Tume ya vyuo vikuu (TCU) yatoa ufafanuzi kuhusu alama za kudahiliwa vyuoni

TCU walisema minimum entry qualifications kwa A levels 2014 & 2016 ni 4 points of course subjects( cutting off marks) equivalents na two Ds.
Wamefanya vizuri kutoa uwezekano wa mtu kuwa na 4 points kwa na ufaulu wa C +E.
Mara hii TCU iwe makini siyo kwa vigezo vya udahili tu lakini pia kwa kuwapeleka wanachuo kwenye vyuo vyenye sifa. Matatizo ya Kampala University kwa wanachuo wa MD na St Joseph campuses za Songea na Arusha yasijitoleze tena. Hata mkanganyiko wa Wanachuo wa UDOM Diploma special program nao isijirudie. TCU ni moderator wa viwango vya Elimu Tanzania- wakizembea Elimu ya Tanzania inakuwa mashakani.
 
a3344035f44bcac393c9d3d6a6789ab9.jpg
vipi kama ni A+F ? maana point hapo nina point tano,vipi na mimi nimo kwenye degree zijazo? total points=5
 
Sasa tofauti hapo ya tangazo lililopita na hili Jipya iko Wapi??
Cut off points ni zilezile 4 hawajapunguza Kitu lakini nashangaa watu Wanajishauwa Kwa Tangazo jipya!!

Wengi wanacheka na hapa C + E = 4 points.
ila nakumbusha tu: HIZO D + D na C + E ni MINIMUM ENTRY na Wala sio MAXIMUM ENTRY, nyinyi Ni Chaguo la 5, Kwahiyo Possibility Ya Kukosa Chuo ni Kubwa Zaidi Kuliko Kupata.

Possibility Ya Kupata Chuo iko Hivi:-
1) DIVISION ONE A-LEVEL
2) DIVISION TWO A-LEVEL (C + C + D) Points 8.
3) DIPLOMA HOLDERS (GPA > 3.5)
4) DIVISION TWO (C + D + D) Points 7.
5) DIVISION THREE (C + E, & D + D) Points 4.

Nyie endeleeni Kujishauwa tu wakati Nafasi Yenu ni Ya Tano Lala Salama.
Hebu weka matokeo ya diploma mwenye GPA ya 3. 5 na kuendelea then utaona ni jinsi gani diploma holder wanavyobanwa ili wabakie middle level workers
 
Aah wangetumia mfumo wa principals yaani minimum 2 principals unaenda chuo. Mambo ya points ni kubana watu wasiende chuo. Majority wako ns E sasa watakosesha wengi kwenda chuo. Halafu masomo ya sayansi ni magumu huwezi ukayaweka sawa na ya arts at least kwa sayansi wngechukua mpaka E
 
We ulihesabiwa masomo mangapi wakati unaenda chuo?.....unakoelekewa utauliza kwanini form four wanahesabu masomo 7 tu?
 
Point: wito kwa wazazi, mhimize watoto wasome Yale makimbination ya kusoma huku unasinzia ndo watatoka. Mf (HKL, HGK, HGE ) la sivyo ukimuacha asome PCB, EGM, PCM risiki ya kumwita ****** ni kubwa. Maana atapata D E au EEE halafu atapigwa chini. Hii ndio Tanzania ya viwanda bhana, tuliosoma PCB tunayaelewa maumivu acha wengine wabaki kushabikia
Mi mtoto wangu ksmwe hatasoma sayansi kwa staili hii ya ukokotoaji wa points no way. Atasoma SHE, HSG lakini sio PCB Au PCM atafelishwa na mtindo huu
 
Nisije nikakutukana bure. Website yao wameweka Matangazo Mawili, moja ilo jingine ndio lime mention OD 3.5 sijaliweka kwakua hakuna kilichobadirika na O.D haina utata. Poleni na GPA zenu za 2.7 mtaishia kua Technicians hadi kufa. Moron.
Uwe na hekima hebu ona hyo difference 2. 7 hadi 3. 5 ni asilimia ngapi hizo wameongeza? No naona lengo lao ni kubakisha watu wengi wawe middle level workers
 
Miye sijaelewa wanaitaji uwe na point 4.0 kwa ufaulu wako yani hata tu apate D+E+E au wanaitaji hizo point 4.0 zipatikane katika masomo mawili tu siyo masomo matatu kama nilivyoeleza hapo kuwa DEE na je GS vipi hawajaipa mkao tena?
 
Miye sijaelewa wanaitaji uwe na point 4.0 kwa ufaulu wako yani hata tu apate D+E+E au wanaitaji hizo point 4.0 zipatikane katika masomo mawili tu siyo masomo matatu kama nilivyoeleza hapo kuwa DEE na je GS vipi hawajaipa mkao tena?
Mawili katika masomo ya kombi yako.
 
Jamani kabla hamjaja kushangilia Tangazo la TCU kaa chini tafakari katika nafasi yako au ya mwanao au ya ndugu ako katika kwenda chuo! Wengi mnafurahia lakini naona mnafurahia huku mkiwa hamjaelewa nini cha kufanya au nini kinacho takiwa!!!

Ikumbukwe kuwa Wanaomba nafasi ya chuo sio wale walio maliza Form 6 mwaka 2016 hapana! Kuna walio maliza Form 6 nyuma ya 2016! Sasa basi unachoshangilia wewe katika Tangazo hili ni nini??

Labda niwakumbushe nyuma kidogo muone Tofauti ya sasa na Ya miaka ya nyuma kabla ya viwango hivi!!

Ikumbukwe kuwa MSIMAO WA TCU UMEBAKI PALE PALE WALA HAWAJABADIRISHA ILA WAMEFAFANUA MSIMAMO WAO!! SASA UNAFURAHIA UFAFANUSI WA MSIMAMO MKALI AU UNA FURAHIA NINI??

Miaka ya nyuma MINIMUM POINT (CUTTPOINT) ilikuwa ni point 2.0 yaani ukiwa na E,E unakua na point 2 kwamba utaenda chuo lakini hiyo ni minimum huwezi kuwa sawa na mtu mwenye C,C au D,D kwa miaka hiyo ambapo kimbilio la wengi ilikuwa ni kozi zile za extra!!

Lakini sahizi MINIMUM POINT (CUTT POINT) zimepanda kutoka 2.0 hadi 4.0 je huoni utofauti hapo kabla ya kushangilia??? Je iko wapi nafasi ya yule aliye maliza mika ya 2013 kurudi nyuma katika kwenda chuo ambaye alikuwa na E,E na alikuwa anasifa za kwenda chuo?

Sijui kama mnaangalia hicho kitu au mnafurahia kwa mwenye AEE wa mwaka 2016 kwenda chuo? Na usidanganye kuwa wewe una AEE una point 6 watakuconsider na wakamuacha mtu mwenye C,C au mtu mwenye B,C lazima waangalie umebalance vipi!! Ishu sio point zako wewe ishu wewe umebalance vipi ?

Pia Kwa mwenye Point 4.0 yeye chuo cha serikali kupata ni kuomba Mungu sana! Ni ukweli kuwa wenye ufaulu mzuri hupelekwa vyuo vya serikali na wale ndelindeli hupelekwa private ambako ada ni kubwa na solution huwa kuto kwenda chuo kusubiri mwaka unaofuata!!! Na mwisho wa siku yanakukuta haya!!

Guyz angalieni hichi kitu kwa jicho pana sio kukurupuka na kuja kufurahia hapa akati watu wengi wanumia kiutani tani hivi!

Asikudanganye Mtu wala usidanganyike wakati wa kuomba chuo Huwa kuna vitu viwili tifauti kuna Vigezo vya chuo kwamba chuo chetu tunataka wanafunzi gani na kuna ufaulu wa TCU unaweza kuwa una ufaulu wa TCU lakini huna ufaulu wa chuo fulani! Nitakupa mfano unielewe hapa namaanisha nini! TCU wanataka point 4.0 hizo minimum lakini chuo Kama Muhimbili labda wao wanataka point 6 hapo ndipo shida inapokuja TCU inakwambia unasifa za kwenda Muhimbili lakini Muhimbili wanakwambia huna sifa za kuwa hapa,je kimbilio lako wewe ni wapi? Ndo maana utaona wanakwambia DUE TO COMPITION sijui nini nini huko!!! Lakini kupitia hili la TCU watu watakuja kulia hapa na kuahirisha mwaka wengi tuuu!!

Asikudanganye mtu point 4.0 ni kwa masomo 2 lakini hayo masomo jitahidi ubalance sanaaaaaa uwe umebalance eti una A,F una Point 5 halafu unafurahia utakuja kulia hapa au una A,E una point 6 halafu unafurahia hapa utakuja kulia na kimbilio lako litakuwa ni vyuo vya private na utasoma kozi ambayo hukuipendaa!! Wekeni akiba ya Maneno Yenu!!! Waoneeni huruma walio walio ahirisha mwaka kwa matatizo mbalimbali kwani udahili wao kwenda chuo ni wa wasi wasi!!

Kwa watu wa diploma msijidanganye msimamo wa TCU unamaanisha umebaki pale pale lazima uwe na GPA 3.5 kitu ambacho sio kirahisi rahisi kukipata hasa kwenye Diploma Za afyaa,hawajafafanua wakiwa na maana hilo la GPA ya 3.5 limeeleweka!!

Enzi za kikwete angewateteeni lakini zama hizi hiyo means imepitishwa kwa kishindo!!

Shikamoo Ndalichako na sasa ni Wazi kuwa chuo kikuu sio kwa kila mtu bali ni kwa wachache!! Ni safi kwa maendeleo ya nchi lakini side effect ni vilio vikubwa kwa wengine!
 
Hiyo ya Diploma hawajatoa clarification bado.. Tusubiri Guide book mbona una mchecheto
Mkuu, fanya abortion tu. Hujaona au? Kwanza OD mnahitaji ufafanuzi wa nini? Swala ni GPA ya 3.5 period. Mlizoeshwa 2.7 mkienda vyuoni mna pwaya pwaya. Sasa vyuo wataviona wale bright tu. Wengine mkafanye u-Technician kwenye Halmashauri huko Kiteto.
 
Uwe na hekima hebu ona hyo difference 2. 7 hadi 3. 5 ni asilimia ngapi hizo wameongeza? No naona lengo lao ni kubakisha watu wengi wawe middle level workers
TUTUO sorry kiongozi. Kuna dogo alinichafua hapo juu ndio maana nikaja hivyo. Sorry.

Lakini kaka, unajua Diploma hawana Average GPA, wao wanaangalia GPA ya mwaka wa mwisho Tu. Sasa, hiyo tayari ni Advantage kwasababu GPA ya mwisho mtu anaweza kufanya makubwa ulichangia na masomo/module kama Projects ambazo zina units nyingi sana kwahiyo zinaongeza GPA ulipata A or B+.

Kiongozi, bila kufanya maamuzi magumu kama haya, nchi itaendelea kua na wataalamu fake.
 
Nawapa hongera waliofaulu vizuri(div 1&2) Kuna wenye div 3&4 wamenuna. Wapo wa div 3 wamekubali matokeo, wanajua watakwama mikopo hata wakichaguliwa. Wameridhika wakijua wamejitahidi kwa uwezo wao na kupata hicho walichopata licha ya mazingira magumu ya shule zetu. Japo wanaweza kuwa wanawajua wenzao fulani (na ni wengi) wamefaulu vizuri, watapata mikopo, lakini waliipata mitihani lakini hawakushikwa nayo!
 
Back
Top Bottom