Tumekosa ustaarabu katika kusitiri miili ya wenzetu

January 2016 nilipewa jukumu la kutafuta gari la kusafirisha mwili wa marehemu mmoja kutoka Arusha airport to mount meru hospital. Nikapiga simu nikatafuta ambulance. Dereva alipofika airport akakataa akasema ambulance haisafirishi maiti nitafute pickup. Hakunipa sababu ya kukataa, aliondoka bila kudai hela ya usumbufu huku akilalamika yeye aliambiwa ni mtu na sio maiti. Kwani maiti sio mtu?
 
Naomba nikupinge mleta uzi.
Ile ajali imetokea bila kupangwa na eneo ilipotokea ni mbali na makazi ya watu hata ukifuatilia kwa karibu utagundua waliohusika kuchomoa miili kutoka kwenye gari ni wasafiri waliokuta tukio limetokea hivyo hawakuwa na hizo nguo za kufunika miili ile.
Pili ni akili gani itakujia ya haraka kuusitiri mwili ingali kuna miili mingine inahitaji kuokolewa?
Binafsi nimewahi kushuhudia ajali na niliona jinsi gani watu hurukwa na ufahamu wanapookoa miili ya marehemu au majeruhi.
Kosa sio kusitiri bali ni kupiga picha za wafu/majeraha makubwa na kusambaza mitandaoni bila ruksa ya mamlaka husika.
 
Ufahamu wa wewe unaepost umekaa juu Ya kochi na aliesimama mbele Ya mwili wa marehemu (miili in reference Ya tukio la Arusha) ni Tofauti sana sikia tu haya matukio
 
Ufahamu wa wewe unaepost umekaa juu Ya kochi na aliesimama mbele Ya mwili wa marehemu (miili in reference Ya tukio la Arusha) ni Tofauti sana sikia tu haya matukio
Si kigezo cha kutofanyika stara katika kuhifadhi vizuri miili ya wapendwa wetu . Maiti thamani yake ni kama aliyekuwa hai
 
unaongea as if ni kitu kinachoweza kupanga, ndo mana ikaitwa ajali kwahiyo hata ushugulikaji wake unakuwa wa dharula
Mimi nasemea kwa siku zijazo kwani sijui kama ile ni dharula mkuu inabidi tuwe tunaiga kwa wenzetu wao huja ambulance
 
Kama sio picha hizo mngekuwa mnajadili nini ? Bora hizo picha zimeonekana ila kumbuka hizi picha wakatizinapigwa TBC ambao kimsingi ndo walipaswa kutuletea taarifa sahii wao walikuwa wakionyesha taarabu,kwahiyo mfumo mzima wakutoa na kupata habari nimbovu na hauvumiliki.Tv za Kenya walitoa muda wao nakufuatilia tukio lile lakini kwetu tunaviziana ata kwa mambo ya kitaifa kama haya tunapuuza alafu mnaleta adithi za abunwasi na falsafa feki HAPA KAZI TU.Ujinga huu na ubaguzi huu unaoendelea katika Taifa letu havivumiliki akifa mtawala vyombo vyote viko uko lakini Raia wamezidiwa ata wanyama,akifa faru tume inaundwa lakini akifa Raia mnamfunika na majani alafu mnalalamikia picha.Chunga sana unafiki wenu tenda haki kabla haijaja siku mbaya kwenu ambapo mtalua na kusaga meno.
 
Si kigezo cha kutofanyika stara katika kuhifadhi vizuri miili ya wapendwa wetu . Maiti thamani yake ni kama aliyekuwa hai
Mkuu msiba hauzoeleki na mfadhaiko ambao mtu humpata unaweza punguza weledi hata ktk jambo analofanya kama umeshawahi kutwa na hii situation sidhan kama utabishana nam na mm naamini they did the best they could kulingana na resource walizokuwa nazo
 
HII NI MADA YA KIPUMBAVU SIJAPATA KUONA...HILO ENEO LA MTO WA MBU KUFIKA KARATU NI MBALI NA MJINI...PIA HAO WATU WALIOFIKA KUTOA MSAADA TUWASHUKURU...KUMBUKA WAMETOA MAITI KUTOKA NDANI YA KORONGO REFU(SIJUI KAMA MTOA MADA UNALIFAHAMU)...PIA MAITI MOJA INAHITAJI GARI MOJA KIHESHIMA, SASA HAYO MAGARI 35 YANGETOKA WAPI KULE POLINI..HAPA UWANJANI TU HILO GARI LA JESHI LIMEBEBA MAITI ZAIDI YA 20( HILO LA PILI)....TUACHE MANENO MENGI TUWASHUKURU HATA HAO WANAKIJIJI CHA RHOTIA KWA MSAADA WALIOTOA...WAMAMA WALITOA KANGA NA VITENGE HADI VIKAISHA..
 
Nijuavyo mie kuna kitengo cha maafa. Kwa ufahamu wangu mdogo nilidhani moja ya shughuli zao ni kutoa vifaa ikiwa ni pamoja na huduma za kuwapeleka wahanga hospitalini mapema na kutoa huduma ya kwanza eneo la tukio na kuhakikisha wahanga wanapata matibabu/huduma mapema iwezekanavyo. Na ninafikiri kila mkoa una kitengo hiki. Lakini cha achabu wao huwa wa kwanza kufungua account ya maafa na kupokea rambirambi. Ngachoka kabsa
 
Muda mwingine Tuangalie Na vitendea kaz mahala husika je Vilikuwepo

Si Kira msaada anaokupa mtu Ni Mzur Mwingine ni wa kimaslai
 
Acheni kuwa watu wa lawama tu..... Mnaudhi. Hivi huko porini nguo za kufunika miili yote hiyo zingetoka wapi? Tuwashukuru wasamalia waliojitoa kunasua miili.

Wewe unayesema eti ambulance ingekuja una matatizo sio bure.
 
Nakubaliana na wewe asilimia zote.. Watanzania wengi wana moyo wa kusaidia wakati wa ajali. Lakini wengi hawajui nini cha kufanya wakati huo.

ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU

Umma upewe elimu inayohusiana na ajali na uokozi..
Picha nyingi zinapigwa na kusambazwa bila hata tahadhari wala kusitiri sehemu zisizostahili kuonekana.. Wengine wamefunikwa majani daah!

TCRA... Mamlaka husika where are you?? Ondosheni hizo picha kwenye mitandao ya kijamii
Hakuna kitu kilicho niumiza zaidi km kuona wamefunikwa majani! ina maana hawana thamani tena! Wenyeji wa eneo husika wameshindwa hata kutoa vpande vya kanga kweli? Inauma sana kw Kweli.
 
Mimi nafikiri wakati umefika wa mamlaka husika kupiga marufuku picha za ajali, majeruhi na wafu na kuziweka mitandaoni. Kuwe na adhabu kali kwa wote watakaokiuka hili. Tuwatendee haki majeruhi na wafu.

Ndugu wanaJF,

Katika ajali iliyotokea juzi Arusha,kila mtu atakubaliana nami kwamba utaratibu mzima uliotumika katika kuwasitiri wenzetu haukuwa mzuri na sahihi.Jana katika kipindi maalumu cha Clouds TV,mmoja wa wazazi pia alilalamikia hili.Maiti za watoto zilizivyotolewa kwenye korongo,wengine wana kiatu kimoja,wengine wana soksi moja mguuni na wengine nguo zao zimevuka kabisa.

Mbaya zaidi hata uondoshaji maiti eneo la tukio mpaka mortuary,kwa kutumia pick up na miili ya watoto imepandana hapakuwa na ustaarabu hata kidogo.Niombe tu mamlaka husika ijue kwamba,machungu ya mzazi yanaongezeka sana hasa baada ya kuona mwili wa mwanae ukiwa katika state ya namna hiii.

Mtoto wa mwenzio ni mwanao.
 
Back
Top Bottom