.... Must be a citizen). Yaani lazima awe raia wa nchi ile. Sisi huku wanaingia na kutoka kwa raha zao. Hii haikubaliki. Lazima kuwepo control ya kutosha.
Nampongeza sana Rais na Waziri wa Kazi Ajira na Vijana kwa kuliona hili na kuanza kulifanyia kazi. Naomba tuwasaidie waheshimiawa hawa kwa kuweka hapa Makampuni yenye kuajiri Wageni kwa kificho huku wakiwanyima Watanzania wenye sifa fursa ya kufanya kazi kwenye nchi yao. Maana wakienda kwenye nchi za wenzetu wataambiwa ooohh sio raia, ohh hawajui kiingereza, nk. Na sisi tuamke maana " ......chelewa chelewa huumiza matumbo".
Weka jina la kampuni hapa ili Vyombo vinavyohusika vichukue hatua stahiki Mara moja...
Nawasilisha.
Kabla hujatolea macho makampuni ya kigeni ambayo kimsingi wanaoyaendesha ndiyo wanaotayarisha vigezo vya ajira,iombe serikali yako sikivu inayoongozwa na "ngariba wa vijipu uchungu" ifufue viwanda ilivyoviuwa na vilivyogeuzwa maghala ya kuhifadhia bidhaa.
Haiingii akilini kwa serikali sikivu ya chama cha majipu(CCM)iuwe viwanda yenyewe,kisha iuwe Elimu,halafu iwalazimishe wawekezaji wa sekta ya viwanda wawaajiri watu wao ambao hawana sifa.
Serikali hii sikivu kabisa ya CCM iliyojipambanua kuwa inauchukia ufisadi na kwamba ipo katika mchakato wa kuunda mahakama ya mafisadi ili mafisadi wafungwe haraka kwa kifungo kisichozidi miezi sita,kisha wapelekwe kusafisha jiji ili kupambana na kipindupindu kwa muda wa miezi minne,kabla ya kuwabugudhi wawekezaji kwa kuwalazimisha kuwaajiri watu wasio na vigezo,ilipaswa iwekeze katika mapinduzi ya viwanda kwa kujenga viwanda vya kutosha ili izalishe ajira kwa wananchi wake badara ya kuwalazimisha wawekezaji kutoa ajira ambazo hata kama zikitolewa,bado hazikidhi mahitaji ya wasio na ajira nchini.
Ili ionekane kweli inawiwa na ukosefu wa ajira,inapaswa pia iwape kipaumbele wale vijana wa Masaki IT maarufu kwa jina la L46b7,ambao sasa hivi wamegeuka kero katika jamii kwa kuombaomba wakati walishiriki kikamilifu kupora haki ya Watanzania kubadili uongozi kupitia sanduku la kura.
Haiwezekani serikali inayohubiri injili ya Elimu bure kwa watu wake ili kutoa fursa ya kusoma na kujipatia fursa ya ajira hizo inazoziimba,leo hii inayakana mahubiri yake kwa kujenga matabaka ya upatikanaji wa Elimu,ndiyo,utahubirije Elimu bure na wakati huohuo ujitengee Shule 11 bora tena zingine zinazoendeshwa kwa kodi zetu mfano Shule ya Msingi Diamond ya DSM,ziwe za kulipia?Inawezekanaje uhubiri injili ambayo wewe mwenyewe huiamini? Mbona mawaziri wako wanaotokwa mishipa ya shingo Bungeni na kwenye majukwaa ya wadanganyika wanaselfika mitandaoni wakiwa wamebeba watoto wao wakiwa kwenye uniform za FEDHA SCHOOL?
Badala ya kutolea macho sekta za watu binafsi,serikali ianze utekelezaji wa ahadi ya kujenga viwanda ilivyoahidi nchi nzima wakati wa kampeni.Inachopaswa kufanya ni kuhakikisha wageni hao wanafuata sheria za nchi za kufanya Kazi na kuishi nchini,si kuwapangia wenye viwanda watu wa kuwaajiri.