Tumepigania HAKI yetu ya kuwakilisha nchi EALA, Kuna wanaotulaumu kwa kupigania haki yetu.

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Tumepigania HAKI yetu ya kugombea kuwakilisha nchi EALA Kwa kutumia njia zote sahihi Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Tukishinda na kupata haki hiyo tutashukuru. Tukishindwa na kukosa haki hiyo tutatii maamuzi ya Kamati ya Kanuni.

Kuna watu wanatulaumu kwa kupigania haki yetu. Tukishinda watasema tumebebwa na tukishindwa watasema tumebwagwa. Ndio binadamu walivyo, haswa binadamu wabinafsi, waliojaa chuki, husda na woga ( inferiority complex). Watu wa aina hii wanastahili jambo moja tu, KUWAPUUZA.

Sisi tumetumia njia za kikanuni kutafuta tunachoamini ni haki yetu, haki ya kugombea. Tutatii maamuzi ya vikao na kusonga mbele. Hii ni ' battle ' moja tu kati ya battles nyingi Sana zilizopo mbele yetu. Katika kila battle tunajifunza, tunakomazwa na tunaweka akiba Kwa battle za mbele. Wanaona kila battle ni Zero-Sum game na kwamba wanamaliza maneno yote dhidi ya wanaowaona ni adui zao Leo na kusahau adui mkubwa zaidi, tunawaona. Tunawatazama. Tunabonyea na kuwapisha.

Siku watakapoona uwiano wa 0.002 unahitajika katika VITA kubwa mbele yetu, tutapigana nao lakini ni lazima tutawakumbusha kuwa HUU NI MCHANGO wetu japo mdogo.

We move on. Kwa funzo lingine kubwa Sana kwenye harakati za kujenga Demokrasia ya Uhakika nchini kwetu

Zitto Kabwe

Kiongozi wa Chama
 

You always fight the wrong battle.
“Choose your battles wisely. After all, life isn't measured by how many times you stood up to fight. It's not winning battles that makes you happy, but it's how many times you turned away and chose to look into a better direction."
 
Taifa letu linahitaji wanasiasa wanaoamini ktk misingi, sio fursa. ACT wazalendo washukuru hata hizo kura laki moja ambazo mama Mghwira aliwapatia, funzo kubwa la uchaguzi wa mwaka 2015 ni kwamba watanzania wanataka wapinzani wafanye kazi pamoja.

Nampa pole ZZK kwakuwa yeye sio mpendwa wa rais kama ilivyokuwa awamu iliyopita. Awamu hii ni zamu ya profeseri Mapumba kupendwa. Asiposhirikiana na UKAWA ktk hili la EALA, atakuwa mpweke daima maana silaha zote za kuwaharibia UKAWA amepewa profeseri, chama twawala hawana cha kumpa. Akibahatika kupata, basi ataambulia mchuzi tu-nyama ni za Sakaya na 'mwenzi' wake.

Pole nyingine ni kutoendelea kupata madili ya NSSF kupitia kampuni zake za mfukoni.
 
Nimekuelewa kama vita hiyo unapigana against Chama Tawala.Ukitaka Chama tawala kutoa nafasi kwa vyama vilivyo na uwakilishi mdogo Bungeni.Maana.yake.badala ya kuchujua vitu 6 CCM ingechukua vitu 4 ,kimoja kingeenda Act na kingine NCCR.

Lakini Act mnataka.kunyang'anya kitu toka kwa Wapinzani wenzenu ndiyo maana hamueleweki.
 
Kimsingi jamaa ni mpuuzi na opportunistic, hyena syndrome
 
Unanifurahisha unaposema taifa linahitaji wanasiasa wanaoamini katika misingi siyo fursa. Hata hizo fursa zikiwepo zilenge kuleta umoja wa wapinzani kuliko kuleta migawanyiko. Uchaguzi Mkuu 2015, walitumia nguvu nyingi kubomoa wapinzani wenzao, uchaguzi mdogo wa Mbunge na madiwani pia walitumia nguvu nyingi kupunguza kura za wapinzani wenzao. Ifike mahala waamini ktk ushirikiano ili pale wanapokuwa na uungwaji mkono mkubwa vyama vingine pia viwaachie
 
we kenge kweli kwa hiyo CHADEMA ndio wenye haki na upinzani? kwa nini usiseme CHADEMA ndio wameshiriki kupunguza kura za ACT ? ACHENI UBINASI KENGE NYIE
 
CHADEMA hawa hawa waliomuhujumu Mtatiro mpaka akakosa ubunge? na aliemkosesha ubunge Mtatiro akazawadiwa ubunge wa viti maalum.....CHADEMA ni wabinafsi sana
 
Swali kwa ACT Wazalendo, wapinzani wana nafasi 2 za uwakilishi EALA ambazo pia mnazipigania kwa kuwa ni "haki yenu"; je, zilipatikanaje? Mbona mnapenda sana kuvuna msichopanda enyi watu? Wapande wengine mvune nyie; desturi za wapi hizo? Kuweni na aibu na appreciation japo kiduchu. No doubt, those guys were really traitors. Yaani tabia ziko dhahiri hadi leo; maslahi binafsi hata usipostahili.

Kama wale wengine waliacha chombo baharini katikati ya maadui leo wanapigania ruzuku. Wanasiasa na hususan "wapinzani" uchwara nchi hii ni kikwazo kikubwa cha nchi kusonga mbele kisiasa. Mnatia aibu sana halafu mkikosolewa mnajificha chini ya mwamvuli wa "tunaonewa" chini ya utetezi wa upande wa pili. Pumbaf!
 
Ruyagwa uko sawa,lakini kwa kua Chadema hili linawagusa,tegemea dharau, matusi na kejeri za kila aina.

Hawa ndo chadema,pole sana
 
Ruyagwa uko sawa,lakini kwa kua Chadema hili linawagusa,tegemea dharau, matusi na kejeri za kila aina.

Hawa ndo chadema,pole sana
Wako sawa? Jasho na gharama waingie wengine wao wajichumie kiulaini pasi hata kuwashirikisha walioingia gharama? Huu sasa ni zaidi ya umalaya.
 
Mawazo ya mkuu wa chama ni mazuri sana. Ila kwa vile Watanzania tunataka demokrasia bandia huwa hatutaki yale ya msingi.

Kama UKAWA wanaamini katika umoja wangewashirikisha wapinzani wote, si kukaa pekee yao na waseme wengine hawahitaji kuwa na uwakirishi. Ni kosa na kutotambua wengine ni urafi.

Tunaomba tuunge hatua hizi za ACT kwa vile zinapambana na demokrasia bandia ndani ya nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…