Tanzania au tuseme Afrika kwa ujumla tukiifananisha na Marekani, tunapata pengo la miaka 100 au 300, kiuchumi, kimaendeleo, elimu, siasa, technolojia, sayansi, ustawi wa jamii, afya nk.
Congratulates. We like your move, we admire your attempt when compared a third world country with one of the greatest country in the world, the giant United States of America.
Ndio maana wengine sisi tumebakia na hamu kubwa na fikra za Mwalimu Nyerere, upeo wake and elimu yake ya political science ilikuwa ni accurate and more practical. Katika kauli zake alituonya kujifananisha au kuji positioned kwenye mataifa makubwa na kutuhatarisha tunaweza kumezwa.
Tukijibu swali lako.
Tukilijibu swali lako kwa kufanisha Afrika na Marekani, tutajikuta kunajikashifu sisi wenyewe.
Utawala wa awamu ya 5 umekuwa kama suala la Sodom na Gomora, adhabu ya Mungu iliyokuja kuangamiza huo mji iliwakumba wabaya na wazuri.
Harakati na kombora la awamu ya 5 la kupigana na ufisadi lilitukumba waliokuwa wabaya na wazuri. Watakaoangalia nyuma, watajeuka mnara wa chumvi. Suala sasa ni mbele kwa mbele.
Tujipange kama Taifa, tujenge umoja wetu bila kujali tofauti zetu za kidini, kikabila au kisiasa.
Jukumu la kulijenga hili Taifa sio la la Mheshimiwa peke yake, ni la kila kitovu kilichozaliwa hapa Tanzania.
Tushirikiane, Mshikamano, Tujenge nia nzuri, Kutakiane mema na mazuri, muhimu kuengeza kasi ya Uzalendo na mapenzi ya watu wetu na ardhi yetu. Mungu atatubariki.
***Tukiirudisha Marekani miaka 100 iliyopita, ndio tunaona yaliyotokea Marekani miaka hiyo, ndio sasa yanatokea kwenye mataifa yetu hapa barani Afrika, ikiwa na pamoja kuzuia "Freedom of Speech", kufunga wahandishi wahabari, kukanyaga haki za Binaadamu, viwanda duni, viongozi wenye madaraka makubwa kufuatilia mambo madogo magodo na majungu ya mitaani yasiyokuwa na faida ya Taifa katika jamii ya Kimataifa, kupenda kupelekana majela bila hatia, kutoheshimu Umoja wa Mataifa na kushirikiana na waasi kama M23 au wabaguzi kama Israel nk.
DRC, Sudan ya Kusini, Burundi nk